Makampuni ya simu yadharau agizo la Serikali (TCRA)

Kampuni za Simu hazifanyii kazi Maagizo ya Mtandaoni.
 
Hawa tcra nao ni jipu... Yaani walikaa chini wakakubaliana na makampuni juu ya bei mpya.. kisha leo wanaamua kusitisha... Walipokubaliana mwanzo hawakuona kuwa bei hizo ni mzigo kwa mwananchi? Je wao sio sehemu ya jamii ya kitanzania? Maisha ya raia hawayajui? Hawa jamaa yafaa watupishe maana kazi imewashinda..
 
Kwa nn wakati huu?? Hembu nijibu kwa logic
Serikali / TCRA na Ndugulile wao walijifanya wanajali wanyonge na ili waonekane wanafanya kazi sana wakaja na masharti / bei elekezi kwamba kuanzia April lazima mitandao ifuate masharti hayo..., na sio kufuata tu bali hata tabia ya kubadilisha badilisha waiache..., na sio kwenye Bundle tu hata kwenye voice calls waliwapangia..., na hapa bado wanavuta pumzi ili na whatsapp call waipige pini (eti inapunguza mapato)

Hii nchi ya Ujima yenye Uchumi wa Kati wa kinadharia..., inayojifanya eti ni Free Market....
 
Kwanini tusiwekeze kwenye Ttcl yetu bhanaa tuiudumie kupitia budget yaetu ya serikali tutimue ma kampun yote haya kichef chef

hapana, ukifanya ivo makampuni mengine yataondoka kwenye ushindani na ndo apo utaanza kupangiwa bei kichefuchefu mda huo kunakua hakuna alternative! kwa mfano safaricom ya kenya na airtel ya kenya, GB 1 unanunua approximately kwa tsh 10,000 ya tanzania
 
Lazima wapewe barua rasimi na hapo ndipo ucheleweshaji unaweza kutokea

Naamini waliagizwa kwa maandishi na maamuzi yoyote ya kutengua maagizo ya awali lazima pia yawe ya maandishi.
.

kuna mtu nliongea nae jana ana kitengo kikubwa tigo alisema itachukua mda angalau wiki wapange vifurushi upya tena
 
Vifurushi haviwezi badilika kwa matamko ya kisiasa, isitoshe ni wao waliopandisha..
Endeleen kungoja, mtangoja milele
 
kuna mtu nliongea nae jana ana kitengo kikubwa tigo alisema itachukua mda angalau wiki wapange vifurushi upya tena
Wanapanga nini tena wakati walikuwa navyo, si warudishe tu vya zamani. Au ndio haturudi tena vile vifurushi vya zamani?
 
Halotel Bado hawajabadilisha aisee

1,000 ni 400 MB
3,000 ni 1.3 GB
 
Hivi unadhani huko core kwenye mitandao kuna button ya restore factory settings kama kwenye tecno?
 
Yashaanza kutekeleza
 

Kama imechukua miezi mitatu kufanya yale makosa kwanini ichukue mwezi mmoja kurekebisha?

Lakini kama dhamira ya Waziri ilikuwa kushusha gharama za vifurushi kufikia 1mb kwa Tsh 2-9!

 
Wanapanga nini tena wakati walikuwa navyo, si warudishe tu vya zamani. Au ndio haturudi tena vile vifurushi vya zamani?

probability ya kurudi vya zamani ni 0.0001% kutokana na yale mazungumzo, kuna uwezekano wamepewa oda watengeneza vipya ambavyo ni juu kidogo ya vya zamani
 
Eti wameendelea kuwaibia wananchi.... KWANI ALIYESABABISHA HUKO UNAKOITA KUIBIA WANANCHI NI NANI? WAO KABLA YA HUO UNAOUITA WIZI, WALIKUWA WANATOZA KIASI GANI? Serikali yetu, katika hili imekurupuka... MAKAMPUNI YA SIMU HUWA YANAHITAJI MUDA KUWEZA KUREKEBISHA PROGRAMS ZAO... Yaani TAMOKO limetoka jana, leo hii menu zote ziwe tayari...!!!!! Siyo kama kusaini cheki kiongozi...!! Hivi serikali imetoa bei elekezi kwa hayo mabadiriko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…