Makamu Mwenyekiti CCM, Mzee Mangula: Bagamoyo tuliahidi kujenga Gati sio Bandari

Mzee Mangula sumu aliyopewa ina mzingua.

Atueleze Chato Airport na daraja Busisi ni kwa Ilani ipi?
Mangula akumbuke kuwa Bogamoyo ni eneo la Sultan wa Oman, Sultan ndiye anayetoa pesa za ujenzi wa hiyo bandari. Mwacheni ajenge, watanganyika mkishindwa kulipa hilo deni atakuwa amerejirejeshea nchi yake iliyoporwa.
 
Halafu binafsi naamini ni CCM tu ndiyo itakayo tupa UKWELI wa suala hili la GHATI au BANDARI huko Bagamoyo na UKWELI juu ya aliyosema Kamanda wetu JPM kuhusu utata wa ujenzi na uwekezaji hapo Bagamoyo wa hiyo inayosemwa sasa na kupigiwa UPATU na kila mtu toka Serikalini hapo IKULU hadi huko BUNGENI, ambako wengi wao waliupinga sana huo Mradi, yaani walikubaliana na Kamanda wetu JPM LAKINI leo wamegeuka U -TURN na kuunga mkono Mradi huo na hapo hapo wakimkana Kamanda wetu JPM. What A SHAME ON THESE PEOPLE!
 
Haaaa tumekutana,Slender bridge ni ukurasa wa ngapi kwenye ilani.
Mzee Mangula wanamharibu
Mangula atutajie ukurasa ktk ilani ya ccm ambapo tutasoma ujenzi wa uwanja wa ndege chato, daraja la Busisi, mbuga ya burigi na uwanja wa mpira wa kubeba mashabiki laki moja huko chato.
 
Naomba video ya wakati Mheshimiwa Mzee Philip Mangula akiyazungumza haya, kwanza.

Ushahidi wa video ni muhimu sana.
 
Tukiwaambia ccm imesha pasuka, hamtuelewe.

Haya sasa, ngoma ndio kwanza imeanza.

Najua mama atapata wakati mgumu sana 2025
Ajiangalie jamaa asijewekewa sumu tena. Ila huyu mzee acha awekewe sumu tu. Nikikumbuka alivyokuwa anamuandama, kumfanyia figisu, madharau, majungu na kumtukanaga Rais Edward N Lowasa yani acha
 
Mangula akumbuke kuwa Bogamoyo ni eneo la Sultan wa Oman, Sultan ndiye anayetoa pesa za ujenzi wa hiyo bandari. Mwacheni ajenge, watanganyika mkishindwa kulipa hilo deni atakuwa amerejirejeshea nchi yake iliyoporwa.
Mbona mkataba wa miaka 99 tunaingia na Wachina?
 
Mzee wetu Mangula,Mungu akulinde.

Ni kweli haimo kwenye ilani ya CCM.
Sasa hivyi wanatekeleza ilani ya Msogagang,wazee wa tupatupa waliouza gesi,waliouza migodi kwa Bei Chee,maana ndo alikuwa waziri wa madini,wazee wa kujirusha,wazee wasiofikiri Mara mbili,wazee wa kushobokea Ulaya,wazee wa fitina.
 
Mzee Mangula anatambua vyema ubabaishaji wa chama chake cha CCM. Anatambua kuwa kwa muda mfupi amehudumu chini wa wenyeviti wawili tofauti wa chama chake.

Anatambua kuwa ijapokuwa wote wawili walikuwa ni mtu na makamu wake wa rais, na wote walishiriki kwa pamoja kuinadi ilani ya chama chao, lakini jambo la kuchangaza kwa sasa inadhihirika tofauti kubwa ya kimsimamo kati yao.

Hali hii ndiyo inamfanya kamarade Mangula kujaribu kuweka mambo sawa. Lakini inaonyesha kwa sasa Mwenyekiti Taifa aliyeko naye ameshaota mapambe, hutachelewa kusikia akiambiwa kuwa maoni yake ni "NONSENSE".

Mzee Mizengo Pinda eeeh! naomba uanze sasa kupiga jalamba, kutokana nguvu ya wapambe inakupasa kufanya hivyo. Naona imefika muda wako ya kutwaa mizigo ya kamarade Mangula.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Kina Mangula walishazoea kuwa na boss anayewatukana na kuwafokea, Na walimuogopa japo hawakumheshimu.
Sasa huyu anayesema "naomba" mfanye hili na lile wamesha m-reduce into nothing.
Alianza Pole Sasa wengine wanakuja kidogo kidogo.
 
Kura=Nonsense kwa mfumo wetu.
Atapita kwa 98%

Na hiki ndio kitu ambacho watanzania wengi hawakielewi..

Nchi hii ishakuwa Corrupted,, Kura ni ushahidi tu ili dunia isione sheria zimevunjwa...
 
asa hilo gati litakua na kazi gani bila kujengwa bandari?
 
Huyu mzee nae anachekesha, si kawaida ya CCM kujisifia wamefanya zaidi. Sasa haoni kuwa kujenga bandari badala ya wametekeleza, na wameenda mbali zaidi wanatakiwa kujipongeza na kupongezwa na CHADEMA. 😉😉😉😉
 
kabla jogoo halijawika tutakua tushapoteana mbaya.
 
Mambo ni moto ndani ya CCM, watu wanakwenda kugawana mbao, mwenyekiti (Samia) ameamua kupimana ubavu na makamu wake (Mangula) kisa mgawo wa 10% kwenye mradi wa Bagamoyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…