Makarani wa sensa hawatalipwa malipo yaliyobaki kama hawatafikisha kaya 100 kila mmoja

Kwahio na Kama nchi ambao tutakuwa hatujapata value for money kwa Kaya Zote kutokuhesabiwa nani atawajibishwa ?

Anna Makinda atarudisha Gharama iliyotumika ? Au Sensa itabidi irudiwe ?

Yaani hii statement inaleta sintofahamu..., yaani wanaona kutokuwalipa watu ndio suluhisho sio kuhakikisha kila kaya imehesabiwa..., au wanataka makarani waanze ku-cook data ?
 

Kumbe watu wanajulikana wapo milioni 60? Sasa tena sensa ni ya nini hii?
 
Kumbe watu wanajulikana wapo milioni 60? Sasa tena sensa ni ya nini hii?
Hayo ni makisio yangu tu jamaa; kila mtu ana makisio yake. Na Sensa za zama hizi ni zaidi ya idadi ya watu
 
Ndio maana nimeona Kuna makarani wanatumia pencel badala ya pen
Lengo wanijazie wenyewe au ndio utaratibu?
Inaruhusiwa ikiwa kama tablet imegoma, watawasilisha hilo dodoso
 

Sio wote wana namba za NIDA, mimi mwenyewe mkuu wa kaya lakini sina kitambulisho cha NIDA lakini tulihesabiwa! Pale kwenye NIDA anapika tu, anaweka dash!
 
Kwa nini sensa zilizopita hazikuwa na sarakasi au kelele nyingi kama hii??
 
Washawapiga kisaikolojia.

Yeye kama Mtakwimu mkuu analionaje hilo kwaaeneo ya vijijini hukoo ambapo nyumba moja kwenda nyingine ni kilometa tatu kwa uchache
 
Hili zoezi mbona lilikuwa na muda mrefu wa maandalizi, karani kwenda kila nyumba kuuliza hapa tayari au bando inaweza kumletea shida.
 
Nilijua tu. Hao ndio MABOSS wa Tanzania. Kazi zao huwa Ni kuwatishia watu huku wao hawajui chochote kinachoendelea.

Kifuatacho hapo Ni KUPIKA DATA kumfurahisha huyo a mpuuzi kama wanavyopika data za chanjo.
Na aliyefikisha kaya hizo mia ku relax kabisa na pengine kuacha kabisa kuhesabu
 
Kwa wito huu tunatafuta kupikwa kwa data feki ilimradi mtu afike idadi 100.
 
Hivi hawakufanya pretesting kuweza kujua kaya moja inachukuwa muda gani na kila msensa mmoja anatakiwa apewe kaya ngapi ili kuweza kumaliza kwa siku saba?
  • Trial ikifanyika kadiri ya taratibu, yawezekana haikwenda vyema sana ikapelekea maandalizi hafifu, au nchakato upatikanaji wa makarani haukuwezesha kupatikana watenda kazi bora n.k.
  • Kwenye utekelezaji halisi changamoto hazikosekani.
  • Kwa maoni yangu, ni vyema kusema kazi isipokamilika vyema makarani hawatolipwa. Piece work based pay hailetaji ubora, hasa kwa mtanzania.
 
Naona bado hao makarani wanaweza kufanya mchezo ilimradi wafikishe hizo kaya 100, hii sensa maandalizi yalifanyika muda mrefu lakini utekelezaji wake unavyokwenda ni kama vile hapakuwepo na maandalizi.
Kuna jambo lo lote kama taifa tulilowahi kufanya likafanyika kwa ufanisi na weledi?

Fomu hizi walitakiwa wapewe wakuu wa nyumba 10 waandikishe watu wanaokaa katika sehemu zao na makarani hawa wangeenda kuzikusanya tu na kuingiza data katika vishikwambi vyao. Lingekuwa zoezi rahisi sana na lisingekula Tsh. bilioni 600+ (usije kushangaa karibia nusu yake zimepigwa!)

Sasa hivi kuna uwezekano mkubwa wa kupata unreliable data.
 
Hili zoezi,wametunyima tu,ilitakiwa makarani tuwe wengi,kazi ifanyike hata siku mbili,sasa kifyatacho ni upikaji wa data,na maneno aliyotoa huyo mama,yatatumika kuwadhulumu baadhi ya makarani,siku ya mwisho.Watendaji,madiwani na viongozi wengine,watawakata pesa makarani.Hadi sasa,sidhani kama hata asilimia 50 imefikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…