Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20240312_063514_Opera%20Mini.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Christina Mndeme kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Machi 12, 2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.
Screenshot_20240312_064443_InstaPro%20.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali huku akimteua Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)- Bara, Anamringi Macha kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga.

Macha amewahi kuhudumu kama Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani humo.

Kwa uteuzi huo, huenda nafasi yake ndani ya CCM ikajazwa na mtu mwingine.

Screenshot_20240312_064542_InstaPro%20.jpg
 
Kennedy Musonda wa Yanga na Clatous Chama wa Simba ni miongoni mwa wachezaji 24 wa Zambia watakaoshiriki mashindano maalum ya kirafika yatakayofanyika baadaye mwezi huu huko Malawi.

Katika mashindano hayo, Zambia itacheza mechi tatu dhidi ya Malawi, Kenya na Zimbabwe.

Kocha wa Zambia, Avram Grant amewaita makipa Lawrence Mulenga, Charles Kalumba na Toaster Nsabata wakati mabeki ni Benedict Chepeshi, Zepheniah Phiri, Stoppila Sunzu, Frankie Musonda, Dominic Chanda, Gift Mphande na Kebson Kamanga.

Viungo ni Benson Sakala, Lubambo Musonda, Miguel Chaiwa, Emmanuel Banda, Frederick Mulambia, Joshua Mutale, Clatous Chama, Abraham Siankombo na Obino Chisala.

Kocha Grant ameita washambuliaji watano ambao ni Patson Daka, Kennedy Musonda, Andrew Phiri, Golden Mashata na Lameck Banda.

Screenshot_20240312_064648_InstaPro%20.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amemwagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo kuanza doria nyakati za usiku katika stendi ya mabasi Same mjini, ili kuwabaini na kuwakamata wanaotumia stendi hiyo kufanya mambo yasiyo na maadili.

Amesema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakilitumia eneo hilo la stendi vibaya na kwamba kila siku zimekuwa zikikutwa kondomu zilizotumika zimezagaa ndani ya stendi hiyo.

Mgeni ametoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika viwanja vya stendi hiyo, wakati akisikiliza kero mbalimbali za wananchi wa wilaya hiyo.

"Hili eneo la stendi kuna watu wanalitumia vibaya sana, tunakumbana na kondomu kila siku hapa stendi, kuna kitu gani kinafanyika hapa, OCD nikuombe fanya doria kamata wote weka ndani uwachukulie hatua kwa mujibu wa sheria," amesema DC Mgeni.

Ameongeza: "Wanatuharibia sana watoto wetu hapa Same, mimi kama mkuu wenu wa wilaya na mwakilishi wa Rais katika wilaya hii ya Same na kama mwanamke, nina uchungu sana na hawa watoto, niwaombe sana wazazi timizeni wajibu wenu,"

"Sitaki kusikia tena kuna kondomu hapa, na kila mzazi awe mlinzi wa mwenzake hata kama mzazi unaona yule mtoto sio wa kwako anarandaranda maeneo ya hapa stendi nyakati za usiku, mtoto wa mwenzake ni wa kwako, mweleze mzazi mwenzako usione kama una kiherehere unakuwa umeokoa taifa la kesho,"

Screenshot_20240312_064749_InstaPro%20.jpg
 
Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umekamilisha tathmini ya awali ya vihatarishi vya usalama na afya katika eneo la mradi wa kuzalisha umeme wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere (JNHP) lililopo Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.

Kifungu Na. 60 cha Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003, wamiliki au wasimamizi wa sehemu za kazi, wanawajibika kuhakikisha maeneo yao ya kazi yanafanyiwa tathmini ya vihatarishi vya usalama na afya walau mara moja kwa mwaka.

Lengo la tathmini hiyo ni kupata taarifa muhimu zinazohitajika, kuandaa mikakati madhubuti ya kulinda uwekezaji na kuwakinga wafanyakazi dhidi ya athari za vihatarishi katika eneo la kazi husika.

Taarifa ya kukamilika kwa tathmini hiyo imetolewa na OSHA kwa vyombo vya habari leo Machi 11, 2024 baada ya viongozi wa taasisi hiyo kufika eneo la mradi kama sehemu ya kukamilisha kazi hiyo ya tathmini.

Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda amesema mwaka 2022, Shirika la Umeme (Tanesco), liliiomba OSHA kufanya tathmini ya awali ya vihatarishi katika eneo la mradi na kutoa ushauri elekezi kuhusiana na uimarishaji wa mifumo ya kudhibiti vihatarishi mahali pa kazi.

Screenshot_20240312_064843_InstaPro%20.jpg
 
Silvano Massawe (42) mkazi wa Kijiji cha Namwai Wilayani ya Siha mkoani hapa mkulima, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya wilaya na kusomewa shitaka la kumuingilia kinyume na maumbile mwanafunzi wa kike (13) kidato cha kwanza shule moja Wilayani humo, ambaye ni binti yake wa kuzaa.

Mwendesha mashitaka wa Serikali David Chisimba akisoma mashitaka mbele ya Hakimu mfawidhi wa Mahakama hiyo Elibahati Petro, amesema tukio hilo lilitokea Februari 21 mwaka huu katika Kijiji hicho.

Amesema siku ya tukio mwanafunzi huyo alikuwa nyumbani nyakati za mchana ambapo mshitakiwa alimuingilia kinyume na maumbile huku akifahamu fika kuwa kufanya hivyo ni jambo mbaya na ni kinyume na sheria.

"Amefanya kosa kinyume na kifungu namba 154 (1) (b) na (2) cha Sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022," amesema Chisimba.

Baada ya kusomewa mashitaka yake mshatikiwa huyo ameyakana yote lakini ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo amepelekwa rumande hadi 21 Machi mwaka huu atakapokuja kusomewa hoja za awali.

Screenshot_20240312_064959_InstaPro%20.jpg
 
View attachment 2932368
Kifungo cha maisha kinamuhusu.
 
Back
Top Bottom