Makonda aanza kukamata wakusanya madeni (auctioneers) wanaotumwa na mabenki

Biashara yenu ya mikopo kausha damu dhamira yake kubwa ni dhuluma. Sio kusaidia watu
 
Hapo Makonda ndio unapowaumiza viongozi wenzie..kuna mikoa ya Dar es salaam na Mwanza kuna changamoto kibao lakini viongozi wapo tu kuzunguka na magari na Ving'ora.
Wamemzima kwenye Uenezi ameibukia Arusha..Media zote ziko Arusha kwa Makonda.
 
Ulisha kaa ndani ww ukikaa siku tatu tu akili inakaa sawa.Usiombe ukaenda huko acha kabiisa.
Lile tapeli Mmasi lilikua linamgomea Waziri Jerry Slaa kutoka ndani ya nyumba, likatupwa Nondo, ndani ya lisaa likaomba poo kwa Waziri na likahama usiku huo.huo! Usicheze na sukumia ndani,kunatisha balaa,hasa kama siyo mzowefu nako!!
 
Yeye alienda kukopa
Akapewa mkataba akausoma
Akasaini
Alisaini baada ya kujirizisha na mkataba.

Kashindwa kulipa
Nyumba ndiyo ilikuwa rehani
Wakopwshaji wanataka pesa yao

Wanauza nyumba yako (rehani) wanachukua million tatu Yao + riba. Ya juu wanakurudishia.

Kuna tatizo gani hapo? Kama ulikopa rudisha. Kama uliweka nyumba rehani, wewe ndiyo ulikubali.

WaTamzania tujifunze kuheshimu sheria (rule of law); hapo Makonda kafanya rule by law.

Angemsaidia huyo mdaiwa aende mahakamani.
 
Kuna Uhuni kati ya Wakusanya madeni na maofisa mikopo wa Benk.... wanatumia ufinyu wa uelewa wa wakopaji kudhurumu hasa Nyumba na viwanja vilivyo wekwa kama dhamana ya mikopo.... aingiii akilini deni la 5 millions lina sababisha nyumba ya 50 M kuuzwa na hawa wakusanya madeni na mwenye nyumba asipewe ata shilingi. Humu JF kuna uzi mmtu analalamika hati yake ya nyumba huu ni mwaka wa 5 NMB Tabora awataki mrudishia.Kama alijakukuta wewe au ndugu yako wa karibu unaweza ona hili la makonda ni uvunjifu wa sheria, ila likiwa lako usingesema haya!
 
Hapa ndio wasaa unashauri angefanya biashara sio? Au angelima sio? au angefuga sio? Wewe unaefanya hivyo vitu milioni 50 unazo?
 
Kumbe pesa za BANK ni zetu wananchi? Sasa mbona hatupewi.


KAZI ni kipimo cha UTU
 
umeongea kitoto sana, yaani kama mtu wa miaka 15 usiye elewa maisha ni nini

sema umejaliwa kujua kusoma na kuandika ila akili ya kuchambua mambo naomba nikwambie hauna hata kidogo
Wewe mpumbavu ungekaa kimya. Sasa hapo Makonda kachukua tu maamuzi ya kisiasa ila mahakamani huyo aliyeuziwa nyumba hachomoki na anaweza ongezewa deni la kulipa gharama za kesi. Acheni kutaka huruma kwenye biashara za watu.
 
Nakuunga mkono. DAWA YA DENI NI KULIPA.
 
Makonda ni unpredictable kabisa na hiyo itampaisha sana!!

Binafsi Kwa sasa ndio mtu pekee anaweza kukipa uhai chama chetu coz wengine wamekalia kula TU na kushiba hakuna anaetatua kero za wananchi!!

huyu ndio hasta kama ana mapungufu ni Bora tunaiona imapact yake kuliko hai wengine hawaonekani wanafanya nini zaidi ya kumuandama Lisu anaesema ukweli na uzembe wetu wenyewe was kutotatua KERO za muungano live bila chenga!
 
Hapa Makonda ndio anatimiza wajibu kama Baba mlezi wa mkoa na wananchi wake. Wahuni wa Arusha mwisho wao umefika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…