Makampuni ya simu yadharau agizo la Serikali (TCRA)

Makampuni ya simu yadharau agizo la Serikali (TCRA)

Vodacom wana kiburi kwakuwa mfadhili wao mkuu ni serikali. Viongozi wote wa serikali na taasisi zake wanazo line za Vodacom, kila mwezi wanapewa vifurushi vya kutisha ambavyo hata wangetumia vipi hawawezi kuvimaliza ndani ya mwezi.

Hela wanayovuna Vodacom serikalini hata hawatuhitaji tena tunaotaka tutumie kifurushi cha sh 2,000 kwa wiki.
Dah aisee.Hivi ina Maana Kampuni ya Voda na Hao Tigo ni Wakubwa Kuliko Serikali? Mbona wanataka kumchefua Rais wetu ambaye Kaanza vyema sasa Malalamiko kama haya Watanzania si Wataanza kutuona Sisi CCM kama ni Wale wale tu.

Jamani wasaidizi wa Rais kama mnasoma hizi thread mwambieni Mama,au ndio mpo tena mmeanza kumharibia kwa kuwa yuko fire na anatupenda Watanzania?🤷🤷🙆🙆
 
Kwenye kusimamia utekelezaji wa matamko MEKO alitisha ijapokuwa nilitofautiana nae kwenye baadhi ya mambo..

Tangu Mama atoe 24hrs ya marekebisho ya vifurushi mpaka sasa hakuna kilichofanyika kwenye baadhi ya makampuni ya simu.

Mama utakua bora zaidi ya Meko kama utatoa Tamko na kusimamia UTEKELEZAJI WAKE.

Tabaka la chini tunaumia jamani.
 
Bado wanarudisha gharama zao za kuingizwa chaka na waziri
 
Habari Wakuu, Naona kuna Mitandao ya Simu hadi sasa ni kama wamekaidi Amri ya Serikali Kuhusu Vifurushi. Hivi Serikali nayo ndio imeamua Kuwafumbia macho?

Mfano wa Mitandao hiyo ni Vodacom,Tigo...Je Serikali Imeshindwa Kuwafatilia?
This is a litmus test to Samias' government.Jee,ina meno,au ni debe shinda?
 
Halotel ndo kwanza wakaweka mambo mapya wanayoyajua wao.

Ila kwa kfiupi kama wangekuwa wamakaidi maelekezo wangeshughulikiwa lakini ukiona yanayofanyika hakuna anayesema kuwa wamekosea na mamlaka zinawaacha,basi usiwaulize tena mitandao ya simu wanafanya nini bali ziulizwe mamlaka husika kwanini zimebariki hali hiyo.
 
Habari Wakuu, Naona kuna Mitandao ya Simu hadi sasa ni kama wamekaidi Amri ya Serikali Kuhusu Vifurushi. Hivi Serikali nayo ndio imeamua Kuwafumbia macho?

Mfano wa Mitandao hiyo ni Vodacom,Tigo...Je Serikali Imeshindwa Kuwafatilia?

It means the corporates are now running the show.
 
Acha TCRA wapambane na zimwi walilolitengeneza wao
 
Mamlaka ya Mawasiliano TCRA ilitangaza kuwa imesitisha Vifurushi Vipya kuanza Kutumika na kuahidi kuwa Vitarudishwa Vifurushi vya Zamani Baada ya Siku 4.

Leo ni Siku ya 5 lakini bado havijarudishwa na Makampuni yanaendelea Kutuibia.

Tunaiomba TCRA iyaagize mara Moja hayo Makampuni kutii Agizo lake Bahati mbaya sana WAZIRI husika yupo KIMYA
 
Wengiene wamerudisha lakini bado wamechakachua sio kama vya zamani na vingine wametoa kabisa.

Haya makampuni ni wajinga na wasipowajibishwa wananchi tutashangaa sana.

Cc: mama
 
Kuna kitu wanakitafuta
Tusije kulaumiana
President akianza kazi
 
INAONESHA JINSI GANI MAKAMPUNI YA SIMU CHINI YA BARAKA ZA TCRA YANAVYOZIDI KUTUNYONGA!
Screenshot_20210407-140318_1617793420427.jpg
 
Back
Top Bottom