Makamu Mwenyekiti CCM, Mzee Mangula: Bagamoyo tuliahidi kujenga Gati sio Bandari

Makamu Mwenyekiti CCM, Mzee Mangula: Bagamoyo tuliahidi kujenga Gati sio Bandari

Memento

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2021
Posts
4,423
Reaction score
9,986
Mzee Mangula anasema kwenye ilani ya CCM 2020-25 hawakuahidi bandari ya bagamoyo bali waliahidi ghati tu.

Hivyo anashangaa mjadala wa ujenzi wa bandari bagamoyo unatoka wapi.

Mzee Mangula hapa nadhani wa kumuuliza zaidi ni mwenyekiti wake ambae alisema ana habari njema kuwa wamefufua mazungumzo mradi wa bandari Bagamoyo.

Huu mshangao wa mzee Mangula una walakini ndani yake.

Chini nimeweka video Mama Samia akisema ana habari njema kuhusu ujenzi wa bandari bagamoyo, ngoja tuone panapovuja.

---

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula amewataka Watanzania kutohangaika na upotoshaji unaofanya na baadhi ya watu mitandaoni kuhusu ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, na kwamba wamuache Rais Samia Suluhu Hassan afanye kazi yake ya kutekeleza mipango ya maendeleo.

Amesema hayo akizungumzia ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani ambapo amebainisha kuwa bandari hiyo haijapitishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya 2020-2025, hivyo hakuna sababu ya kuwapotosha wananchi, badala yake waunge mkono utekelezaji wa miradi iliyoahidiwa.

“Nashangaa huu mjadala unatokea wapi kwa kuwa mradi huo haupo. Hakuna haja ya watu kupotosha wananchi,” amesema Mangula akizungumza na Gazeti la Uhuru na kueleza kwamba kilichoahidiwa ni ujenzi wa gati ya Bagamoyo.

“Ipo miradi ya maboresho ya bandari, lakini kwa upande wa Bagamoyo kilichopitishwa ni ujenzi wa gati, sio bandari,” amesema Mangula.

Juni mwaka huu akizungumza na wafanyabiashara, Rais Samia Suluhu Hassan aliweka wazi kuwa serikali imeanza mazungumzo ya kufufua mradi wote wa bagamoyo ambao unajumuisha bandari na eneo la maalum la uwekezaji.

Akiwa madarakani, Hayati Rais John Magufuli alikataa kuendeleza mradi huo ambao mkataba wake ulisainiwa wakati wa uongozi wa mtangulizi wake, Rais Dkt. Jakaya Kikwete, kwa maelezo kwamba masharti yake hayakuwa rafiki na kwamba yangeliingiza Taifa matatizoni.

Nape Nnauye amjibu Mangula, ni Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo



Screenshot_20211130-151056.jpg
 
Bible inasema Maisha ya Mwanadamu ni miaka 70. Kuwaachia watu wafanye kazi beyond their life span ndiyo tatizo linapokuja.

Kama Mangula anajua kuna tatizo kwenye huo mradi si aseme wazi wazi tu. Yaani yeye ni mtu kweli wa kumuogopa Maza. God forbid!
 
Mbona aliyoandika Mzee Mangula ni tofauti kabisa na unayosema wewe? Weka ushahidi otherwise itakuwa unamlisha maneno
 
si sawa hata kidogo kuingia mikataba itakayo wafunga wajuku zetu ( tena wengine ambao hata bado hajazaliwa) kwa takriban miaka 99!

kwa kweli huu ni zaidi ya ufisadi????
 
Katiba mpya ilikuwemo katila ilani ya CCM ya mwaka 2015, Mangula mbona hajawahi kutwambia kwa nini CCM haikulazimisha serikali yake ilitekeleze hilo?
 
Bible inasema Maisha ya Mwanadamu ni miaka 70. Kuwaachia watu wafanye kazi beyond their life span ndiyo tatizo linapokuja.

Kama Mangula anajua kuna tatizo kwenye huo mradi si aseme wazi wazi tu. Yaani yeye ni mtu kweli wa kumuogopa Maza. God forbid!
Kizee kishenzi kwani yote aliyoyafanya Jiwe yalikuwa kwenye ilani? Kupoteza na kuua watu ,kununua wapinzani , kumpiga Lisu risasi kulikuwa kwenye ilani
 
Back
Top Bottom