Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Tanzania ya viwanda.
Hayo unayoyaita "madeksi" kwenye picha JKT hawawezi kuyatengeneza?
Mzigo unaoingia kwa manifesto yenye jina la mtu unataka kuelezeaje?

Madawati ya shule za mkoa wa Dar yanaagizwa na RC tena kwa jina lake? Na hataki kulipia ushuru?

Procurement procedure ndio zinasema mkuu wa mkoa anaweza kuagiza chochote ili mradi kiitwe cha matumizi ya umma?

Fedha ya kununulia hio mzigo iliyoka kwa nani? Kama jina la mzigo ni Paul Makonda basi fedha za kununua katoa/kalipa yeye.

Hilo kanisa alilotumia kugawa laana kwa wanunuzi wa hayo makontena litakua kanisa la hovyo kabisa.

Acheni kujitoa ufahamu....muda ni mwalimu mzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kila aliyepigiwa mnada makontena au magari yake pale Bandarini angeenda wanunuzi walaani ANGEBAKI NANI?
 
TEA wanaweza kulipa vifaa ambavyo hawajaagiza?Tena vimekuja kwa jina la Makonda!
Malengo ya Makonda na TEA yanashabihiana kuhusian na hayo makontena; sasa kuliko mimi niyanunue nipeleke kwenye shule zanfu Uganda si bora TEA wakafanya hivyo?LOL
 
Ko jamaa anajiita MLIMA, afu yule kiongozi wa malaika anajiita JIWE..... Basi sawa!!!!!!!
 
Mdhamini kidogo
FB_IMG_15353586467652410.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahah...haya ni mahoka!!

Bwana Makonda lipa ushuru wa forodha makontena yatoke, acha kibri
 
Taarifa huripotiwa kwenye vyombo vya habari kama runinga, redio, magazeti, majarida na mitandao ya kijamii. Iliporipotiwa taarifa ya uingizwaji na uwepo wa makontena yenye jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mwanzoni iliripotiwa kuwa Makonda 'aliyakana' makontena hayo.

Baadaye, ripoti zinadokeza kuwa RC Makonda 'aliyatambua' makontena hayo yaliyokuwa mikononi mwa TRA na kudai kuwa yalikuwa na samani za shule za mkoa wa Dar es Salaam. 'Akatishia' hata 'kuwashtaki' TRA kwa Rais. Mambo yakawa kimya hadi sasa inaporipotiwa kuwa TRA wamejaribu kuyapiga mnada bila mafanikio.

Sasa inaarifiwa kuwa RC Makonda amekwenda kanisani 'kufanya maombi maalum' ya kukwamisha mnada wa makontena yake. Ametishia kuwa yeyote ambaye atayanunua atapata laana! Kimsingi, ni Dhahiri sasa kuwa RC Makonda anayatambua na kuyapigania makontena yake. Makontena hayo yana nini hasa? Kwanini yalikuja kwa jina lake?

Namsihi RC Makonda, katika hili la makontena yanayoshikiliwa na TRA, aeleweke. Aiache TRA ifanye kazi yake na si kutaka kuionyesha TRA kama iliyo kwenye 'mission' naye kuyahusu hayo makontena. Mnada ufanyike na mambo mengine yaendelee. Namsihi RC Makonda kuacha pia kuwatisha 'kimaombi' wateja wanaotaka kuyanunua makontena hayo.

Kazi njema wakuu wote!
Anajisumbua tu asubiri rungu kutoka kwa mkuu litue kwake maana anayoyafanya yanamchafua mteuzi wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria ni msumeno. Lazima kodi ilipwe.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sijui kwanini nashindwa kukubali hili sakata. Naona kama ni sinema ili tuamini kwamba sheria zinambana kila mtu. Usikute hata macontainer halisi yalishatolewa hayo yaliyo hapo ni bosheni tu. Kisa ichezwe movie kutuaminisha kwamba hata viongozi wanadhibitiwa kwenye kulipa kodi.
 
Back
Top Bottom