KELVIN DE BRUYNE ALIVYOISHI NA MSALITI THIBAUT COURTOIS.
Ni majira ya Kiangazi 2012 kwenye fukwe nzuri zenye barizi safi kama Mto Kilombero, Morogoro! Ndipo hapo panaitwa Ibiza huko nchini Hispania, nyota Kelvin De Bruyne akiwa na Mpenzi wake Caroline Lijnen, Mtalaam leo alitaka kutoa ukweli wa moyo wake ambao ulikuwa unamtesa wakati wote.
KDB aliketi vyema na kumwambia Mpenzi wake kuhusu usiku mmoja wa Kiangazi cha 2011 wakati alivyowaalika Caroline na Rafiki zake, ule usiku wa bata na starehe, kumbe KDB yeye alimzimia mmoja kati ya Mshemeji zake pale! Tungi zilikolea na maongezi yalizidi, Caroline akakata moto baada ya kuwaka sana.
Shemeji hakuwa mchoyo, alijisemea alichopewa na Mungu kumnyima Mwanaume dhambi! Shemeji hakuwa Mchoyo hakutaka kufa na utamu wake! Alimkaribisha KDB chumbani kwake na kuzima taa vyema! Shahidi ni shuka na kuta za hotel, feni ilizunguka 360 kama Bint wa Kizigua ama Kidigo, KDB Middle wa mpira hiyo siku alikuwa anacheza Middle kweli.
Utamu wa usaliti ule ukamfanya KDB amwambie Mpenzi wake ukweli kwa dhambi ile ya mwaka mmoja nyuma! Mwanamke akamwambia chagua kati yangu ama huyo! KDB akamchagua yeye Mpenzi wake na maisha hayakuwa hivyo tena kuanzia hapo, migogoro ilikuwa mingi na Mwanamke hakuwa na amani tena.
2014 Chelsea iliwatoa kwa mkopo Thibaut Cortois kuelekea Atletico Madrid na KDB alienda Ujerumani, ni Maswahiba wazuri na wote wanacheza timu ya taifa ya Ubelgiji! Sasa Caroline alikuwa na safari ya Madrid, akamtext Shemeji yake Cortois, wakaonana Jijini Madrid, Ushemeji ulinoga pale ambapo Kipa wa mpira alimpikia chakula kitamu sana Bibie.
Kwa maelezo yake alivutiwa sana na pishi la Cortois pale jikoni na akajikuta amevutiwa nae sana, ndipo hapo alipomtunuku burudani kitandani! Kisha nae akaenda kwa KDB na kumwambia nisamehe nimekucheat kwa Rafiki yako Thibaut Cortouis! Ugomvi ulikuwa mkubwa sana kati ya Wanasoka hao wawili kisa Utamu.
KDB aliitwa na Kocha wa Ubelgiji kama anahitaji amwite Thiba National Team ama wamteme? KDB akamwambia Kocha mjumuishe kipa wa mpira, mambo ya Utamu sio vitu vya kuharibu timu ya taifa, tutafanya kazi hakuna shaka! KDB hakutaka mambo ya UTI yaharibu taifa lao