Makapuku Forum

Makapuku Forum

[emoji599] JUST IN: Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ameamua kuwaita nyota wake wa kikosi cha kwanza aliokuwa amewapa mapumziko mafupi akiwamo Khalid Aucho, Pacome Zouzoua na Yao Kouassi.
.
Gamondi amewataka mastaa hao haraka kambini kujiandaa na mechi zijazo za mtoano za Mapinduzi.

………….
Screenshot_20240106_144827_Instagram.jpg
 
SIMBA KUSHUSHA MKATA UMEME
.
Mabosi wa Simba wanasema kazi ndo kwanza imeanza na sasa wamemgeukia kiungo Mkabaji anayejua boli kutoka Senegal [emoji1211] Babacar Sarr aliyewahi kuibuka mchezaji bora katika Mechi za Klabu Bingwa ya Nchi za Kiarabu Julai 31 mwaka jana wakati akiichezea US Monastir ya Tunisia.
.
Kiungo huyo mkabaji anayetumia vyema miguu yote mwenye umri wa miaka 26 yupo katika mazungumzo na mabosi wa Simba kuletwa ili kucheza kiungo ya chini kuituliza timu baada ya waliopo kama Mzamiru, Sadio Kanoute kushindwa kumpa anachotaka kocha Benchika.
.
Mbali na Sarr na jina la Erick Mbongossoum ambaye ni raia wa Chad, Chanzo changu ndani ya Simba kimesema kuwa uamuzi wa mwisho upo ndani ya saa 48 kuanzia leo ili kupitishwa kwa jina moja.
.
Screenshot_20240106_144959_Instagram.jpg
 
Hamas imelaani mashambulizi ya jeshi la Israel dhidi ya waumini wa Kipalestina na kuwazuia baadhi yao kuingia msikiti wa Al-Aqsa kwa swala ya Ijumaa kwa siku ya 13 mfululizo, wakidai ni kuwanyima uhuru wa kuabudu.

Katika taarifa kundi hilo limetoa wito kwa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuchukua jukumu lao la kulinda Jerusalem na Msikiti wa Al-Aqsa, dhidi ya kile ilichokitaja kuwa "hatari ya Uyahudi" na kuzuia ukiukaji wa haki ya Waislamu na Msikiti wa Al-Aqsa.

Shirika la habari la Reuters limesema kuwa, wanajeshi wa Israel leo wameimarisha ulinzi kwa ajili ya kuzuia Wapalestina wanaotaka kuswali katika Msikiti wa Al-Aqsa.

Kipande cha video ilichosambaza Reuters kilionyesha wanajeshi wa Israel wakiwa wamesimama nyuma ya vizuizi na kuwarudisha waumini nyuma kabla ya swala ya Ijumaa.

Screenshot_20240106_145133_Instagram.jpg
 
Klabu ya Borussia Dortmund ipo kwenye mchakato ya kuwania saini ya nyota wake wa zamani Jadon Sancho anayeichezea Manchester United.

Sancho (23) amekuwa na wakati mgumu tangu ajiunge na United akitokea Dortmund lakini mambo yameharibika zaidi ilipodaiwa kuwa na sintofahamu na kocha wake Erik ten Hag.

United haipo tayari kumuuza winga huyo lakini wamedai wapo tayari kumtoa kwa mkopo na kukataa kuweka kipengele cha kumuuza moja kwa moja hivyo italazimika kulipa sehemu kubwa ya mishahara ikiwa atarejea Dortmund kwa mkopo.
Screenshot_20240106_145239_Instagram.jpg
 
UKUTA WA KONGO LEO UNAONZA MECHI YA KIRAFIKI DHIDI YA ANGOLA.

Golikipa - Lionel Mpasi ( Rodez AF, France [emoji632])

Centre Back - Chancel Mbemba (Marseille, France [emoji632])
Centre Back - Henock Inonga (Simba, Tanzania [emoji1241])

Left Back - Arthur Masuaku ( Besiktas, Turkey [emoji1250])
Right Back - Gedeon Kalulu (Lorient, France [emoji632])

Kuna Mchezaji mmoja tu kutoka Ligi ya Afrika ndani ya Ukuta wa Kongo dhidi ya Angola.
Screenshot_20240106_150117_Instagram.jpg
 
THAMANI YA MKATABA WA EDWIN BALUA KWENDA SIMBA.

Kwa mujibu wa vyanzo vyangu amesaini kandarasi ya miaka mitatu ambapo Simba watalipa kiasi cha Million 150 (Signing fee) huku Prisons wakilipwa ikikadiriwa kama Million 25 (Transfer Fee).

Dili zuri??___
Screenshot_20240106_150244_Instagram.jpg
 
KELVIN DE BRUYNE ALIVYOISHI NA MSALITI THIBAUT COURTOIS.

Ni majira ya Kiangazi 2012 kwenye fukwe nzuri zenye barizi safi kama Mto Kilombero, Morogoro! Ndipo hapo panaitwa Ibiza huko nchini Hispania, nyota Kelvin De Bruyne akiwa na Mpenzi wake Caroline Lijnen, Mtalaam leo alitaka kutoa ukweli wa moyo wake ambao ulikuwa unamtesa wakati wote.

KDB aliketi vyema na kumwambia Mpenzi wake kuhusu usiku mmoja wa Kiangazi cha 2011 wakati alivyowaalika Caroline na Rafiki zake, ule usiku wa bata na starehe, kumbe KDB yeye alimzimia mmoja kati ya Mshemeji zake pale! Tungi zilikolea na maongezi yalizidi, Caroline akakata moto baada ya kuwaka sana.

Shemeji hakuwa mchoyo, alijisemea alichopewa na Mungu kumnyima Mwanaume dhambi! Shemeji hakuwa Mchoyo hakutaka kufa na utamu wake! Alimkaribisha KDB chumbani kwake na kuzima taa vyema! Shahidi ni shuka na kuta za hotel, feni ilizunguka 360 kama Bint wa Kizigua ama Kidigo, KDB Middle wa mpira hiyo siku alikuwa anacheza Middle kweli.

Utamu wa usaliti ule ukamfanya KDB amwambie Mpenzi wake ukweli kwa dhambi ile ya mwaka mmoja nyuma! Mwanamke akamwambia chagua kati yangu ama huyo! KDB akamchagua yeye Mpenzi wake na maisha hayakuwa hivyo tena kuanzia hapo, migogoro ilikuwa mingi na Mwanamke hakuwa na amani tena.

2014 Chelsea iliwatoa kwa mkopo Thibaut Cortois kuelekea Atletico Madrid na KDB alienda Ujerumani, ni Maswahiba wazuri na wote wanacheza timu ya taifa ya Ubelgiji! Sasa Caroline alikuwa na safari ya Madrid, akamtext Shemeji yake Cortois, wakaonana Jijini Madrid, Ushemeji ulinoga pale ambapo Kipa wa mpira alimpikia chakula kitamu sana Bibie.

Kwa maelezo yake alivutiwa sana na pishi la Cortois pale jikoni na akajikuta amevutiwa nae sana, ndipo hapo alipomtunuku burudani kitandani! Kisha nae akaenda kwa KDB na kumwambia nisamehe nimekucheat kwa Rafiki yako Thibaut Cortouis! Ugomvi ulikuwa mkubwa sana kati ya Wanasoka hao wawili kisa Utamu.

KDB aliitwa na Kocha wa Ubelgiji kama anahitaji amwite Thiba National Team ama wamteme? KDB akamwambia Kocha mjumuishe kipa wa mpira, mambo ya Utamu sio vitu vya kuharibu timu ya taifa, tutafanya kazi hakuna shaka! KDB hakutaka mambo ya UTI yaharibu taifa lao
Screenshot_20240106_150343_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom