Makonda amesema kweli; wengi wa viongozi wa Serikali hii ya CCM wanafanya usanii kumpa sifa Rais Samia, lakini kivitendo wanamhujumu

Umemaliza kila kitu kiongozi,..miradi ilikuwa mizuri lakini kwa uwezo wetu,isingewezekana twende nayo yote kwa pamoja..NEVER..na shida ndio ilianzia hapa..yote kwa yote,ACHA MUNGU AITWE MUNGU!
 
Ukweli utatuweka huru ! 🙏
 
Mkuu tatizo kubwa la nchi yetu ni mifumo mibovu iliyowekwa ambayo inamfanya kiongozi yeyote mkuu kuonekana mungumtu hivyo watawala hufanya wapendavyo,hivyo suluhisho ni viongozi wa chini ku opt uchawa ili wasavaiv
Kweli kabisa !
Na mpaka sasa bado wakubwa hawajaliona hili na kuazimia kulifanyia marekebisho kwenye Katiba. !!
Lakini mimi naamini iko siku atakuja kupatikana Kiongozi Mkuu atakaye wasulubu wenzake kupitia madaraka yake aliyonayo kwa mujibu wa Katiba hii mpaka maji wataita mma. !!
Ndipo watakapolia na kusema laiti tungejua !!
Mifano ilishajionyesha kuanzia 2016 !
Kwamba kumbe akipatikana Mwamba Nchi inaweza ikanyooka !!
🙏🙏🙏
 
Kila awamu zilizopita bidhaa zilipanda bei , lakini tunachojiuliza ni kwamba zilipanda kwa kiasi gani ?
Je kwenye awamu hii watu wamepandisha sana bei za bidhaa kuliko awamu zilizopita ?
Ni kweli Kila awamu, bidhaa mbalmbali zilipanda.

Swali la kujiuliza, je upandaji huo wa bidhaa ulikuwa katika Hali halisi?

Ndiyo maana, Mimi nimetoa mfano wa bidhaa 2 zilizopanda maradufu bei zake, nazo ni bei ya sukari, iliyopanda Kwa almost 100% na nauli za mabasi nayo ni almost 50%

Ukiangalia bei ya sukari, utaona kuwa kuna baadhi ya watu, ambao wamesababisha "scarcity" ya bidhaa hiyo ili ipande.

Tukija Kwa upande wa nauli za mabasi, tujikumbushe sababu kuu walizotoa hao wamiliki wa mabasi, wakati wanawaomba LATRA kupandosha nauli hizo, sababu kuu walizotoa ni kupanda Kwa bei ya mafuta ya petroli katika soko la dunia.

Swali la kuwauliza hao LATRA ni kuwa, mafuta yameshuka bei Katika soko la dunia, je kuna uhalali Gani wa kuendelea kutumia bei hizo hizo za nauli wakati bei za mafuta ya petroli zimeshuka??
 
Wanaomuita mhalifu ni Chadema bila ushahidi.

Makonda amekuwa heavyweight awamu ya 5 na Sasa awamu ya 6
 
Tatizo lipo Kwa Rais mwenyewe kupenda kusifiwa kuliko uhalisia wa matokeo ya kazi anayofanya,
 
Wanaomuita mhalifu ni Chadema bila ushahidi.

Makonda amekuwa heavyweight awamu ya 5 na Sasa awamu ya 6
Unasemaje wanaomuita mhalifu ni Chadema pekee?

Hivi nani asiyejua kuwa yeye Makonda, aliingia kwenye kituo Cha habari Cha Clouds TV, akiwa na askari wenye mitutu, ambapo ni kitendo Cha jinai??

Hivi ni nani asiyefahamu kuwa hata kwenye nchi za wenzetu, walibaini uhalifu wa huyu Bashite, hadi nchi ya Marekani, kumpiga marufuku kukanyaga katika ardhi ya nchi hiyo, yeye na familia yake, Kwa kile walichokiita kuwa yeye Makonda, anawanyima Raia wa nchi hii kuishi??

Hivi kweli umewaelewa wamarekani Kwa kusema kuwa Makonda, anawanyima raia wake haki ya kuishi??
 
- Sio wote wanaoogopa kumjibu Makonda, ndio maana Bashe alimjibu, na hiki ndicho nilichozungumzia kwenye my first comment uliyojibu kwa namna uliyoona kwako inafaa, hope hapa nimekuonesha vizuri nini nilikuwa namaanisha na umeelewa.

- Makonda amepewa kazi ya kukitangaza chama chao, kumkejeli humu JF wakati kule field tunaona watu wanaojitokeza kumsikiliza, hata kama mtawaita wajinga, na Makonda mumuone mjinga, lakini huo ndio ukweli, ana watu wanaomfuata na kumsikiliza, ndio wenye matatizo yao wanaotaka misaada, huu ni mfano wangu wa pili nilioandika kule juu ukaishia kujibu ulivyoona inafaa.

- Lastly, unasema your way of thinking ni kama ya Askofu Bagonza, hapo aliposema sasa wananchi wanapenda dikteta zaidi ya demokrasia hope upo nae pamoja!.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
- Sio wote wanaoogopa kumjibu Makonda, ndio maana Bashe alimjibu, na hiki ndicho nilichozungumzia kwenye my first comment uliyojibu kwa namna uliyoona kwako inafaa. Hope hapa nimekuonesha vizuri nini nilikuwa namaanisha na umeelewa. Hao watu wawili wana mgogoro kati yao lakini wanakuwa connected na kumsifia Samia, hivyo wote wanabaki salama.

- Makonda amepewa kazi ya kukitangaza chama chao, kumtukana matusi ya nguoni kama mnavyofanya, au kumsifia kwa wale wanaomsifia, wote mnaonesha anafanikiwa kwenye kazi anayoifanya ya kukitangaza chama chake, ndio malengo ya kazi aliyopewa.

- Lastly, unaposema unafikiria kama Askofu Bagonza, hope inamaanisha uko pamoja nae hata pale anaposema wananchi sasa wanataka kuongozwa kidikteta zaidi ya kidemokrasia!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hapa kwetu bei hupanda tu !
Huwa hazishuki ! Sijawahi kusikia nauli zimeshuka !
 
Hilo la kutubu dhambi Mimi simo.hilo analijua muumba wetu
kwa matatizo uliyoyaorodhesha hapo kwa wengine wetu huku vijijini siyo vipaumbele vyetu.
Hata hiyo sukari hatuijui inatumiwa kwenye nini.sisi tunamahitaji yetu muhimu kama maji.huduma za Afya Nk
asanteni kwa yote
 
Ukweli unajulikana. Na utaendelea kujulikana.

This is a typical Grand art of Fabrication.
 
Maswali yako yanaonesha dalili ya kama haukuwepo Nchini ndiyo umekuja toka ughaibuni..

Bahati mbaya sana jamii haiwezi kuweka rekodi ya tarehe ya kila bidhaa ilipopanda bei,nadhani unataka kutumia kichaka hicho kuficha udhaifu wa baadhi ya watu.

Kuanzia bajeti mpya ya serikali 2021/2022 ndiyo karibia kila bidhaa ilipoanda bei kwa kiwango cha juu ( utajua aliekua kiongozi mkuu alikua nani)

Utakumbuka ni kipindi hicho hicho kuna mtu alikua anasisitiza kuwa "kila kitu kitapanda bei" huku akisema ni kwa sababu ya covid...ndipo wafanyabiashara wengi wakaanza kupandisha bei za bidhaa maradufu..

Utakumbuka ni kipindi hicho Waziri mkuu aliingilia kati akamuagiza waziri wa viwanda Dr.Ashantu kupitia FCC wafanye uchunguzi ni kwanini bei za bidhaa zimepanda sana, FCC wakaja na majibu ya kuwa "hakuna sababu za msingi zilizofanya bidhaa kupanda bei"

Baada ya hapo yule yule aliesisitiza kuwa bidhaa zitapanda bei kwa sababu ya covid,akaja tena na maneno kuwa bidhaa zitapanda kwa sababu ya ukraine.

Kila awamu ya uongozi,bidhaa zilipanda bei,ila kwa kiasi gani zimepanda na sababu zilizosababisha upandaji huo ndiyo jambo la mjadala...

Kabla ya bajeti ya 2021/2022 ( kwa baadhi ya maeneo)
1:- Nomdo 12 mm, tulinunua elfu 19, ilipanda hadi elfu 28
2 :- Bati 30G, bando moja tulinunua laki 220,ilipanda hadi 350
3:-Mafuta ya kula ikawa gumzo
4:-Sabuni kila unavoenda dukani utakuta bei mpya
5:-kwa kifupi ni kila kitu
 
Hapa kwetu bei hupanda tu !
Huwa hazishuki ! Sijawahi kusikia nauli zimeshuka !
Bei zinapaswa kushuka, kama gharama za bidhaa hizo zimeshuka katika soko la dunia au soko la ndani.

Ukiona bei hazishuki, kutokana na factors hizo 2, ujue kuwa kuna hujuma
 
Bei zinapaswa kushuka, kama gharama za bidhaa hizo zimeshuka katika soko la dunia au soko la ndani.

Ukiona bei hazishuki, kutokana na factors hizo 2, ujue kuwa kuna hujuma
Kabisa
 
Makonda ananikumbusha Sauli wa kwenye biblia,toka kuwa mtesi mpaka kuwa mtetezi akiitwa baadae Paul.

Tumuelewe tu,watu ubadilika.
Sauli wa Tarso [emoji1], na baadaye akabatizwa na kuitwa Mt Paulo.

Kweli umewaza mbali sana mkuu.
 
Makonda anachokifanya ni sawa, kuchukua chupi ya baba ake iliyotoboka na kuitembeza mtaani.
Manake mambo anayosema leo anawavua nguo wazazi wake ambao CCM,hivyo akimariza ziara ajiandae kuwa barozi Malawi au Zambia, CCM hawana utamaduni wa kujivua nguo.
Kwahiyo kwakua amewavua nguo wenzake ajiandae kukutana na Kisanga kabla ya 2025.
Manake wazee wa kuchutama wamechutama.
 
Yeye mwenyewe Makonda hizo ziara zake zinamhujumu Samia kwani uozo unaoibuliwa unafanywa na wateule wake na wote ni makada wa CCM
 
Aliyewataua walaji hao kwa wingi tunaachaje kuamini kuwa naye ni mlaji?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…