Makamu Mwenyekiti CCM, Mzee Mangula: Bagamoyo tuliahidi kujenga Gati sio Bandari

Bible inasema Maisha ya Mwanadamu ni miaka 70. Kuwaachia watu wafanye kazi beyond their life span ndiyo tatizo linapokuja.

Kama Mangula anajua kuna tatizo kwenye huo mradi si aseme wazi wazi tu. Yaani yeye ni mtu kweli wa kumuogopa Maza. God forbid!
Sio kweli ni 120yra yakizidi sana.
 
Wenyeviti watatu,tangu kwa JK
Kauli ya JPM na CAG inamajibu,
Kauli zilizofuata zina maswali mengi kuliko majibu
1.Tupo kwenye mazungumzo kuona mapungufu yako wapi
2.Waziri,hakuna mkataba uliwahi sainiwa na hakuna nyaraka yoyote.
3.Ilani yetu inaonyesha kujenga gati.
Gati la nini?
Kwanini bunge huwa halichambui mikataba nakuwekwa wazi kama walivyofanya kwenye Tozo.
 
Mzee Mangula ana nafasi ya kumuona mwenyekiti wake muda wowote tena kwa jambo lolote.

Inashangaza mzee Mangula anaongea na waandiahi wa habari kupinga/kuhoji maagizo na maelekezo ya mwenyekiti wake kuhusu ujenzi wa bandari ya Bagamoyo .

Alichokifanya mzee Mangula siyo desturi, siyo utamaduni na ni kinyume na kanuni na taratibu za Chama Cha Mapinduzi.

Mzee Mangula aitwe, ahojiwe na apewe kalipio kali. Kama akikaidi avuliwe uanachama.
 
Tuliwaambia toka mwanzo watenganishe kofia hizi wakagoma, sasa unapata wapi nguvu ya kumpinga Mwenyekiti wako wa chama ambaye ndiye Rais wa nchi na amri jeshi mkuu nje ya vikao vya chama.

Huyu mzee naona waliomshauri wamekosea sana.
 
Mzee Mangula ana nafasi ya kumuona mwenyekiti wake muda wowote tena kwa jambo lolote.

Inashangaza mzee Mangula anaongea na waandiahi wa habari kupinga/kuhoji maagizo na maelekezo ya mwenyekiti wake kuhusu ujenzi wa bandari ya Bagamoyo...
Mwenye ni dhamu ndaninya ccm ni nani?
 
Tuliwaambia toka mwanzo watenganishe kofia hizi wakagoma, sasa unapata wapi nguvu ya kumpinga Mwenyekiti wako wa chama ambaye ndiye Rais wa nchi na amri jeshi mkuu nje ya vikao vya chama.

Huyu mzee naona waliomshauri wamekosea sana.
Kwa Taarifa yako Mangula anaweza kuanzisha vuguvugu la kumtoa Rais na likafanikiwa.
 
Kwa Taarifa yako Mangula anaweza kuanzisha vuguvugu la kumtoa Rais na likafanikiwa.
sahau ndugu, sahau kabisa, kwa mfumo wetu na katiba yetu Rais huwezi kumfanya chochote, sana sana utaishia kuumia.

Kama unabisha kamuulize Mzee Membe alikwama wapi kupiga kampeni hata moja, na majuzi kaomba kujisalimisha mwenyewe, mikono juu mwendo wa mateka.
 
Tuliwaambia toka mwanzo watenganishe kofia hizi wakagoma, sasa unapata wapi nguvu ya kumpinga Mwenyekiti wako wa chama ambaye ndiye Rais wa nchi na amri jeshi mkuu nje ya vikao vya chama.

Huyu mzee naona waliomshauri wamekosea sana.
Nyie jamaa bana, haya mambo ndio yalifanya jiwe akosee kabisa. Kina makamba na kinana walivyompinga aliwashughulikia Ila wote tulisema haikua sawa.
Sasa huyu nae mnataka apite njia hizohizo.
 
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† mzee Mangula hapimi alama za nyakati anafikili Mzee Mkapa bado yuko hai au Magufuli.

Anapaswa atambue kuwa waliopo na wenye nguvu chamani ni Mzee wa Msoga na Mama mwenyewe.

Hebu ajikumbushe bifu lake na Mzee wa Msoga lilivyokuwa mpaka ukatupwa nje ya ulingo.

Mzee Mangula acha hizo usije ukajiharibia wakati unafikia mwishoni, acha insurbodination kwa Mama, utaishia kubaya.
 
Sio kweli ni 120yra yakizidi sana.
Sawa Mkuu. Point yangu ni kwamba hawa Wazee hawana faida kwa Taifa.... Wamekuwa ni waoga kuliko hata watoto wa Form 2. This is not right.

Hata USA, wakati wa Trump former leaders wengi waliongea wazi walipoona Jamaa anapitiliza. Sasa kwetu wao ndiyo washangiliaji au wakizungumza, wanazungumzia nusu nusu tu ... Bitting around the bush.
 
Basi atulie
Ina maana ile imani tuliokua nayo kuwa kipindi Cha Samia watu watakua huru kutoa maoni yao imeishaisha?
Tunataka kusema jiwe alikuwa sahihi kuwashughulikia akina membe, kinana na makamba?
 
Kwa Taarifa yako Mangula anaweza kuanzisha vuguvugu la kumtoa Rais na likafanikiwa.
Weee! Atakifanyia wapi? Kwa nguvu gani?

Alisulubiwaga na Kikwete huyu mzee akaenda kulima nyanya kwao Matibhila Iringa huko. Mbona hakuthubutu kumwondoa Kikwete?
 
Yaelekea Mangula ni miongoni mwa lile kundi lililokua halitaki Hangaya awe Rais after Magufuli kufariki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…