Mzee Mangula anatambua vyema ubabaishaji wa chama chake cha CCM. Anatambua kuwa kwa muda mfupi amehudumu chini wa wenyeviti wawili tofauti wa chama chake.
Anatambua kuwa ijapokuwa wote wawili walikuwa ni mtu na makamu wake wa rais, na wote walishiriki kwa pamoja kuinadi ilani ya chama chao, lakini jambo la kuchangaza kwa sasa inadhihirika tofauti kubwa ya kimsimamo kati yao.
Hali hii ndiyo inamfanya kamarade Mangula kujaribu kuweka mambo sawa. Lakini inaonyesha kwa sasa Mwenyekiti Taifa aliyeko naye ameshaota mapambe, hutachelewa kusikia akiambiwa kuwa maoni yake ni "NONSENSE".
Mzee Mizengo Pinda eeeh! naomba uanze sasa kupiga jalamba, kutokana nguvu ya wapambe inakupasa kufanya hivyo. Naona imefika muda wako ya kutwaa mizigo ya kamarade Mangula.
Sent from my Nokia 2.3 using
JamiiForums mobile app