Makato ya HESLB: Rais Samia tunaomba mrudishe makato ya 8%, pia yazingatie sheria ya kubaki na 1/3 ya basic salary

Makato ya HESLB: Rais Samia tunaomba mrudishe makato ya 8%, pia yazingatie sheria ya kubaki na 1/3 ya basic salary

Hongera na kongole kwa vijana wa BAVICHA maana bila kuwa na vijana walio na chachu ya mabadiliko kama waliopo CHADEMA nchi haiwezi kusonga mbele. Tunaona wenzetu kule UVCCM wao hawaongozi chochote zaidi ya kusifu na kuabudu huku kusubiri waletewe boom vyuo vya elimu ya juu ..

UMUHIMU WA JUKWAA HURU LA VIJANA

VIJANA WA TANZANIA KUANZISHA JUKWAA LAO HURU, NDIYO JIBU LA KUPATA NAFASI YA KUSHIRIKISHWA KTK NGAZI YA MAAMUZI KITAIFA

Duniani ni vijana wa vyuo vikuu ndiyo wanaoongoza kuchagiza mageuzi

Historia inaonesha mara baada ya uhuru wa kwanza kupatikana ktk mtaifa mbalimbalii iwe kwa mtutu wa bunduki au maandamano ya kuondoa wakoloni, baadaye kulifuatia msuguano wa wananchi wenyewe kwa wenyewe kwa kutoridhishwa na wale waliochukua utawala toka kwa wakoloni.

Sababu mbalimbali zilizua msuguano ktk nchi huru kama udiktekta, tawala kamdamizi ya chama kimoja, utawala mbovu, ubaguzi wa kielimu mfano mtoto aliyesoma shule za kata / st. Kayumba anadanganywa kuwa akihitimu chuo kikuu atakuwa na nafasi sawa na mwenzake aliyesoma St. Mary's akamaliza elimu ya chuo kikuu pia anayekimanya kiingereza / kispaniola vizuri zaidi na wajomba wake wapo ktk nafasi za kiutawala n.k

Vijana wengi pamoja na umasikini wa familia zao wanashawishiwa kwenda vyuo vikuu kwa kuchukua mikopo wakiwa na matumaini ambayo ni hadaa kuwa kwa kumaliza elimu ya juu watakuwa sawa na wale watoto wa tabaka la watawala anasema kiogozi wa vuguvugu la wanafunzi wa chuo kikuu wa Chile kamanda Gabriel Boric mwaka 2017.

Hapo ndipo Wanafunzi waliopo ktk nchi kama Sudan, Chile, Cuba, Afrika ya Kusini, Kenya walishiriki kudai mageuzi ili kuondokana na tawala zilizomgoa mkoloni.

Tanzania vijana hawajishughulishi kuhoji mambo yasiyowaridhishs wananchi kama matumizi mabaya ya kodi za wananchi, tozo ziluxokifu wananchi, demokrasia kubinywa, katiba kandamizi n.k

Chile nchi iliyo na kiongozi kijana Gabriel Boric ambaye ndiye rais kijana kabisa wa kuchaguliwa amezaliwa 11 February 1986 ambaye alichukua madaraka ya urais tarehe 11 March 2022 baada ya kushinda uchaguzi mkuu nchini Chile tarehe 19 December 2021 kwa kupata asilimia 60% ktk uchaguzi wa urais.

Gabriel Boric on the Chilean student movement 14 June 2017

Mwanafunzi wa chuo kikuu toka familia masikini anazama ktk mkondo wa madeni ya fedha za mkopo wa elimu ya juu huku akiwa na matumaini potofu ya kupata ajira au kuwepo mazingira hewa ya kujiajiri.

Vijana vyuo vikuu na mijini pia vijijini badala ya kumezwa na ukiritimba wa UVCCM na ahadi kuwa ni viongozi wa kesho huku watoto wa vigogo wa CCM wanapewa nafasi sasa na siyo kesho wanatakiwa kuunda chombo chao kipya cha kutambulika kama mdau muhimu anayehitaji kuonekana katika majukwaa ya siasa pia ktk vituo vya redio, televisheni na mitandao ya kijamii kuchagiza mabadiliko na mageuzi ikiwemo pia kupewa nafasi nje ya mfumo wa vyama ili wagombee nafasi za kuchaguliwa na wananchi.

Gabriel Boric - The 100 Most Influential People of 2022 - TIME

time.com › collection › gabriel-boric

gabriel boric presidente from time.com
23 May 2022 · He is making Chile the social, economic, and political laboratory of the world once again. Stiglitz is a Nobel Prize–winning economist

Pamoja sana kiongozi.
 
Bodi hawakati hela ya mtu, hela anakata mwajiri wako halafu ndio anaipeleka HESLB, wewe banana na mwajiri wako akupe hela yako ambayo amekukata bila utaratibu
Unachokitetea hapa hata hukijui, au unatetea uongo. Kuna wanufaika kibao walimaliza madeni yao zaidi ya miaka 5 iliyopita.

Mwaka huu wa 2023 wamepewa madeni mapya ya kulipa. Na wanakatwa 15% kwenye basic salary yenye mikopo lukuki.

Mabaya zaidi hao HELSB wewakiulizwa wanatoa sababu za kipuuzi puuzi tu. Halafu unasema mwajiri ndiye anayepeleka hayo madeni!
 
Bodi hawakati hela ya mtu, hela anakata mwajiri wako halafu ndio anaipeleka HESLB, wewe banana na mwajiri wako akupe hela yako ambayo amekukata bila utaratibu

Kwan lazima kubishana na hujui kitu mzee
 
Raisi Samia, japo umetukwaza sana na hii issue ya bandari, kuna mambo mazuri umefanya hasa katika kurekebisha baadhi ya mambo yaliyofanyika wakati wa utawala Marehemu Magufuli. Moja ya eneo ulilogusa ni kuboresha masilahi ya wafanyakazi kama kupandisha watumishi vyeo, kuongeza mishahara ingawa ni kwa kiwango kidogo na sasa ahadi ya kurudisha annual increments kwenye mishahara ya wafanyakazi kila mwaka.

Hata hiyo, kuna jambo moja muhimu na linagusa sana wafanyakazi(linaumiza) na hili si lingine bali ni uamuzi wa serikali ya awamu iliyopita kuongeza makato ya kulipia deni la Bodi ya Mikopo(HESLB), kutoka asilimia 8 mpaka asilimia 15 bila kujali mkataba wanufaika walioingia wakati wa kuomba mkopo(kukatwa asilimia 8), na pia makato haya kutozingatia sheria inayotaka Mfanyakazi abaki walau na moja ya tatu(theluthi moja) ya mshara ghafi wake(basic salary) baada ya makato yote ya lazima na mengineo kama mikopo ya mabenki n.k.

Kwa bahati mbaya, hata kama mtumishi ameshafikia ukomo wa hiyo moja ya tatu kwenye take home yake, makato ya HELSB hayazingatii hii sheria bali wanakata tu na matokeo yake mtumishi anabaki na take home iliyo chini ya moja ya tatu ya basic salary yake huku mishahara yenyewe ikiwa ni duni kabisa kwa wafanyakazi wengi wa nchi hii hasa wa serikali na pia hata wale wa sekta binafsi.

Kumbekuni hata CAG aliepita, aliwahi pinga haya makato na akatamka kabisa kuwa yanavunja sheria.

Binafsi sio muumini sana wa hii sheria ya kulazimisha mtumishi abaki na moja ya tatu kwasababu ina mapungufu mengi(niliwahi andika kuhusu haya mapungufu siku za nyuma) na pia sheria hii haikufanyiwa utafiti wa kutosha, ila kwakuwa serikali yenyewe sasa ndio kinara wa kuivunja, basi hii inangeza sababu ya kuona ni bora tu sheria hii ifufutwe kabisa au ifanyiwe marekebisho.

Mtumishi akitaka kukopa, anabanwa na hii sheria, ila ukidaiwa na Bodi ya Mikopo, sheria haizingatiwi wanakata tu. Hii sio sawa kabisa na ni bora hii sheria ifutwe ijulikane moja.

Kuongoza ni kuonyesha njia.

Talk the talk and walk the walk.
Utakuta jitu kutoka hifadhi ya lumumba linapinga tu kisa wewe ni mwana mageuzi.

Hii hoja ni ya msingi sana maana wanao umizwa na hii sheria gandamizi ni watanzania wote.

Hongera sana kwa kuibua hoja ya msingi sana kiongozi.
 
Mama ajatukwanza popote kwenye issue ya bandari iko sahihi , mtakuja kumshukuru badaye kwa kubinaifusisha badari anapenda maendeleo ya Tanganyika, isipo kua wengi ni slow learners.
Kuwakaribisha wawekezaji siyo dhambi bali dhambi ni njia iliyotumika ya kuvizia ndiyo watu wanaona kuwa kuna kasoro
 
Hapana mkuu siko huko ila mimi nakuambia time will tell mama iko sahihi kwenye hiyo bandari, subiri matokeo hao DP world na wamuni nimetumia bandari zao mtaona matokeo hizo hoja za mda hazina mashiko kwasbb bandari haimashike itabaki kua ya Tanzania siku zote
Fuata upepo wa kisuri suri
 
Serikali kwenda kinyume au kukiuka mkataba waliosainiana wanafunzi wa vyuo na bodi ya mikopo, kwa nini hamkujipanga na kwenda mahakamani kupinga? Mkataba ulikuw8% ni kukiuka Sheria kuifanya 15%
 
Mwalimu tafuta tuu plan B mshahara hautokaa ukutoshe... uza hata juisi walimu mnaikera sana serikali wanaona mnamalizia makusanyo
 
Raisi Samia, japo umetukwaza sana na hii issue ya bandari, kuna mambo mazuri umefanya hasa katika kurekebisha baadhi ya mambo yaliyofanyika wakati wa utawala Marehemu Magufuli. Moja ya eneo ulilogusa ni kuboresha masilahi ya wafanyakazi kama kupandisha watumishi vyeo, kuongeza mishahara ingawa ni kwa kiwango kidogo na sasa ahadi ya kurudisha annual increments kwenye mishahara ya wafanyakazi kila mwaka.

Hata hiyo, kuna jambo moja muhimu na linagusa sana wafanyakazi(linaumiza) na hili si lingine bali ni uamuzi wa serikali ya awamu iliyopita kuongeza makato ya kulipia deni la Bodi ya Mikopo(HESLB), kutoka asilimia 8 mpaka asilimia 15 bila kujali mkataba wanufaika walioingia wakati wa kuomba mkopo(kukatwa asilimia 8), na pia makato haya kutozingatia sheria inayotaka Mfanyakazi abaki walau na moja ya tatu(theluthi moja) ya mshara ghafi wake(basic salary) baada ya makato yote ya lazima na mengineo kama mikopo ya mabenki n.k.

Kwa bahati mbaya, hata kama mtumishi ameshafikia ukomo wa hiyo moja ya tatu kwenye take home yake, makato ya HELSB hayazingatii hii sheria bali wanakata tu na matokeo yake mtumishi anabaki na take home iliyo chini ya moja ya tatu ya basic salary yake huku mishahara yenyewe ikiwa ni duni kabisa kwa wafanyakazi wengi wa nchi hii hasa wa serikali na pia hata wale wa sekta binafsi.

Kumbekuni hata CAG aliepita, aliwahi pinga haya makato na akatamka kabisa kuwa yanavunja sheria.

Binafsi sio muumini sana wa hii sheria ya kulazimisha mtumishi abaki na moja ya tatu kwasababu ina mapungufu mengi(niliwahi andika kuhusu haya mapungufu siku za nyuma) na pia sheria hii haikufanyiwa utafiti wa kutosha, ila kwakuwa serikali yenyewe sasa ndio kinara wa kuivunja, basi hii inangeza sababu ya kuona ni bora tu sheria hii ifufutwe kabisa au ifanyiwe marekebisho.

Mtumishi akitaka kukopa, anabanwa na hii sheria, ila ukidaiwa na Bodi ya Mikopo, sheria haizingatiwi wanakata tu. Hii sio sawa kabisa na ni bora hii sheria ifutwe ijulikane moja.

Kuongoza ni kuonyesha njia.

Talk the talk and walk the walk.
Utapeli mtupu walitangaza kuongeza pesa kutoka shilingi 8,500/= kwenda shilingi 10,000/= lakini uhalisia bado ni 8,500/= kwa mjibu iwa barua walizoandikiwa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga Oktoba 2023
 
Kuna taasisi za ajabu sana hapa Duniani, bodi ya elimu ya juu HESLB ya Tanzania pamoja na bima ya afya NHIF ya Tanzania.
Sijui huko Bungeni wanaongelea mambo gani kuhusiana na bima ya afya.
 
Utakuta jitu kutoka hifadhi ya lumumba linapinga tu kisa wewe ni mwana mageuzi.

Hii hoja ni ya msingi sana maana wanao umizwa na hii sheria gandamizi ni watanzania wote.

Hongera sana kwa kuibua hoja ya msingi sana kiongozi.
Asante mkuu. Pamoja sana.
 
Unachokitetea hapa hata hukijui, au unatetea uongo. Kuna wanufaika kibao walimaliza madeni yao zaidi ya miaka 5 iliyopita.

Mwaka huu wa 2023 wamepewa madeni mapya ya kulipa. Na wanakatwa 15% kwenye basic salary yenye mikopo lukuki.

Mabaya zaidi hao HELSB wewakiulizwa wanatoa sababu za kipuuzi puuzi tu. Halafu unasema mwajiri ndiye anayepeleka hayo madeni!
Sijatetea kitu na kweli inawezekana sijui kitu lakini Nadhani hujanielewa vizuri kuhusu nafasi ya mwajiri kwenye makato yoyote unayokatwa kwenye mshahara wako. Wengine tulikuja kupata muafaka baada ya kutishia kumshtaki mwajiri na bodi mahakamani ndio taarifa zikakaa sawa, mana mtu unakatwa na deni badala ya kupungua linaongezeka, sasa unaponiambia mwajiri hahusiki nakuwa sikuelewi vizuri
 
Kwan lazima kubishana na hujui kitu mzee
Sidhan kama tupo humu kuoneshana nani anajua sana, lengo ni kuoneshana njia zinazoweza hilo tatizo kutatuliwa, kwani wengine mwajiri wao amewasaidia kuondokana na hilo janga la kubambikiwa deni la HESLB ambalo halina uhalisia, kuna watu walikuwa wanakatwa badala ya deni kupungua ajabu likawa linaongezeka, lakini kwa kushirikiana na mwajiri wakaweka taarifa sawa. Nafasi ya mwajiri ipo kuhakikisha mtumishi wake anatendewa haki
 
Usione aibu mwalimu...walimu nikama mahouse boi/girl mnafanya vizuri kulea watoto wetu hatuwachukii kiukweli
Kwa hiyo na wazazi wako waliokuzaa (hawa ndiyo walimu wako wa kwanza kabisa kukufundisha kula, kunya, kuvaa nguo, kupiga mswaki, kuoga, kusalimia, kuheshimu wakubwa zako, nk) nao ni ma house boy/girl wako siyo!!!

Kama wewe kweli ni mzazi, basi utakuwa na akili za kitoto kama walivyo hao watoto wako.
 
Back
Top Bottom