Pre GE2025 Makonda ameagizwa na nani kufanya maigizo Nchi nzima!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nature abhors a vacuum.
Ukipewa kazi ukashindwa kuifanya lazima atajitokeza mwingine kuifanya. Anaweza akatokea mwema au kibaka.
 
Nachagua kuwa na wananchi, watu hawa wanaozunguka wamekwenda kutambika kwenye makaburi ya marehemu na kuomba mizimu na zaidi wanaomba ghost za hao viongozi ziwaongoze huku wakijiita walokole.
Wanamtaja Mungu midomoni lakinimioyo yao iko mbali naye.
 
Hahahaha jana mbona Makonda kasema kwa nini Dkt Samia kaamua iwe hivyo maana yeye kama mwenyekiti wa chama ndiye kamtuma. Iko hivi, timu mafisadi, wezi wakiongozwa na akina JM walimuaminisha Dkt Samia timu inayoamini ktk uadilifu ni wabaya sana hivyo hawafai kuongoza serikali, basi Dkt Samia kawateua kila sehemu hahahah na matokeo yake kila sehemu ni uozo hivyo anachokifanya Makonda ni kumbua gamba Dkt Samia kuwa siyo yeye aliyesababisha kudorora kwa huduma za serikali bali ni lile kundi la mafisadi na wezi ambao anajutia kuwateua hivyo sasa anakwenda na timu ya waadilifu na wachapa kazi na anawaomba msamaha watanzania wampe kura 2025
 
ooh, kumbe, kwahiyo ufalme umefitinika.
Hao uliowataja, watarudisha walivyovichota?
Na kama ndivyo, mbona wanaendelea kuwek watu wao kwenye mashirika, idara na wizara?
Mbona wao ndio inasemekana wanapitisha majina nani awe balozi na nani asiwe?
Mbona inasemekana ndio wao wameamua kuweka vituo vya mafuta nchi nzima kila mtaa?
 
Taratibu wanashughulikiwa kimya kimya, wote wataisha, usiwe na wasi wasi, ogopa sana mtu mkimya, unaweza dhani mjinga na hajui hahaha. Sikilizia tu hapo kabla ya 2025 wengine watakimbia nchi wengine rip
 
Nature abhors a vacuum.
Ukipewa kazi ukashindwa kuifanya lazima atajitokeza mwingine kuifanya. Anaweza akatokea mwema au kibaka.
Well noted, and that is what we see.
Kashindwa kuwatumbua watu flani kaamua kuwaletea manaibu, manaibu wameshindwa kumuokota asiye na haya wala soni.
 
Cha kushangaza zaidi, Bashite anatoa 'maelekezo' kwa watu HAO HAO waliosababisha matatizo sugu kwa MIAKA yote kwamba waenda WAKAYATATUE ndani ya MASAA au SIKU! Wananchi nao WANAPIGA MAKOFI wakiamini shida zao zimetatuliwa. Utadhani hii ni mara ya kwanza kwa viongozi kufanya haya MAIGIZO! Msafara ukiondoka, kila mtu anarudi nyumbani amechoka, shida ziko pale pale.
 
Shida nini? Mbona sisi tuliandamana na hakuna baya. Yan shida ipo wap
Mkuu shida ni wananchi kwa nn wanaenda kwa wing?
Shida ni kwa nini wanatoa kero zao?
Shida nin mkuu?
 
Anaieneza CCM

Wengi wanadai Shujaa kafufuka naye kamtokea Makonda πŸ˜‚πŸ”₯
This is for real 😳!
Watu hawataamini lakini Makonda ni unstoppable kwa sasa !
Na inaelekea kwa kujua au kutokujua anayo full backup ya Mama. !!
Ngoja tuone πŸ™πŸ™
 
Shida nini? Mbona sisi tuliandamana na hakuna baya. Yan shida ipo wap
Mkuu shida ni wananchi kwa nn wanaenda kwa wing?
Shida ni kwa nini wanatoa kero zao?
Shida nin mkuu?
Kumekuchaa !
Tuliwaambiaga mkitaka kuwawin watu wengi Nchi hii tembelea nyota ya JPM !
Wakatubeza !
Sasa Naona ngoma inogile !
 
Makofi yanapigwa na walionyimwa elimu na ufahamu na hao hao wanaotoa maagizo.
Wameanzisha shule za kata na kila mtu lazma afaulu hata kama hajui kundika jina.
Wanazalisha bodaboda na wamewapa jina la "maafisa usafirishaji"
Wanaalisha kizazi kibovu kuwahi kutookea Tanganyika,
 
This is for real 😳!
Watu hawataamini lakini Makonda ni unstoppable kwa sasa !
Na inaelekea kwa kujua au kutokujua anayo full backup ya Mama. !!
Ngoja tuone πŸ™πŸ™
Hakuna ngoja tuone! Mazaa kishasoma ramani, kaona hana influence, kaona wengine wanapata umaarufu kuliko yeye na usidhani hasomi tweeter na jf, anasoma na cha kumuokoa kaona aletemropokaji, asiye na soni ndio ashughulike na wanaotaka formu 2025.

Majaliwa,Kigwangala, Makamba, Mpina, Kasheku inasemekana wote wanataka fomu 2025 .
Vita ni kali ndani ya chama.
 
Wwe hujawai kuumwa, na siku ukiimwa mbona utatafuta kila aina ya dawa ili upone, watu wamedhulumiwa wameshitaki kwenye mamlaka husika lakini bado hawajasaidiwa na hadi wamekata tamaa, sasa Mungu kamleta Makonda naona na imani yao imerudi tena! Subiri siku udhulumiwe na wajanja walioiweka serekali mfukoni ndiyo utawaelewa hao wananchi wanaomlilia Makonda awasaidie matatizo yao!!
 
Absolutely correct. Otherwise anachofanya Makonda ni usanii. Ukitaka kuchange system, lazima head wa system hiyo ndiye awe the leading figure otherwise ni ngumu kuchange system wakati mwenye system anaona kila kitu kiko sawa. Hapo ndipo nakubaliana na mtoa mada yawezekana huu ni usanii,

"We are creating and raising our political supremacy and personal popularity on expense of the pervasive poverty, , pain and suffering of the ignorant citizen "
 
Excellent case.....nani ni mtendaji, je kinachofanyika kinaleta taswira ipi kuhusu uwezo wa hao viongozi wakuu wa serikali uliowataja na wengine ngazi ya mkoa na wilaya. Je kama aliyewachangua hao ndio aliyemchagua huyu na kumtuma, hii inaleta taswira ipi kati ya chama na serikali yake. Je hatuoni kuna mgongano hapo wa chama kumreprimand mtumishi wa serikali mbele ya kadamnasi.
 
Nachagua kuwa na wananchi, watu hawa wanaozunguka wamekwenda kutambika kwenye makaburi ya marehemu na kuomba mizimu na zaidi wanaomba ghost za hao viongozi ziwaongoze huku wakijiita walokole.
Wanamtaja Mungu midomoni lakinimioyo yao iko mbali naye.


Wewe ungekuwa kiongozi leo ungefanya birthday party au kwenda Tanesco makao makuu live ukawauliza changamoto zenu ni nini hasa?

Ukirudi kesho na keshokutwa nina uhakika Tanzania tutapata umem. Kauli moja kwa mfumo wetu ya Rais ina uzito mkubwa sana na itatekelezwa bila chenga.

Rais hana muda na hivyo vitu sio muhimu kwake.

Tatizo kubwa lingine ni ardhi, akamtoa Lukuvi mbobezi wa kusaidia maskini, wajane, yatima ameweka wapigaji. Upigaji kila sehemu.
 
Hao walioshindwa kuhudumia si waondolewe?
Kama Makonda ndiye kaletwa , basi waondoe naibu waziri mkuu na waziri mkuu ateuliwe Makonda.
Okay ili uteuliwe waziri mkuu lamza uwe mbunge wa jimbo, wa kuchaguliwa.
CCM si wafanye kama wanavyofanyaga tu, enzi za mwendazake?, waandike barua kama vile Dkt. Faustine Ndugulile kaandika, ajiuzulu na wao wajiandikie wameridhia, Makonda agombe Kigamboni alafu fomu za wapinzani zirudishwe kuwa wamekosea kujaza.
we mbunge apewe uwaziri mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…