Pre GE2025 Makonda ameagizwa na nani kufanya maigizo Nchi nzima!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Umeme, maji, rushwa, nidhamu, rasilimali za taifa zilizouzwa.

Uko wapi waziri, chawa Masaki? Angalia Watanzania milioni 60 maisha yao, unaisha kwa ubabe kwa kodi zao.
 
Wanaofanyaga maigizo ni kina Lisu, Mbowe, Lema ambao hata ukiwalilia shida gani hawawezi kukisaidia hata kwa elfu 10.
Nashukuru kwa majibu yanayomtafakarisha msomaji.

Aidha, hao uliowataja hapo na wenzao wengine ambao hukuwataja, kiutaratibu wanaweza kuwaamuru watendaji wafawidhi na waandamizi wa serikali? Jibu linanielekeza kukuunga mkono kwamba Makonda yuko ndani ya mzingo sahihi.

Nadhani pia kwamba walioshika dola (CCM) ndiyo discretion iko kwy mamlaka yao kuielekeza serikali waliyoiweka madarakani kufuata ilani ya uchaguzi waliyokabidhiwa bila kubweteka ambamo ndani yake kuna ahadi au maelekezo ya kutatua kero za wananchi.

Nadhani tungefuta somo la Civics tukarudisha somo la Siasa maana Civics imejielekeza kutukuza mamlaka zaidi kuliko kutoa elimu ya uraia.

Watz wengi ni wachapiaji wa siasa.
 
Swali ni je, Wananchi wanampokeaje? Je Maeneo mengine yanataman pia afike au?.



Kati yako wewe Mmoja na wananchi maelfu Kwa maelfu wanaojitokeza, Ni nani tumzingatie nani tumpuuze?.
Ni kweli mkuu.

Hasinge address kero maana yake hata wakandarasi (suppliers) wangezikwa fedha zao na masoko ya mitaji walikokopa yangepiga mnada dhamana zao za mikopo. Kwa kuwekwa hadharani wadaiwa ni kielelezo kizuri cha madai kwenye mchakato wa kisheria wa kutafuta haki ama iliyocheleweshwa au iliyonyimwa.

Kwenye kutatua kero za wananchi nadhani sote kwa itikadi zetu tuungane kwamba haihitaji siasa.
 
Wanafanya misafara yao na magari ya beii juu halafu nchini umeme unasumbua sana View attachment 2887136
Ndugu yangu Charles.

Magari ya kifahari yametengenezewa maskini duniani, ndiyo maana Afrika ndiyo soko lao kuu. Umaskini una tafsiri-anuai ukiwemo umaskini wa fikra pia. Matajiri 90% hawatumii magari hayo.

Waziri Mkuu wa Ureno anaenda kazini kwa miguu.
 
Mkuu Butron kutoa umeme, maji, kuzuia rushwa, kujenga miundombinu, elimu bure ni muhimu sana. Vipi kuhusu ukiinginanisha na kutoa sababu, maneno mengi, vitendo sifuri, kuwauza Wamasai, kuuza bandari, Tanganyika, hakuna maji, umeme.

Ungechagua nini?
 
Swali ni je, Wananchi wanampokeaje? Je Maeneo mengine yanataman pia afike au?.



Kati yako wewe Mmoja na wananchi maelfu Kwa maelfu wanaojitokeza, Ni nani tumzingatie nani tumpuuze?.
Wapuuzi ni hao wanajazana
Tumesahau Babu wa Loliondo!!
 
Mwache afanye hivyo sababu hii nchi wajinga ni wengi sana na inahitaji watu wa aina ya Makonda ili wajielewe
 
Bashite anawafanyia mzaha tu wananchi ni ukweli uliowazi bashite hawezi kutatua changamoto yoyote zaidi ya kudeal na petty issues.

Hata wenzake washamjulia ss hv wanachofanya siku ya ujio wake wana acts kama wapo serious akiondoka tu wanamkejeli.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Kila anakokwenda raia wamejaa wamemzunguka na shida lukuki! Utakuta eneo lina RC, RAS, DC, DAS, DED mpaka OCD. Bado kuna TAKUKURU, maafisa ardhi, wajumbe wa nyumba 10/10 na kila idara nyeti lakini wote ni USELESS tu. [emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu,

Hujaelewa tu kuwa kampeni imeshaanza?

Hujaelewa tu kuna mtu anajitengenezea "plausible deniability" ya "si niliwaletea Makonda kapita nchi nzima huku?"
 
Mwache afanye hivyo sababu hii nchi wajinga ni wengi sana na inahitaji watu wa aina ya Makonda ili wajielewe
umesema vyema , west afrika huko Mali, Burkina Faso wameanza kuamka, na wametembe na cahwa waliokuwa wanawakwamisha.
 
Makonda anazunguka nchi nzima si KUTATUA kero za wananchi, bali anachokifanya ni kuuonesha umma kuwa hii nchi HAINA Serikali. Kila anakokwenda raia wamejaa wamemzunguka na shida lukuki! Utakuta eneo lina RC, RAS, DC, DAS, DED mpaka OCD. Bado kuna TAKUKURU, maafisa ardhi, wajumbe wa nyumba 10/10 na kila idara nyeti lakini wote ni USELESS tu. Wanatafuna tu kodi za wananchi!

Jamaa anakusanya wananchi wanaoitwa 'wanyonge', halafu anawauliza "haya semeni matatizo yenu mmoja baada ya mwingine!" Kisha wananchi wanawataja viongozi wa maeneo yao kama DC, DED, wenyeviti wa mitaa kama chanzo cha matatizo yao – ambao wote hao ni wana chama tawala!

Cha kushangaza zaidi, Makonda anatoa 'maelekezo' kwa watu HAO HAO waliosababisha matatizo sugu kwa MIAKA yote kwamba waenda WAKAYATATUE ndani ya MASAA au SIKU! Wananchi nao WANAPIGA MAKOFI wakiamini shida zao zimetatuliwa. Utadhani hii ni mara ya kwanza kwa viongozi kufanya haya MAIGIZO! Msafara ukiondoka, kila mtu anarudi nyumbani amechoka, shida ziko pale pale.
 

Ccm imemea a self destruction machine, inajiharibu yenyewe.


"Mwenezi anazunguka nchi nzima si KUTATUA kero za wananchi, bali anachokifanya ni kuuonesha umma kuwa hii nchi HAINA Serikali"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…