Makarani wa sensa hawatalipwa malipo yaliyobaki kama hawatafikisha kaya 100 kila mmoja

Makarani wa sensa hawatalipwa malipo yaliyobaki kama hawatafikisha kaya 100 kila mmoja

  • Kama ni kweli, nadhani Sensa ya Majaribio nayo ilichakachuliwa au haikuandaliwa vizuri ikapelekea maandalizi yasiyo halisia.
  • Idadi ya makarani ni ndogo sana! Makarani kama laki 2 hivi wawafikie watu karibia 60 m kwa dodoso lile. Inatia shaka, hasa mashambani
Makarani ni wachache sana,haki ya Mungu,hawatafikisha hata asilimia 70 ya idadi yote,japo hela imetumika na inatumika nyingi.Kwa idadi ndogo ya makarani,naunga mkono suala la makaratasi kugawiwa na kukusanywa lingefanyika,sasa unawaza walishindwa kuwaza hivyo?
Ujingaujinga tu,hii nchi inaliwaliwa hovyo,watu tuna zaidi ya miaka mitano,hatuna ajira,zikija fursa wanagawana tu,na wakigawana hawafanyi kwa ufanisi,inauma sana.
 
Dah... Hawa watu washanikata stimu. Maana imebaki siku moja na ndani ya kishikwambi ndio kwanza nina kaya 35. Nafanyeje huku kwetu Makunduchi kupata kaya kumi kwa siku ni shughuli.
Mvivu wewe

Na huo muda wa kuingia humu, mchana wote huu unaupata wapi?
 
Ninazunguka mtaa walionipa nacheckcheck nyumba then naenda kukaa mwembeni na kishikwambi changu napika mapilau ya kutosha nawapelekea wale, Cha kufia na kishikwambi mkononi hataaa

Utapika utaweza?

Utagundulika tu.

Uzuri digitali inaonyesha kwenye ramani kila mtu alipo.

Na usisahau walishapita na kuweka nyumba hizo.

Utatrackiwa.
 
Kwani malipo kamili ya sensa yapo vp
 
Mvivu wewe

Na huo muda wa kuingia humu, mchana wote huu unaupata wapi?
Ndugu shida kuwa wewe huijui makunduchi. Kwa eneo nililopangiwa kaya moja hapa nyengine kilomita mbili ndani huko. Halafu unafika unakuta nyumba imefungwa na hakuna usafiri. Kwa mazingira kama hayo kama mia moja unadhani nitazifikia? Ndo pale unapoona upoze machungu kwa kishkwambi uingie
 
Back
Top Bottom