Makonda aanza kukamata wakusanya madeni (auctioneers) wanaotumwa na mabenki

Dawa ya deni ni kulipa na hizo ni sheria hakuna shortcut wewe ukitaka hiyo kabadili sheria zinazosimamia.minada.
Na unapokopesha unatakiwa kutumia akili. Kuna miongozo. Jiulize huyu mtu akishindwa kulipa na tukajikuta mahakamani nitaeleweka? Nitapewa vibali vya kufilisi na mahakama? Au nitalazimika kuhonga ndo kibali kitoke? Sasa wengi wanahonga, kibali kinatoka mwishowe ndo mwenye mali akijiongeza kidogo tatizo kubwa zaidi linazaliwa.
 
Kwa nini mahakamani asieleweke? Mlalamishi ndio awahi mahakamani kama ameonewa.

Makonda hawezi tatua kesi ya mahakamani acheni upuuzi
 
Kazi ya Mahakama ni kutimiza makubaliano ya wahusika, makubaliano ni hiyari, mahakama haiwezi kupachika vipengele vyake katika mkataba kwa kuwa itaondoa sharti la kufanya mkataba uwe hiyari ya wahusika.
 
Wewe ulitaka afanye nini kwa wananchi wanaoonewa?

Wewe ciembe unachuki kukbwa sana na Makonda na kwa taarifa yako huyu ndiye atakuwa rais wako muda sio mrefu kama hautaki yeyuka hewani.
 
Kama unazijua taratibu za kufilisiwa na namna vibali vinavyopatikana na wewe ni mkuu wa mkoa ungefanya hivyo hivyo kama makonda sababu kuna harufu ya Rushwa kwenye upatikanaji wa vibali au hawakuwa na vibali.

Kwa uelewa wangu wa haya mambo, nyumba ya M50 kupewa kibali na mahakama cha kufilisi kwa mkopo wa M3 na riba yako ipo kisheria si rahisi maana deni litakuwa dogo na lazima utakuwa ulifanya kosa la kutohakiki uwezo wa mkopaji wakati unatoa huo mkopo. Yaani wewe uliangalia dhamana tu, ukajilipua kumbe unamkopesha mtu asiyekidhi vigezo vya kukopeshwa.

Katika mazingira haya mahakama inaextend muda wa marejesho na kapenati kidogo. Unaweza kuambiwa rejesha elfu hamsini kila mwezi.
 
Sikatai kuwa kunaweza kuwa na controversies kwenye issue nzima. Ninachopinga ni ufanyakazi kazi wa aina hii, kufanya mbele ya kamera ili ujikombe. Kuna shida gani mgogoro kama huu kama utatatuliwa ofisini baada ya kusikiliza pande zote? Na zaidi, hili ni tatizo sugu la nchi nzima. Tumefikaje hapa? Kutoka ofisini na kusikiliza kesi moja moja itasaidia nini badala ya kutengeneza mifumo ya ku deal na mambo kama haya ifanye kazi?
 
Kwa nini mahakamani asieleweke? Mlalamishi ndio awahi mahakamani kama ameonewa.

Makonda hawezi tatua kesi ya mahakamani acheni upuuzi
Kwa hicho kiasi kama taasisi ilitoa mkopo kisheria, na riba imefata miongozo ya BOT, deni sio kubwa na mkopaji hakuwa na sifa za kukopeshwa hata kama ana dhamana, sasa katika hayo mazingira Mahakama isingeweza kutoa kibali cha kufilisi labda kwa njia za rushwa.

Makonda kanusa harufu ya Rushwa kwenye upatikanaji kibali cha kufilisi hakuna kingine.
 
Hayo mambo ya sifa za kisiasa nakuunga mkono. Alipaswa kuwaita ofisini kama kuna jinai ataigundua tu.
 
Twende mbele na kurudi nyuma. Wewe umeenda kukopa mkopo wa Tshs 3m. Ukasema naweka nyumba yangu amana kwa ajili ya mkopo, ina thamani ya Tshs 50M. Sasa usiporudisha mkopo hao waliokukopesha wafanyeje? Kwa nini wakati wa kukopa usiweke amana kitu cha thamani ya mkopo?

Kisheria ni kwamba, wakiuza nyumba yako ya Tshs 50m, wataiuza kwa mnada, na wanaweza wapate Tshs 30m. Ila watakupa Tshs 27m baada ya kuchukua zile zao Tshs 3m. Ndio maana katika amana za namna hii, ni bora wewe uuze nyumba mwenyewe, unaweza kupata fedha zaidi.

Kwa hiyo hapa Makonda ndio anakosea. Anashughulika na haya mambo kisiasa. Huu ni utaratibu unakubalika kabisa katika masuala ya mkopo. Huyu mkopaji hakulazimishwa kuweka nyumba kama amana, yeye ndio aliamua, kwamba nikishindwa kurudisha uzeni nyumba yangu.

Sasa watu hapa msifanye assumption kwamba nyumba ya Tshs 50m imeuzwa na wakopeshaji wakachukua zote Tshs 50m. Hapana, kama wameuza kwa Tshs 50m, watachukua hela yao tu, ile nyingine wanamrudishia
 
Hapa Makonda ndio anatimiza wajibu kama Baba mlezi wa mkoa na wananchi wake. Wahuni wa Arusha mwisho wao umefika
Kama wale wahuni wa Tanga,Jerry Slaa kawapiga za chembe wakatapika nyongo za dhuluma! Huku Slaa, huku Makonda,Mama Samia yeye atulie,ale bata,kazi yake kesha maliza,na ni nzuri sana,maana ukisikia mitapeli inaanza kulia kwenye jiwe gizani, ujuwe hilo limempata!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…