Makonda amesema kweli; wengi wa viongozi wa Serikali hii ya CCM wanafanya usanii kumpa sifa Rais Samia, lakini kivitendo wanamhujumu

Makonda amesema kweli; wengi wa viongozi wa Serikali hii ya CCM wanafanya usanii kumpa sifa Rais Samia, lakini kivitendo wanamhujumu

Maswali yako yanaonesha dalili ya kama haukuwepo Nchini ndiyo umekuja toka ughaibuni..

Bahati mbaya sana jamii haiwezi kuweka rekodi ya tarehe ya kila bidhaa ilipopanda bei,nadhani unataka kutumia kichaka hicho kuficha udhaifu wa baadhi ya watu.

Kuanzia bajeti mpya ya serikali 2021/2022 ndiyo karibia kila bidhaa ilipoanda bei kwa kiwango cha juu ( utajua aliekua kiongozi mkuu alikua nani)

Utakumbuka ni kipindi hicho hicho kuna mtu alikua anasisitiza kuwa "kila kitu kitapanda bei" huku akisema ni kwa sababu ya covid...ndipo wafanyabiashara wengi wakaanza kupandisha bei za bidhaa maradufu..

Utakumbuka ni kipindi hicho Waziri mkuu aliingilia kati akamuagiza waziri wa viwanda Dr.Ashantu kupitia FCC wafanye uchunguzi ni kwanini bei za bidhaa zimepanda sana, FCC wakaja na majibu ya kuwa "hakuna sababu za msingi zilizofanya bidhaa kupanda bei"

Baada ya hapo yule yule aliesisitiza kuwa bidhaa zitapanda bei kwa sababu ya covid,akaja tena na maneno kuwa bidhaa zitapanda kwa sababu ya ukraine.

Kila awamu ya uongozi,bidhaa zilipanda bei,ila kwa kiasi gani zimepanda na sababu zilizosababisha upandaji huo ndiyo jambo la mjadala...

Kabla ya bajeti ya 2021/2022 ( kwa baadhi ya maeneo)
1:- Nomdo 12 mm, tulinunua elfu 19, ilipanda hadi elfu 28
2 :- Bati 30G, bando moja tulinunua laki 220,ilipanda hadi 350
3:-Mafuta ya kula ikawa gumzo
4:-Sabuni kila unavoenda dukani utakuta bei mpya
5:-kwa kifupi ni kila kitu
Mkuu nakubaliana na aya ya pili kutoka mwisho katika hoja yako. Binafsi sijapinga hoja kwamba vitu havijapanda katika awamu hii.

Mkuu Ninacho kataa ni mchango unaosema kuwa vitu vimeanza kupanda awamu hii.

Huu ni mjadala muhimu, tuelimishame, kukumbushana, kusahihishana bila ushawishi wa mahaba kwenye awamu yoyote!

Na kuweka kumbukumbu sawa sijatoka ughaibuni. Nipo bongo kabla Mwendazake hajaanza kupiga push up majukwaani!
 
Mkuu nakubaliana na aya ya pili kutoka mwisho katika hoja yako. Binafsi sijapinga hoja kwamba vitu havijapanda katika awamu hii.

Mkuu Ninacho kataa ni mchango unaosema kuwa vitu vimeanza kupanda awamu hii.

Huu ni mjadala muhimu, tuelimishame, kukumbushana, kusahihishana bila ushawishi wa mahaba kwenye awamu yoyote!

Na kuweka kumbukumbu sawa sijatoka ughaibuni. Nipo bongo kabla Mwendazake hajaanza kupiga push up majukwaani!
Hata Mimi nakuungs mkono kuwa awamu zote bidhaa mbalmbali zinapanda.

Tunachpbishiana hapa ni je upandishaji wa bidhaa katika awamu zilizipita
Ulikuwa na sababu za msingi za upandishaji huo?

Je katika awamu hii , kuna sababu za msingi za kupandisha, jinsi walivyopandisha??

Hiyo ndiyo hoja ya msingi, tunayobishiana nayo.
FULL STOP
 
Mbona YY KIZIMKAZI nae anahujumu Tanganyika.
1.Umeme...NO
2.Sukari.....NO
 
Mkuu usipumbazwe kabisa, chui habadiliki madoa ya ngozi yake asilani.

Matatizo uliyoyaainisha yana ugumu wa kuyatatua kwa haraka pasipo mpango mkakati uliosukwa vizuri. Makonda anajua fika shida ilipo maana kwenye vikao muhimu yumo.

Mabwawa tunayotegemea ni ya muda mrefu, hayana service na yamejaa tope hivyo kina cha maji kimepungua mno, unahitaji muda kuondoa hilo tope, wakati ukiwa hautumii hilo bwawa.
Makonda anafahamu vizuri. Ndio maana hazungumzii hilo anagangamara na individual issue.

Ili uyatoe matope mabwawani unahitaji chanzo cha nishati mbadala ambacho kwa bahati kwetu ni gesi, Makonda anafahamu jinsi baba yake, Mwendazake alivyovurunda na kuvuruga mkakati okozi, mbadala na wa kudumu wa nishati ya umeme, gesi ya kupikia majumbani na viwandani kisa tu ukosefu wa asilimia 10% kwa upande wake.

Kama ni mkweli na amejinyumbua kuwa kiumbe kipya awaambie wananchi shida ilipo!!!

Ukumbuke kipindi cha Mwendazake biashara nyingi zilikufa, wawekezaji wengi walisepa na viwanda vingi vilipunguza uzalishaji na hivyo matumizi ya umeme kushuka.

Makonda anajua vizuri na alijifunza barabara kutoka kwa babake, Mwendazake kuwa mbele ya macho ya the poor illiterate masses, watumishi wa serikali are the best punching bag!!!

Kuhusu upandaji wa bidhaa na nauli sababu zake ni very varied ila the common denominator ni mafuta, dolar, mvua na government policies juu ya kodi. Mvua imenyesha nyingi kwa kipindi kirefu, kwenye process ya uvunaji wa miwa haiwezekani!
It is obvious na ilitegemea kuwepo na uhaba na penye uhaba bei hupanda!

Uagizaji wa bidhaa mbali mbali umekutana na uhaba/ukata wa dola nchini! Kigingi kingine licha ya dola kuadimika, madafu yetu yameporomoka, huku serikali imeng'ang'ania msimamo wa kubaki na kodi hata ikiwezekana kuongeza kodi mpya bila kupandisha mishahara!

Unategemea kwa mazingira haya kwa wafanyabiashara bei itashuka!

Makonda anafahamu fika yote haya! Kama ni mkweli na ni kiumbe kipya basi awaambie ukweli wananchi!!!
Ujinga mtupu kipara na maharage chande wamepiga matrilioni ya pesa na kuiingiza tanesco mikataba ya kilaghai kisha kusepa,walianza na visingizio kibao,bajeti kubwa ya kukarabati,wewe na wenye akili kama yako ni utoko wa zinaa
 
Watu walifurahishwa na uongozi wa jpm ,sasa Makonda ndio mtu ambaye ana ujasiri kama jpm kwa kupatiwa ulizi na support ya kutosha kutoka katika mhimili mkuu. Kwa sehemu ameweza kuamsha matumaini ingawa bado sana sababu yupo chini ya mtu kimamlaka kama atapewa urais ,He can deliver with no excuse term.
 
Hiyo inasababishwa na upole wa kiongozi mkuu, anawapa vyeo halafu hawapi direction watendaji wake wafanye vipi majukumu yao, matokeo yake unakuta kila mmoja anaanza kwenda na njia yake, wakati mwingine inafikia wao kwa wao kupishana kauli ilimradi wabaki na sifa moja kuu, ya kumsifia mama.

Kinachotokea sasa Makonda anazunguka huko mikoani na wale wenye matatizo yao wanajitokeza mikutanoni, hawa ni haki yao kufanya hivyo kwasababu mtu ukiwa na shida mara nyingi huwezi kujali nani atakayekusaidia, ilimradi ujue yupo wa kusikiliza, basi utamfuata ukamwambie.

Wengine wanaona Makonda msanii, lakini binafsi nikitazama kile anachofanya Makonda kwa sasa, na uungwaji mkono anaopata, naona kabisa amewazidi wale wanaojiona wanajua "kufuata taratibu", waliopewa kazi ya kukinadi hicho chama chao ikawashinda, ndio maana Samia akaamua kumpa hiyo kazi Makonda, anayeonekana sasa kuifanya zaidi yao.

Baadae, kinachokuja kuyaunganisha hayo makundi mawili ni ile kauli moja tu toka kwa makundi yote, "mama anaupiga mwingi" hapo makundi yote mawili, licha ya tofauti zao kiutendaji yanabaki salama kwa mamlaka yao ya uteuzi.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Miongozo ya kila nafasi ipo
 
Back
Top Bottom