PostGE2025 Makamu wa Rais Nchimbi: Tanzania ipo salama, mazungumzo ya MARIDHIANO kuanza

PostGE2025 Makamu wa Rais Nchimbi: Tanzania ipo salama, mazungumzo ya MARIDHIANO kuanza

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Maridhiano yalipaawa yawepo endapo ushindi ungetofautiana kwa asilia 1 mpaka 10.

Mfano: Samia 52% VS Lissu 49%.

Sasa ushindi wa 98% maridhiano ya nini?

Halafu waliogomea uchaguzi ni CHADEMA, viongozi wake wooote mmewasweka mahabusu kwa kesi nzito nzito za Uhaini!

Hayo maridhiano yanaenda kufanyika baina ya nani na nani? CCM na CHAUMA? CCM na ACT?

Sasa hapo si itakuwa ni sawa na kujipaka mafuta kwa mgongo wa chupa?

Kama wanataka maridhiano ya kweli, basi wenye kesi za uhaini wooote wafutiwe, viongozi wooote wa CHADEMA waachiwe huru na waruhusiwe kufanya siasa.

Hapo kidogo maridhiano yanaweza yakawepo na raia wanaweza wakawa soothed.
Wanawaona watu wote maboga tu,
 
Hayo maridhiano wakafanye na hawa majambazi.
20251104_120304.jpg
 
Mifumo haisomani.Huku viongozi wa CHADEMA wanasakwa wafunguliwe kesi zinazosemwa za mchongo,huku huyu anasema MARIDHIANO kuanza,kuanza na nani ilhali viongozi hao wa CHADEMA walisema hawataki baada ya uchaguzi eti ndo mseme maridhiano,kwanini msingerudhiana kabla?
Hofu ya kupoteza madaraka tu.
 
Baada ya kuua watu 3000+ wanataka maridhiano? serious? yeyote atakae kaa chini na CCM kuridhiana juu hili pia na yeye ni muuaji
 
Nchimbi umejipa laana kwa kushirikiana na shetani. Kwa damu ambazo shetani amezimwaga, jiuzulu ujitenge na shetani. La sivyo utavuna sawasawa na shetani unayemtumikia.

Wewe unazungmzia maridhiano, huyo shetani anazidi kuwateka na kuwabambikia watu kesi za uwongo.
 
Ila jamani tuache utani,Wamama wana huruma sana!Ila Rais wetu alishindwa hata kutoa pole ya kinafiki kwa Watanzania waliopoteza maisha wakati wa uchaguzi wa October!?
 
Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi amesisitiza kuwa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imechukua hatua madhubuti za kulinda umoja wa kitaifa na kuhakikisha wananchi wanaishi kwa utawala wa sheria.

Kauli hiyo alitoa akiwa mwakilishi wa Rais Samia katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika kwa njia ya mtandao kutoka mkoani Dodoma.

Dkt. Nchimbi alibainisha kuwa moja ya dhamira kuu ya Rais Samia ni kuhakikisha mazungumzo ya maridhiano yanatekelezwa ipasavyo, ili Taifa liendelee kuwa na amani, mshikamano, na liwe mfano wa utulivu barani Afrika na duniani.

Aidha, Makamu wa Rais alihakikisha kuwa Tanzania ipo salama na tulivu, na tayari kuendelea kupokea wageni kutoka sehemu mbalimbali za dunia kwa manufaa ya pande zote.
Kwenye operation tokomeza alikuwa Waziri wa Wizara ya Mambo ya ndani watu wengi sana waliuawa.

Wana maji wa kwale kufa maji mazoea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi amesisitiza kuwa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imechukua hatua madhubuti za kulinda umoja wa kitaifa na kuhakikisha wananchi wanaishi kwa utawala wa sheria.

Kauli hiyo alitoa akiwa mwakilishi wa Rais Samia katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika kwa njia ya mtandao kutoka mkoani Dodoma.

Dkt. Nchimbi alibainisha kuwa moja ya dhamira kuu ya Rais Samia ni kuhakikisha mazungumzo ya maridhiano yanatekelezwa ipasavyo, ili Taifa liendelee kuwa na amani, mshikamano, na liwe mfano wa utulivu barani Afrika na duniani.

Aidha, Makamu wa Rais alihakikisha kuwa Tanzania ipo salama na tulivu, na tayari kuendelea kupokea wageni kutoka sehemu mbalimbali za dunia kwa manufaa ya pande zote.
Wataridhiana na nani wakati wale wa chama kinachotakiwa wakae nao ndio hao polisi inawatia hatiani kwa kosa la uhaini
 
Back
Top Bottom