Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 4,805
- 17,850
Mtakwimu mkuu wa serikali NBS, Dr. Albina Chuwa amewatahadharisha makarani kuwa hawatalipwa kiasi cha malipo kilichobaki endapo hawatafikisha kaya 100 kila mmoja, wakati akieleza mwenendo wa zoezi hilo tangu kuanza kwake mpaka hivi sasa. Amesema lengo ni kuhakikisha watu wote wanahesabiwa.
Dr. Chuwa amesema kama kuna karani amehesabu eneo lenye kaya pungufu, kuanzia 50-60 anatakiwa kwenda katika eneo jingine. "Karani asijikute kwamba eneo lake la kuhesabu watu lina kaya 50-60, akakaa akarelax, hapana, tulisema kwamba kama eneo lina kaya 50 au pungufu yu 50, lazima atakwenda kwenye eneo lingine, atakwenda kwenye eneo lingine, atakwenda katika eneo lingine, katika ileile kata, au kata nyingine kwa ajili ya kuharakisha kumaliza kazi hii mapema".
Zoezi hili la sensa litaendelea kwa siku 7 nchini, na sensa ya majengo itafanyika kwa siku 3.