Makazi ya Mbowe huko Machame yatufunze kujitegemea siyo kuiba mali za umma kama wafanyavyo wanasiasa wengi nchini

Chuki zilizomfanya apoteze yote hayo ziliishia wapi?. Kutoka jela leo kesho ukaenda ikulu ni ishara kwamba mfumo unakufahamu vyema na yeye ni sehemu ya viongozi japo sio wa moja kwa moja.
Serikali iliona mbali ingejiharibia sifa ya serikali ya Tanzania katika duru za kimataifa hasa kwa wahisani wao nchi za Magharibi (US na EU)

Ukizingatia serikali ilikuwa haina hoja yenye mashiko kwenye kesi ya ugaidi ya Mbowe

Kutoka jela hadi ikulu ilikuwa ni kujisafisha
 
Kusema kweli hata kule twitter nimeshangaa sana, hivi ni vitu vya kawaida uchagani nawashauri watanzania wazunguke nchi yao. Ukitembea huku uchagani utashangaa sana kuna nyumba hauwezi amini unaweza ukashinda ndani wiki kuna kila kitu. Mimi ni mchaga lakini nilishangaa kuna nyumba zina hadi swimming pool kijijini. Kuna kipindi tulipigiwa simu na fogo twende tukampe kampani ya kuangalia mechi ya EPL kwake. Mimi nipo napambana lazima niangushe mjengo wa maana nyumbani kwanza.
 
Mbowe ni sehemu ya mfumo kwa miaka mingi.
 
Mbowe ni usalama wa taifa wa miaka mingi. Mzee wake ni mmoja wa watu wa mfumo tangu miaka hiyo akiwa bado yupo hai.
Kwa hiyo UWT hatakiwi kuwa tajiri!!??
UWT hatakiwi kulipa kodi inayostahili!!??
UWT hatakiwi kuwa na "legal businesses"!!?
UWT hatakiwi kuweka wazi vyanzo vyake vya mapato!!??

Kama Mbowe ni UWT,basi ni moja ya UWT wachache sana walio bora na mfano wa kuigwa.
 
Sasa mbona JPM alipojenga kwao chato mlimkejeli sana mlimuongelea sana yupo sawa na Mobuto seseko mbona leo mnamsifu mbowe kujenga kwao

Sent from my Infinix X663 using JamiiForums mobile app
 

Watu wanashindwa kuelewa Mbowe alikuwa mdhamini wa Yanga miaka hiyo wakati GSM labda alikuwa shule[emoji1787]
 
Msisahau kutembelea bukoba vijijini pia...

Takwimu za serikali zisiwapumbaze kuhusu mikoa kadhaa

Hapa ni Bukoba vijijini huko ndani ndani

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Bro hiv kwanini watz hawakubali ukweli. Mkubali mtu akifanikiwa acha ngonjera. Kwani Baba yake mbowe alikuwa na watoto wangapi na ni wangapi wamefanikisha ndoto zao. Simpo tuache roho za kichawi maisha ni marahic sana ukikubali ukweli na kuukabili.
 
Broda hii kitu naisema kila siku humu. Kwenye familia kuna mmoja ni taa ya wote ni nature na kwenye Taifa hivyo hivyo kuna kabila moja ni taa ya makabila yote. Ukilidhibiti umedhibiti maendeleo ya nchi hivyo nchini inakuja kushikiliwa na wageni. Wazungu hiz code wamezigundua miaka mingi ndio wanazitumia. Wamarekan wana msemo wao unasema. U can play with america but don't play with the people from Texas.
 
Uko serious kabisa unataka kulinganisha vijiji vya Kilimanjaro na Bukoba?
Hiv barabara ya machame ishajengwa?

Mbowe si ndo mbunge wa huko?

At vijiji...so tunatishana sio...

Kama unataka battle mimi nakuja na wilaya moja tu ya muleba..



Moja ya barabara huko machame.

Naomba usikimbie please

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Mi nawashaur watu wanaojenga kijijin hasa Kilimanjaro. Hilo ni eneo la kitalii. Nyingi ya hizo nyumba hazitumiki muda mrefu hivyo kwa kuepusha nyumba kukaa bila mtu. Ziingizeni Airbnb. Mtakuja kunishukuru. Mi nyumba zangu za kijijin nimeziingiza humo na muda wote wa mwaka ipo full. Hii kitu nilikikuta Nigeria kwa wa Ibo. Hawa jamaa ndio waafrica waliojenga kijijin kweli. Ukifika ni kama uswis. So ombi langu kwa watu wa Kilimanjaro ni kuwa mkoa wetu hauna madini usema yataisha kesho so shughuli za uchumi zitasimama. Ule mlima mpaka Yesu arud ataukuta ni Zaid ya dhahabu Mungu katupa ufanyeni ni kitega uchumi maana wanadamu wanakuja kutoka pande zote za Dunia kuja kuupanda wanalipa.
 
Wivu wa nyumba yako utanila:Maskini wengi comments zao hapa ni za wivu Wengi wanaona wivu, hawajui Mbowe hizi fedha anazo kabla wao hawajazaliwa: Hapo ni Kijijini Machame, wacha Dar, Arusha na Mwanza kote ana makazi :
 
Mkuu umekuza sana mambo, sioni uhusiano wowote kati ya UWT na Mbowe. Watu wangapi wa usalama wa taifa ambao hawajapitia UWT wala skauti?.
 
Vijana mnapotafakari kesho yenu, tangulizeni kwanza fikra na nguvu katika kutafuta utajiri wa haki ndipo mgombee nafasi za kuongoza watu kwa haki.

Nchi kubwa kama Marekani, hiyo ndio falsafa yao. Nazisikilizaga hatuba za Mwalimu Nyerere; anasema rais Kennedy wa Marekani aliwahi kusema: unapogombea urais, jiulize, utaifanyia nini Marekani, na sio Marekani itakufanyia nini! Hii ni tofauti na nchi (nyingi) zinazoendelea.
 
Jamani sipendi kuona waatu mnabishana kwenye keyboard mimi ni mchaga nachowaasa watanzania watembelee nchi yao. Kuna mengi ya kujifunza, haina haja ya kubishana kuhusu wapi ni pazuri au pabaya. Ninachowasihi Watanzania wenzangu msikazane na mitazamo mgandpo tembeeni mjifunze. Haina haja ya kwenda Marekani wala ulaya. Huku huku nyumbani kuna mengi ya kujifunza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…