PostGE2025 Makamu wa Rais Nchimbi: Tanzania ipo salama, mazungumzo ya MARIDHIANO kuanza

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi amesisitiza kuwa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imechukua hatua madhubuti za kulinda umoja wa kitaifa na kuhakikisha wananchi wanaishi kwa utawala wa sheria.

Kauli hiyo alitoa akiwa mwakilishi wa Rais Samia katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika kwa njia ya mtandao kutoka mkoani Dodoma.

Dkt. Nchimbi alibainisha kuwa moja ya dhamira kuu ya Rais Samia ni kuhakikisha mazungumzo ya maridhiano yanatekelezwa ipasavyo, ili Taifa liendelee kuwa na amani, mshikamano, na liwe mfano wa utulivu barani Afrika na duniani.

Aidha, Makamu wa Rais alihakikisha kuwa Tanzania ipo salama na tulivu, na tayari kuendelea kupokea wageni kutoka sehemu mbalimbali za dunia kwa manufaa ya pande zote.

​
 
20251108_154224.png
 
My way or the High Way....

Yaani Makubaliano ni Sisi tunapanga tunachokubali na wengine kazi yao ni kukubaliana na Sisi...; kama wasipokubali tutatafuta watakaokubali...

What's a Waste of Time.... by the way wakati tunasubiri maridhiano tungeanza kuwahukumu na kuwafunga wauaji
 
Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi amesisitiza kuwa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imechukua hatua madhubuti za kulinda umoja wa kitaifa na kuhakikisha wananchi wanaishi kwa utawala wa sheria.

Kauli hiyo alitoa akiwa mwakilishi wa Rais Samia katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika kwa njia ya mtandao kutoka mkoani Dodoma.

Dkt. Nchimbi alibainisha kuwa moja ya dhamira kuu ya Rais Samia ni kuhakikisha mazungumzo ya maridhiano yanatekelezwa ipasavyo, ili Taifa liendelee kuwa na amani, mshikamano, na liwe mfano wa utulivu barani Afrika na duniani.

Aidha, Makamu wa Rais alihakikisha kuwa Tanzania ipo salama na tulivu, na tayari kuendelea kupokea wageni kutoka sehemu mbalimbali za dunia kwa manufaa ya pande zote.
Mnaanzishaje mazungumzo huku mnakamata wapinzani na kuendelea kuwatesa acheni maigizo tukutane 9 December
 
Back
Top Bottom