Pre GE2025 Makonda amjibu Waziri Bashe, asema atamhoji sababu yeye ndiye anakitafutia kura chama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hayo ni maoni yako na mimi siwezi kuyapiga rungu.
Nawajua hao vijana. Inasikitisha Watanzania kwenye hekima hawataki kuingia kwenye siasa hadi watu kama hawa wanaitwa akili kubwa.
 
Mheshimiwa Bashe Alikosea sana kutoa kauli ile hadharani na kuleta picha ya kama dharau kwa watu.ukiwa kiongozi unatakiwa utambue wapi uzungumze na wapi ukae kimya.uongozi mzuri ni pamoja na kuchagua maneno na kauli za kuzungumza mbele za watu.sasa alikuwa anatunishiana na nani misuli? Kwamba katibu mkuu wa chama ni mdogo kwake na hawezi mwambia chochote? Kwamba makamu mwenyekiti wetu wa chama ni mdogo kwake na hawezi mwambia chochote? Hii ni dharau na kujisahau ulikotokea.
 

Ziara zijikite kwa vitu muhimu, umeme, maji. Kwanini mmefunga umeme, maji kwa miaka mitatu.
 
Bashe ana kibru thaana tyu. Makonda sema usiogope sema!!!
 
Bashite ni kilaza hamuwezi Bashe.
Wewe ndiye kilaza mkubwa sana. Na mwaka huu utakufa na chuki zako binafsi kwa Mheshimiwa Makonda. Maana umepiga Majungu yako kwa Mheshimiwa Makonda mpaka umeona kila mtu amekupuuza, na sasa umebakia huna jipya zaidi ya kutekeseka tu moyoni mwako.
 
Makonda akili kubwa,sidhani kama kuna mtu wa kupingana na makonda kwa sasakwa hoa watu,Bashe kachoka nafasi yake wacha tuone
 
Anaetakiwa kumuhoji ni mwenyekiti ambaye ni raisi
Au katibu mkuu nchimbi mwenezi kazi yake ni kueneza na kufafanua sera za chama chake


Halafu mahojiano ni private kwenye sekretali zao huko sio public.....sababu basHe anatumikia watu wa vyama vyote...ila bashite only ccm
 
Wanatuadaha Kwa mambo Yao ya kipuuzi huku ya kwao yakitimia na kuendelea kuzitafuna Kodi zetu tukija shtuka tumepigwa siku mingi wao wanagonga chiazi za mvinyo wa bei ghali toka ufaransa!!
 
Hakuna wanaume wanapiga vijembe, wajitazame uanaume wao hawa majamaa!!
 
Lucas, Bashe katika nafasi yake ya uwaziri yeye kama mtumishi wa Umma, Chama hakiwezi kumwambia lolote. Hizi sio zama za chama kushika hatamu.

Chama kinatakiwa kuishauri serikali na kutoa maagizo kupitia vikao na sio kwa mtumishi wa Umma mmoja mmoja tena majukwaani kwa simu.

Acheni ujinga na kuhalalisha ujinga, ni nani aliwaloga nyie? Mbona mnakuwa wajinga hivi?

 
Naomba unijibu swali hili. Je katika wanaotakiwa kumuhoji au kumpa maagizo Mheshimiwa Bashe uliona mahali popote pale alipomtaja katibu mkuu? Huoni kuwa alimdharau na kuona hawezi kumpa maagizo yoyote yale? Unaona ni sawa hiyo? Huoni ni dharau kwa chama na viongozi wa chama?
 
Chama ndio chenye serikali kwa hiyo hakiwezi kukaa kimya kinapoona mahali kuna changamoto nyingi zinazopigiwa kelele na wananchi. Chama ni lazima kitake ufafanuzi kwa waziri yeyote yule akiwepo Mheshimiwa Bashe.kwa hiyo kama Bashe anajiona ni mkubwa kuliko chama na viongozi wake akiwepo makamu mwenyekiti au katibu Mkuu n.k. basi atafute chama chake au ajiuzulu uwaziri ili Mheshimiwa Rais ateue mtu mwingine atakaye shirikiana na chama chetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…