Makonda amesema kweli; wengi wa viongozi wa Serikali hii ya CCM wanafanya usanii kumpa sifa Rais Samia, lakini kivitendo wanamhujumu

[emoji1666][emoji106]
Unaamini wasaidizi wanamuangusha Samia kwanini asiwaondoe kama anaona wanamuangusha?

Mkiitwa chawa mnakuwa wakali, ukweli ni kwamba Samia amefeli kuliongoza hili taifa, ameshindwa kabisa.

Huu mgao wa umeme zaidi ya miezi sita, ajabu bado mpo mnaoona anajitahidi kurekebisha makosa ya Magufuli!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Tayari Fereshi kamtia doa jingine mama. MAHAKAMA KUU TANZANIA IMETENGUA UAMUZI WA RAIS SAMIA WA KUMSTAAFISHA KWA MANUFAA YA UMMA ALIYEKUWA DC WA TABORA BWANA KOMANYA.
 
Ukumbuke kipindi cha Mwendazake biashara nyingi zilikufa, wawekezaji wengi walisepa na viwanda vingi vilipunguza uzalishaji na hivyo matumizi ya umeme kushuka.
Mkuu Mizania,

Unadai Biashara zilikufa.

Je, ni biashara zipi hizo ili Watanzania tuzijue?

Sio hivyo tu, umedai wawekezaji wengi walisepa na hivyo kufanya viwanda vingi kupunguza , uzalishaji.

Ni sababu zipi hizo zilizo fanya Wawekezaji kusepa, na ni viwanda vipi hivyo vilivyopunguza Uzalishaji? Unayo mifano yeyote ile?

Je, unaweza kutupatia chanzo cha taarifa zako? au hayo ni maoni yako tu?
 
H Huna kumbukumbu wewe Mbwiga. Tuliza Makalio na chuki zako kwa shujaa
 
Kila awamu zilizopita bidhaa zilipanda bei , lakini tunachojiuliza ni kwamba zilipanda kwa kiasi gani ?
Je kwenye awamu hii watu wamepandisha sana bei za bidhaa kuliko awamu zilizopita ?
 
Wewe ndo mpumbavu!! Acha Wizi kafanye kazi ya Umma hakuna atakayekugusa
 
Absolutely true
 
Huwezi kujibiwa πŸ™πŸ™
 
"Samia ni Rais ambaye amefeli kuliko Rais yeyote kwenye historia ya Marais wa nchi yetu". Nakubaliana na mleta mada 100%.
Na kafeli kweli kweli, atahitaji kusaidiwa kijiti cha uongozi hata kwa kutumia figisu.
 
Akili nyingi za watanzania ni kama za huyu Jamaa Kuonyezha kuwa We are reach of foolish people.
What you should know is Hakuna CCM na Serikali Ni watu wajinga tu wakiona Mpishi kabadilishwa wanafikiri zitakuja mboga mpya. Kuweni na akili tunatafuta Kura zenu.
 
Yaap atwambiie so analopoka tuuu
 
Kila awamu zilizopita bidhaa zilipanda bei , lakini tunachojiuliza ni kwamba zilipanda kwa kiasi gani ?
Je kwenye awamu hii watu wamepandisha sana bei za bidhaa kuliko awamu zilizopita ?
Mkuu na kuelewa na hoja yako ina ukweli kabisa.

Tukiwa wa kweli tunapaswa kuanza kuangalia tulipo jikwaa sio tulipodondokea.

Ukweli ni kwamba Magufuli alivuruga the economic fabric and setting ya nchi yetu kwa kiasi kikubwa ndani ya muda mfupi. Madhara yake ndio yanaanza kujionyesha sasa!

Magufuli aliweka mazingira magumu ya kufanya biashara nchini, mazingira yaliyowafukuza wawekezaji wengi wa nje na ndani, wakulima, wafugaji na wavuvi

Magufuli hakufanya chochote kwenye ajira na maslahi ya wafanyakazi. Hii ndiyo nguzo ya mizunguko wa fedha.

Magufuli alianzisha miradi mikubwa mingi kwa wakati mmoja ambayo mpaka ama haijaaza kuingiza fedha au inajiendesha kwa hasara.

Magufuli alikopa kiasi kikubwa cha fedha kwenye ma benki ya ndani na nje ya kibiashara yenye riba kubwa na ya muda mfupi. Muda wa kulipa umeiva.

Magufuli aliharibu mahusiano ya kimataifa kwa namna ambayo misaada na mikopo nafuu ikasitishwa kwetu.

Magufuli alichota kiasi kikubwa cha fedha kutoka mashirika ya umma na mifuko ya kijamii kuanzisha miradi yake hiyo kiasi cha kufilisika.

Kwa Mujibu wa ripoti ya CAG ya miaka mitano 5 ya kipindi cha Magufuli, ndio kipindi ufisadi ulifika zaidi ya Trilioni 1.5 kila mwaka na deni la taifa kuongezeka mara dufu!

Bahati mbaya hayupo, ulitegemea kwa hali na mazingira haya mambo yakae sawa sawa??? Haiwezekani labda ndotoni.

Tukubali kuwa huu ndio ukweli na uhalisia wa maisha. Tulikuwa tunapiga makofi akivuruga, kwa sasa tutulie kimya maumivu yatufungue akili.
 
Huwezi kujibiwa πŸ™πŸ™
Mkuu,

sio kwamba siwezi kumjibu, ila iko hivi kama anaona nilichosema sio kweli ama ni uongo, akanushe au apinge au asahihishe majibu yangu kwa kuweka ukweli wake hapa kutoka hicho chanzo chake ambacho anadai ni cha ukweli.

Huo ndio msingi wa mjadala wowote duniani. Nina amini ataleta hizo facts zake dhidi ya za kwangu ili kutuelimisha na kutusahihisha mapema iwezekanavyo.

Huu ni mjadala sio mpasho!
 
Kama unamuona Makonda is doing a Good Job, he is mentally OK upstairs, then you are done and you are at liberty to think so, but subject people's opinion as I have done! Usijiweke katika level ya proletariats Najua wewe hauko hivyo lakini....... Hao anaowatukana mawaziri etc wanaogopa kumjibu kwa kutetea ugali wao.
Anyway, my thinking is on these lines as expounded by Philosopher, and Psychologist Askofu Bagonza in his post copied here below!!
ALL IN ALL NISAMEHE KAMA YOU WERE NOT PLEASANT WITH MY EARLIER COMMENT, MY APOLOGIES!
Anaandika kwa Ufasaha: Askofu Dr Benson Lwakalinda BAGONZA
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
MAKONDA: Ni Tatizo, Dalili au Suluhisho?

Paul Makonda ni zaidi Katibu Mwenezi wa chama Tawala. Tumewahi kuwa nao wengi na wapo wengi wa vyama vingine. Hakuna kama Makonda uzuri na kwa ubaya. Kwa nini?

1. Kama Makonda ni tatizo basi halina suluhisho. Kwa sababu ndani ya chama tawala huyu ndiye ameonekana. Na kama huyu ndiye bora zaidi, waliobaki wana hali gani?

2. Kama Makonda ni dalili ya tatizo basi dalili huwa hazina tiba. Tusubiri ugonjwa wenyewe ndipo tujue tiba. Mgonjwa anayetetemeka kwa homa, kumfunika blanketi zito si kutibu ugonjwa. Ni kusaidia mayai ya vimelea yaanguliwe na mgonjwa atakuwa na hali mbaya zaidi.

3. Kama Makonda ni Suluhisho basi ni lile la β€œBomoa yote tutajenga kesho”. Mchelea mwana kulia hulia yeye mwenyewe. Yeye amekuwa suluhisho zaidi ya dawa ya rangi mbili inayoua vimelea vyote mwilini.

AMESAIDIA SANA:

- Sasa tunajua hali yetu si njema. Hakuna utawala wa sheria wala wa mfumo.

- Sasa tunajua hasara za kukaa gizani. Ukikosa upinzani bungeni na mabarazani, ukakosa uhuru wa habari, ukakosa wana harakati huru, unastawisha CHAWA kila mahali.

- Sasa tunajua wananchi wanaona bora dikteta kuliko demokrasia, yaani bora shibe ya gerezani kuliko njaa ya uraiani.

- Sasa tunajua wenye shida wanataka mtu si taasisi wala mfumo.

- Sasa tunajua kila suluhisho linazaa tatizo. Ukifuga mbwa mkali wa kulinda wezi, kuna siku atakuzuia wewe usiingie nyumbani kwako.

- Sasa tunajua hakuna bunge huru, hakuna mahakama huru, hakuna DPP huru, hakuna AG huru - ila kuna Chama huru.

HEKIMA: Kuna mbwa akiwinda na kukamata mawindo, huwezi kumfukuza eti anaharibu ngozi. Atakula kitoweo chote na mwenye mbwa atakula mchicha siku hiyo.
 
mbona unasema ukweli aisee πŸ’
 
Haya ya 5 kutoka chini ni mbinu nzuri ya kuwashika wanyonge.
 
Mkuu tatizo kubwa la nchi yetu ni mifumo mibovu iliyowekwa ambayo inamfanya kiongozi yeyote mkuu kuonekana mungumtu hivyo watawala hufanya wapendavyo,hivyo suluhisho ni viongozi wa chini ku opt uchawa ili wasavaiv
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…