Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 12,463
- 27,556
- Thread starter
- #41
Yamkini mkuu kama unasema hapa naongopa njoo ulione kanisa lililo jirani yangu ni TAG(TANZANIA ASSEMBLY OF GOD) Ujionee kelele zinazopigwa kuna muda wanakuwa na ibada ya maombi jtano kuanzia saa2 usiku hadi saa6 mkuu hulali siku hiyo hadi wamalize ibada hiyo.Mtoa maada,tofautisha kati ya makanisa ya kilokole na makanisa ya watu binafsi.
Tanzania imekuwa na makanisa ya watu binafsi mengi sana,hayo utakuta analiendesha kanisa yeye mwenyewe anavyoona inafaa. Haya yana kelele sana kusema ukweli,yapo kati kati ya makazi, na muda mwingine hayana watu wengi ila kelele zinasikika mtaa mzima.
Kuna kanisa moja la mtu lilikuwa katikati ya makazi, wanachofanya wana modify tu nyumba ya kuishi inakuwa kanisa; jioni lilikuwa na ibada utakuta kuna watu wawili tu ila hilo kelele🙌🙌🙌 sjui hiyo ina maana gani kwa wenye wanajua?
Zaidi hadi kwenye mtaa limewahi ongelewa lakini hupunguza siku chache tu wanarudi pale pale.
Waumini wao walijenga hoja kuwa kelele za bar hatuzipingi ila kelele za kanisani tunaona kero!