tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,786
- 4,494
Makamu wa Rais Samia Suluhu aikisalimiana na Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Dkt. Fredrick Shoo mara baada ya kuwasili kwenye Ibada ya Kuzindua Dayosisi ya Magharibi Kati na kumuweka Wakfu na kumuingiza kazini Askofu Mteule Dkt. Isaac Kissiri Laiser mkoani Tabora leo.
=====
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dk Frederick Shoo amemtaka askofu mteule, Isaac Laizer kusimama katika haki na asitawaliwe na kiburi cha madaraka.
Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Juni 10, 2018 katika ibada ya kumsimika askofu Laizer inayofanyika katika viwanja vya Kanisa la KKKT Magharibi Kati mkoani hapa.
Amesema asitokee mtu yeyote mwenye mamlaka akamrubuni na kujikuta anasahau kanisa na kumtaka atunze utakatifu na usafi wa kanisa na kufanya kazi kwa uaminifu.
Huku akinukuu maneno ya Mwalimu Julius Nyerere, Askofu Shoo amesema, “pale kanisa litakaposimama na watu wenye mamlaka na kumsahau mnyonge hilo halistahili kuwa kanisa na wala hastahili kuwa mtumishi wa Mungu.”
Amesema askofu Laizer anapaswa kuwa mnyenyekevu asitafute kuheshimiwa, kwa maelezo kuwa kama asipoheshimiwa na watu, basi ataheshimiwa na Mungu, “kheri uheshimiwa na Mungu kuliko mwanadamu.”
Amemtaka kutekeleza mambo matatu ambayo ni kutunza roho za watu, kumhudumia mwanadamu kiroho na kimwili pamoja na kutoa, kutetea haki na heshima ya mwanadamu hasa walio wanyonge na wanaoteseka.