Silvano Massawe (42) mkazi wa Kijiji cha Namwai Wilayani ya Siha mkoani hapa mkulima, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya wilaya na kusomewa shitaka la kumuingilia kinyume na maumbile mwanafunzi wa kike (13) kidato cha kwanza shule moja Wilayani humo, ambaye ni binti yake wa kuzaa.
Mwendesha mashitaka wa Serikali David Chisimba akisoma mashitaka mbele ya Hakimu mfawidhi wa Mahakama hiyo Elibahati Petro, amesema tukio hilo lilitokea Februari 21 mwaka huu katika Kijiji hicho.
Amesema siku ya tukio mwanafunzi huyo alikuwa nyumbani nyakati za mchana ambapo mshitakiwa alimuingilia kinyume na maumbile huku akifahamu fika kuwa kufanya hivyo ni jambo mbaya na ni kinyume na sheria.
"Amefanya kosa kinyume na kifungu namba 154 (1) (b) na (2) cha Sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022," amesema Chisimba.
Baada ya kusomewa mashitaka yake mshatikiwa huyo ameyakana yote lakini ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo amepelekwa rumande hadi 21 Machi mwaka huu atakapokuja kusomewa hoja za awali.
View attachment 2932368