Makofi ya leo bungeni, wabunge wapatiwe huduma ya kwanza

Wabunge wa CCM na wale mamluki wengine, wanaifilisi timu nchi! Sioni kama wana tija yoyote ile. Yaani mpaka Rais ameamua kuwafundisha wajibu wao!

Wenyewe walishazoea utaratibu mpya na wa kipuuzi kabisa wa kuisifia tu serikali na Rais wake!
 
Hata akikutana anataka wajadili jinsi ya kufanya siasa zenye tija kwa nchi.

Maana yake baada ya kukutana hatutarajii kuwaona akina Lisu wakiponda Atcl, Sgr, bwawa la Nyerere kuwa ni miradi ya hovyo badala yake wataanza kusema hiyo ni miradi ya watanzania.


Kwa akili zao wanahisi mama ataenda kuwaruhusu kufanya maandamano kila siku.
 
Baadhi ya kazi adhimu za bunge ni kutunga Sheria, kujadili bajeti za wizara mbalimbali na kuikosoa serikali (Trust and Verify) katika nyanja mbalimbali za kiutawala wake.

Vivyo basi nilitegemea bunge liwe limesheheni lawyers, Economists, Auditors and Accountants etc.
Badala yake bunge limesheheni Vilaza wa darasa la saba na form four failures wasiojua chochote kuhusu Sheria, uchumi na Utawala.

Unafikiri viongozi wa dizaini hiyo wataleta chachu yeyote ya mabadiliko ya kiuchumi zaidi ya kuwa wapiga mapambio na vigelegele tu bungeni?

Ni aibu na fedheha kubwa sana kwa taifa letu kuendelea kuona bado tunaingiza wabunge wenye sifa ya kujua kusoma na kuandika tu na tukibaki kuwategemea wafanye mabadiliko katika ulimwengu huu wa mapinduzi makubwa ya sayansi na teknolojia wakati hawana maarifa yeyote kuhusu Sheria, Uchumi na Utawala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walipiga makofi kote ila ilipofika kwenye Demokrasia yakakaa nzwiiii.Kimyaaa,hata Covid-19 hawakusikika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…