Makanisa Nchini Mjitafakari

Alafu ukienda kutoa sadaka kanisani usichukulie kama umempa mchungaji we fanya kama umetoa kwa MUNGU ndio itakapo hesabika, wacha laana na adhabu ya MUNGU juu ya sadaka kutumiwa vibaya itawatafuina
Nichukulie hivi hapo Nitakuwa natumia Akili kweli. Yaani Nichukulie tu. Hiki ndicho kitu kinasemwa sana Na Wachungaji ili wawachote vizuri akili

[emoji835]Mungu hana Mikono kama Ulivyo wewe
[emoji835]Mungu hataki kitu kama Wewe unavyotaka taka Vitu
[emoji835]Mungu hataki chochote kile kutoka kwako.

Jiulize tu wewe hiyo mia 2 mpka Ma laki unayotoa Yanamuongozea nini Mungu kwa Mfano. Ila Hawa Miungu Mnaowapelekea huko kanisani ndio Yanachukia Usipoyapelekea Kitu na Yanachukia Pale unapokiwa hutoi Kitu maana Yanajua Kabisa kwamba Hizo sadaka haziendi kwa Mungu
 
Poa poa tutajua ukweli ukifa
 
Watakuja kukupinga maana walishajazwa upumbavu ,,,ila ukweli utabaki ulivyo sadaka ya kweli ni kusaidia yatima ,,wagonjwa na wajane,,pamoja na kujilinda na mabaya ya dunia,,,

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
 
Huu Uzi unahisu kutokutoa sadaka?, kama ndio.... sema... niendelee kusoma, hata Mimi sipendelei utitiri wa sadaka
 
Ni kuyafuta kama alivyofanya kagame, maana hakuna njia nyigine. Wanawake ndiyo wahanga wakubwa sijui wanatafuta nini kwa manabii uchwara!
 
Ni Kama Kuna ujumbe fulani Unataka kuufikisha lakini kwa andiko hili wengi watapoteza mwelekeo..! .

Wajue Ukweli

Mungu Katika Biblia ameagiza 'Nitoleeni Fungu la Kumi sababu hiyo ni haki yangu, na akaongeza nijaribuni Kwa njia hiyo Muone kama sitawafungulia madirisha ya Mbinguni.!

Mungu huyo umemjua anataka Fungu la Kumi baada ya Biblia Kuja. Kabla ya Hapo je Ulikuwa Huishi au Hao mababu zako waliokuzaa mpka leo Hii unajua Hiyo Biblia walikuwa Wanamtolea Nini?

Kuna sehemu ameagiza 'pandeni juu milimani mkalete miti mnijengee Kanisa...!
Yote hayo ili Jina Lake Litukuzwe..

Mungu haitaji Hayo Yote Mnajidanganya sana. Sasa Watu wakikataa Kujenga Atafanyaje..!!. Au ndio anashusha Moto kutoka Mbinguni kuwaunguza. Mungu hana Mahali pa Kukaa Hayo ni Mawazo ya Kumuumba Mungu katika Mawazo yenu ili mmfananishe na Binadamu. Kwahiyo Mungu akikaa Katika Kanisa Lako hilo Je Huko Kwingine kwenye Makanisa anakuwa amekaa Nani ?

Mmemfanya Mungu Binadamu. Mara Mungu anasikia..mara anakaa..mara anaongea.. mara ananena kwa Lugha.. mara Anatembea tembea... Mara Mkono wake ni Mkubwa.. Mara mmeuona Mkono wa Bwana haya ni Mawazo ya Kumtengeneza Mungu ambaye Hammjui





Sadaka Toeni kwa Binadamu nyie kwa Nyie Mungu haitaji Chochote kutoka Kwako huna Kitu cha Kumuonga Mungu akubariki. Maana Mungu alipokuumba alikupa Akili uitumie Mwenyewe kujitafutia Baraka Za Maisha. Kwa Mungu tunaomba Majala tu.

Hivyo Vingine hata Binadamu wasiomjua Huyo Mungu wako wanavyo na Wala Hawatikisikia wala Kutoa sadaka zako unazosema Ni Lazima. Kama Unapeleka Sadaka Kwa Mtu ili akuombee inajidanganya na Mtaendelea kuharibikiwa kila Siku na hata Nafuu hamtaiona
 
Ukisoma nyuzi za aina hii ndio hasa utaijua akili ya mwafrika ilivyo. No wonder ilikua rahisi sana kwa wazungu kututawala na kutufanya watumwa. Na hata leo wazungu wakitaka kurudi kutu colonize tena tutawapokea kwa mikono miwili. Waafrika mpaka tuje tujitambue ni miaka 1000 ijayo..!
 
Huu Uzi unahisu kutokutoa sadaka?, kama ndio.... sema... niendelee kusoma, hata Mimi sipendelei utitiri wa sadaka
Unahusu Njia Nzuri ya Kusaidiana Hapa Duniani kama Binadamu wenye Akili Timamu
 
Ukifa Huwezi jua Ukweli.

Unakuwa Mfu na Kwenye Biblia si wameandika Wafu hawaongei wala Wasikii jambo Lolote kwahiyo huwezi Jua Ukweli ukifa. Utajua Ukweli ukiwa Hapa unaona na Kusikia
Asikudanganye mtu ukifa ndio unakuwa kwenye real life hapo utateseka kwa matendo yako mwenyewe
 
Asikudanganye mtu ukifa ndio unakuwa kwenye real life hapo utateseka kwa matendo yako mwenyewe
Ushawahi simuliwa Hayo na Mtu aliyewahi kufa???

Kuna Watu wanakufa na Wanaenda Kuwa Misukule huko wakitumikishwa na Kutolewa ndimi zao . Hayo ndio Real Life unayoyasema. Au huyo Mtu akija ndio utamwambia Hivyo kwamba Alikuwa kwenye Real Life
 
Ushawahi simuliwa Hayo na Mtu aliyewahi kufa???

Kuna Watu wanakufa na Wanaenda Kuwa Misukule huko wakitumikishwa na Kutolewa ndimi zao . Hayo ndio Real Life unayoyasema. Au huyo Mtu akija ndio utamwambia Hivyo kwamba Alikuwa kwenye Real Life
hahahah Naona umeninukuu vibaya kmuu sikumaanisha hivyo
siongelei misukule bali watu waliokufa baada ya muda wao waliopangiwa na MUNGU kuisha
 
Wala huandikiwi dhambi kwa kutotoa sadaka ila unajikosesha baraka zako mwenyewe
Daaah Binadamu Mtakatifu Unajikosesha Baraka kwa Kutokutoa Sadaka kwa Hao Wa Kanisani!?

Mungu amekuuumba Kwamba usipompa Anakunyima Baraka! Yaani Mungu amekuumba Amekupa Uwezo wa kutengeza Pesa ila Ukimnyima hizo Pesa Anakunyima Baraka

Ungejiuliza kwanza Hata Washenzi..Wezi..Majambazi..malaya..Mafisadi.. Wachoyo wamepewa Baraka za Kuishi vizuri hapa Duniani kuliko wale ambao Hawafanyi madhambi hayo

Mungu amekuwekea Akili Hapo Ulipo baraka zako utazipata Ukitumia akili zako vizuri kutafuta Vitu. Hao wanaoiba ..wanafanya ufisadi .. wanaofanya uzinzi.. wote wanamtegemea Mungu ila Wanachokosa ni Kumtii Mungu basi
 
Pia hivyohivyo ila kwenye zaka ni laana zinakufuata na unazikosa baraka
Ngoja Nikuambie Kitu kimoja Ndugu yangu. Ulishajiuliza kwanini Kuna Mirundikano ya Michango ila Ina Badilika Majina Tu. Leo Sadaka.. Kesho Zaka. Kesho kutwa Harambee..Mwakani hiki na hiki n.k Ni njia ya Kukupumbaza Ili uone Mungu ndio anataka Kumbe Sivyo

Mungu hakuchukii usipotoa sadaka wala Zaka. Mungu hachukii Mtu Yeyote yule ni Wewe na Akili yako Keshakuumba . Hana Haja ya Kuhitaji Chochote kile angehitaji hayo Asingekuwa Mkamilifu Huyo Mungu maana Anahitaji vitu kutoka Kwako ili Akamilike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…