Makamu Mwenyekiti CCM, Mzee Mangula: Bagamoyo tuliahidi kujenga Gati sio Bandari

Jibu kwa Mzee Mangula mbona ni rahisi.

Ataambiwa huo mradi wa Bandari hauhusu ahadi za chama chao kwa vile ni mradi wa watu binafsi.

Hawa walioamua kuiuza nchi hawawezi kukosa majibu, hata kama hayaridhishi.
 
Ataambiwa huo mradi wa Bandari hauhusu ahadi za chama chao kwa vile ni mradi wa watu binafsi.
Ni mradi wa watu binafsi, au ni mradi ambao baada ya muda fulani tutatakiwa tuwe tumelipa gharama za kujenga mradi huo ili uwe wa taifa?!
 
Kwakweli , kama Mzee kikwete alisaini mkataba ule ukiwa na masharti Yale , anapaswa kuliomba msamaha taifa
 
Dogo kwanini unalazimisha kufananisha uzalendo na mambo hayo?
Mangula atutajie ukurasa ktk ilani ya ccm ambapo tutasoma ujenzi wa uwanja wa ndege chato, daraja la Busisi, mbuga ya burigi na uwanja wa mpira wa kubeba mashabiki laki moja huko chato.
 
Wana siasa kama wanasiasa. Katika ubora wao. Hii bandari naona kama itapata tabu sana kutokea. Inapingwa na inapingwa na inapingwa..kisirisiri na hata hadharani
 
Ni mradi wa watu binafsi, au ni mradi ambao baada ya muda fulani tutatakiwa tuwe tumelipa gharama za kujenga mradi huo ili uwe wa taifa?!
Huko ni baadae mkuu, mipango ya CCM ni ya muda maalum, mara nyingi ni miaka mitano, ikifuatia uchaguzi mkuu.
Hata hivyo Mzee Mangula atapewa sababu tu, si yeye ni Makamu; Mwenyekiti alishabariki mradi wenyewe.
 
Hili Gazeti la Uhuru halijakoma tu? Sina hakika kama maneno haya kayatoa Mangula kweli au vipi lakini Ilani ya CCM 2015-20, Ukurasa wa 66 (Toleo la Kiswahili), kifungu Na. 41(Usafiri wa Majini) (d) Kuanza Ujenzi wa Bandari Mpya za Bagamoyo na Mwambani Tanga. Labda Mangula angetuambia Bandari hii ishajengwa kama Ilani ilivyoahidi?
 
M
Mangula mnafiki sana yule mzee kama rangi yake. Si amuulize mwenyekiti wake wanafanya kazi ofisi moja?
 
Tukiwaambia ccm imesha pasuka, hamtuelewe.

Haya sasa, ngoma ndio kwanza imeanza.

Najua mama atapata wakati mgumu sana 2025
Hakuna kitu kama hicho as long as ameshima mpini hakuna mwamaccm wa kusema SU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…