Hongera na kongole kwa vijana wa BAVICHA maana bila kuwa na vijana walio na chachu ya mabadiliko kama waliopo CHADEMA nchi haiwezi kusonga mbele. Tunaona wenzetu kule UVCCM wao hawaongozi chochote zaidi ya kusifu na kuabudu huku kusubiri waletewe boom vyuo vya elimu ya juu ..
UMUHIMU WA JUKWAA HURU LA VIJANA
VIJANA WA TANZANIA KUANZISHA JUKWAA LAO HURU, NDIYO JIBU LA KUPATA NAFASI YA KUSHIRIKISHWA KTK NGAZI YA MAAMUZI KITAIFA
Duniani ni vijana wa vyuo vikuu ndiyo wanaoongoza kuchagiza mageuzi
Historia inaonesha mara baada ya uhuru wa kwanza kupatikana ktk mtaifa mbalimbalii iwe kwa mtutu wa bunduki au maandamano ya kuondoa wakoloni, baadaye kulifuatia msuguano wa wananchi wenyewe kwa wenyewe kwa kutoridhishwa na wale waliochukua utawala toka kwa wakoloni.
Sababu mbalimbali zilizua msuguano ktk nchi huru kama udiktekta, tawala kamdamizi ya chama kimoja, utawala mbovu, ubaguzi wa kielimu mfano mtoto aliyesoma shule za kata / st. Kayumba anadanganywa kuwa akihitimu chuo kikuu atakuwa na nafasi sawa na mwenzake aliyesoma St. Mary's akamaliza elimu ya chuo kikuu pia anayekimanya kiingereza / kispaniola vizuri zaidi na wajomba wake wapo ktk nafasi za kiutawala n.k
Vijana wengi pamoja na umasikini wa familia zao wanashawishiwa kwenda vyuo vikuu kwa kuchukua mikopo wakiwa na matumaini ambayo ni hadaa kuwa kwa kumaliza elimu ya juu watakuwa sawa na wale watoto wa tabaka la watawala anasema kiogozi wa vuguvugu la wanafunzi wa chuo kikuu wa Chile kamanda Gabriel Boric mwaka 2017.
Hapo ndipo Wanafunzi waliopo ktk nchi kama Sudan, Chile, Cuba, Afrika ya Kusini, Kenya walishiriki kudai mageuzi ili kuondokana na tawala zilizomgoa mkoloni.
Tanzania vijana hawajishughulishi kuhoji mambo yasiyowaridhishs wananchi kama matumizi mabaya ya kodi za wananchi, tozo ziluxokifu wananchi, demokrasia kubinywa, katiba kandamizi n.k
Chile nchi iliyo na kiongozi kijana Gabriel Boric ambaye ndiye rais kijana kabisa wa kuchaguliwa amezaliwa 11 February 1986 ambaye alichukua madaraka ya urais tarehe 11 March 2022 baada ya kushinda uchaguzi mkuu nchini Chile tarehe 19 December 2021 kwa kupata asilimia 60% ktk uchaguzi wa urais.
Gabriel Boric on the Chilean student movement 14 June 2017
Mwanafunzi wa chuo kikuu toka familia masikini anazama ktk mkondo wa madeni ya fedha za mkopo wa elimu ya juu huku akiwa na matumaini potofu ya kupata ajira au kuwepo mazingira hewa ya kujiajiri.
Vijana vyuo vikuu na mijini pia vijijini badala ya kumezwa na ukiritimba wa UVCCM na ahadi kuwa ni viongozi wa kesho huku watoto wa vigogo wa CCM wanapewa nafasi sasa na siyo kesho wanatakiwa kuunda chombo chao kipya cha kutambulika kama mdau muhimu anayehitaji kuonekana katika majukwaa ya siasa pia ktk vituo vya redio, televisheni na mitandao ya kijamii kuchagiza mabadiliko na mageuzi ikiwemo pia kupewa nafasi nje ya mfumo wa vyama ili wagombee nafasi za kuchaguliwa na wananchi.
time.com › collection › gabriel-boric
23 May 2022 · He is making Chile the social, economic, and political laboratory of the world once again. Stiglitz is a Nobel Prize–winning economist