PostGE2025 Makamu wa Rais Nchimbi: Tanzania ipo salama, mazungumzo ya MARIDHIANO kuanza

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Huyu rafiki yake GT Mayor Quimby, anapenda sana misafara na ving'ora.
 
Hayo mazungumzo ya maridhiano mnazungumza na walioathirika au mnazungumza na vibaraka wenu wa upinzani??
 
Maridhiano yalipaawa yawepo endapo ushindi ungetofautiana kwa asilia 1 mpaka 10.

Mfano: Samia 52% VS Lissu 49%.

Sasa ushindi wa 98% maridhiano ya nini?

Halafu waliogomea uchaguzi ni CHADEMA, viongozi wake wooote mmewasweka mahabusu kwa kesi nzito nzito za Uhaini!

Hayo maridhiano yanaenda kufanyika baina ya nani na nani? CCM na CHAUMA? CCM na ACT?

Sasa hapo si itakuwa ni sawa na kujipaka mafuta kwa mgongo wa chupa?

Kama wanataka maridhiano ya kweli, basi wenye kesi za uhaini wooote wafutiwe, viongozi wooote wa CHADEMA waachiwe huru na waruhusiwe kufanya siasa.

Hapo kidogo maridhiano yanaweza yakawepo na raia wanaweza wakawa soothed.
 
Wewe ni mpuuzi sana
Unafurahia mateso ya watanganyika
Post nyiiingi
 
Kaenda huku kaacha huku Nyuma Polisiccm wanaendelea kukamata kamata hovyo watu kuwabambikia kesi za uhaini, Polisiccm wanazidisha chuki mara dufu, hayo maridhiano atamkuta nani nje?
 
Nasubiri kuona serikali itaridhiana na nani? Ushindi wa 97.66% na hakuna miongoni mwa wagombea waliolalamika kuhusu tukio la uchaguzi kwa wagombea 16, sasa maridhiano ya nini? Na nani? Kwa lengo gani?​
 
Nasubiri kuona serikali itaridhiana na nani? Ushindi wa 97.66% na hakuna miongoni mwa wagombea waliolalamika kuhusu tukio la uchaguzi kwa wagombea 16, sasa maridhiano ya nini? Na nani? Kwa lengo gani?​
Kura za mifukoni za Tume ya ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…