Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Makonda waziri wa Samia amesema anakusudia kujenga msikiti wa dola milioni 80 mpaka 100 Arusha kwa ajili ya Utalii watu kutembelea na pia watu wa hadhi ya ubunge kupata sehemu nzuri ya kuswalia.
Mimi nafikiri hajashauriwa na kuelewesha vizuri . Arusha ni mji wa Wakristo wengi, Waislamu ni wachache (minority). Huo msikiti ni bora angeshauriwa kuujenga Zanzibar au Dar.
===========
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Arusha Mjini, Paul Makonda amesema anatarajia kujengwa kwa msikiti mkubwa Jijini Arusha ambao, mbali na kuwa sehemu ya ibada, pia utakuwa kivutio cha utalii.
Makonda amesema Arusha inapaswa kutumia fursa zinazotokana na wageni na matukio makubwa yanayofanyika Jijini humo ili kuongeza shughuli za biashara na kukuza uchumi wa wananchi.
“Tunampango mkubwa hapa Arusha wa kujenga msikiti, sio wa Watu kuishia kuswali tu, bali utalii; yaani mtu akifika anaenda kutalii,” amesema Makonda.
Aidha, Makonda amewapongeza viongozi walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza kuwa uongozi ni dhamana na jukumu la kusukuma mbele maono ya Taifa.