Verse uliyo quote inaeleweka kabisa
KWELI INAELEWEKA SANA
YESU ALILETA UPANGA
Sawa na mafundisho ya Biblia tumeelewa tayari kwamba Bwana Yesu alikuwa mtume kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Sasa tuone kwamba Bwana Yesu Kristo alileta kitu gani na alitumwa na nini?
Mwenyewe anatueleza lengo la kutumwa kwake, anasema:
1. Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani. La, sikuja kuleta amani, bali upanga. Kwa maana nalikuja kumfitinisha mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu. (Mathayo 10:34-35).
2. Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wa kike, naam na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. (Luka 14:26).
3. Je, mwadhani ya kwamba nimekuja kuleta amani duniani? Nawaambia la, sivyo, bali mafarakano. (Luka 12:51).
4. Bwana Yesu alitayarisha wafuasi wake kwa ajili ya kuleta fujo na vurugu na aliwaamrisha akawaambia:
“Lakini sasa mwenye mfuko na auchukuwe, na mwenye mkoba vivyo hivyo, naye asiye na upanga akauze joho lake akanunuwe upanga. (Luka 22:36).
5. Siyo maneno tu bali katika maisha yake alionesha hata kwa vitendo vyake kwamba alikuwa mtu wa fujo.
Biblia inasema kwamba:
“Yesu aliingia ndani ya hekalu akawafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni. Akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwa wakiuza njiwa.” (Mathayo 21:12).
6. Akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akizipindua meza zao. (Yohana 2:15).
7. Kwa sababu ya mafundisho yake, wanafunzi wake walikuwa wajeuri kiasi hiki kwamba walikuwa wakitumia upanga kwa ujasiri. Biblia inasema: ”Na tazama, mmoja wao waliokuwa pamoja ya Yesu akanyoosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumwa wa kuhani mkuu, akamkata sikio.” (Mathayo 26:51).
Sasa mmesoma historia ya Bwana Yesu Kristo na mafundisho yake kuhusu kuleta fitina na fujo duniani na kuharibu amani ya watu.
Na inashangaza wakati baadhi ya Mapadri wanatangaza au inaandikwa juu ya ‘sticker’ za magari kwamba “There is peace in the blood of Jesus” yaani ipo amani katika damu ya Yesu.
Ilhali yeye alikuwa siyo mwenye kuleta amani duniani bali upanga, fujo na fitina.
Sisi Waislamu tunaamini kwamba Bwana Yesu (Masihi) alikuwa Nabii wa Mwenyezi Mungu na alitumwa kwa lengo maalum, lililotajwa kwa ulimi wake katika Qur'an Tukufu kwamba:
“Nisadikishaye yaliyo mbele yangu katika Taurati na kutoa habari njema ya Mtume atakayekuja nyuma yangu jina lake ni AHMAD.” (QUR'AN 61:7).
Pia sawa na mafundisho ya Qur’an Tukufu, nabii Isa a.s. alifungamanishwa na amani katika maisha yake yote: “Na amani iko juu yangu, siku niliyozaliwa na siku nitakayokufa na siku nitakayofufuliwa kuwa hai.” (19:34