miwani ya maisha
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,733
- 2,511
Huko kanisani si ndipo alipomwaga chozi baada kung'ang'aniwa aweke cheti mezani".............sasa nayaamini maneno ya Nape rasmi, kuwa kwa elimu/ufahamu wa huyu mtu kamwe hawezi elewa mfumo wa siasa na serikali inavyofanya kazi". Yaani RC anashindwa kujua sheria za kodi zinasemaje?????? Anakimbilia kanisani??
I seeNdani yake hukosi mercedes ya bethidei kwa mama daudi
Weee jamaa unasema kwa hili la makontena aeleweke aiache TRA ifanyekazi yake!! Huyu anatakiwa aeleweke kwa mambo mengi sana, amechafua watu majina yao kwa madawa ya kulevya, operesheni ya kutelekeza watoto, kauli mbovumbovu nyingi, ukweli kuhusu jina na elimu yake, etcTaarifa huripotiwa kwenye vyombo vya habari kama runinga, redio, magazeti, majarida na mitandao ya kijamii. Iliporipotiwa taarifa ya uingizwaji na uwepo wa makontena yenye jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mwanzoni iliripotiwa kuwa Makonda 'aliyakana' makontena hayo.
Baadaye, ripoti zinadokeza kuwa RC Makonda 'aliyatambua' makontena hayo yaliyokuwa mikononi mwa TRA na kudai kuwa yalikuwa na samani za shule za mkoa wa Dar es Salaam. 'Akatishia' hata 'kuwashtaki' TRA kwa Rais. Mambo yakawa kimya hadi sasa inaporipotiwa kuwa TRA wamejaribu kuyapiga mnada bila mafanikio.
Sasa inaarifiwa kuwa RC Makonda amekwenda kanisani 'kufanya maombi maalum' ya kukwamisha mnada wa makontena yake. Ametishia kuwa yeyote ambaye atayanunua atapata laana! Kimsingi, ni Dhahiri sasa kuwa RC Makonda anayatambua na kuyapigania makontena yake. Makontena hayo yana nini hasa? Kwanini yalikuja kwa jina lake?
Namsihi RC Makonda, katika hili la makontena yanayoshikiliwa na TRA, aeleweke. Aiache TRA ifanye kazi yake na si kutaka kuionyesha TRA kama iliyo kwenye 'mission' naye kuyahusu hayo makontena. Mnada ufanyike na mambo mengine yaendelee. Namsihi RC Makonda kuacha pia kuwatisha 'kimaombi' wateja wanaotaka kuyanunua makontena hayo.
Kazi njema wakuu wote!
lakini haya makontena hayana mwenyewe, yaliamua kuja Tz kutembea yakakosa mwenyejiMkuu ina maana wewe vitu vyako vikipigwa mnada utakaa kimya?
Kwan makonda ni nan hasa kias kwamba awanyime uhuru taasisi kubwa ya kiserikali kufanya kazi zake kwa uhuru?
Kuna mambo mengine viongoz Wetu wanafanya kias kwamba unajiuliza uyu mpaka leo anafanya nin kwann asipangiwe kazi nyingine ya kufanya au apigwe tuu chin..!!!!
Uyo jamaa kwa jinsi magu anavyo mlea ipo siku atakuja toa kauli za dhiaka kwa rais na uwongoz wake....
Sent using Jamii Forums mobile app
Laana ya wasiojulikana itamhusu na mzee atamshughulikia mnunuzi tena huenda kupitia TRA hao hao. Msimamo na kiburi cha Makonda dunia nzima inajua kinatoka wapi.Mtu anunue bidhaa kwa hela yake, kwa njia halali kabisa tena hadharani: laana inaingiaje hapa???!! Aisee.... Kazi kweli kweli....
Sent using Jamii Forums mobile app
Sio mimi tu hata Dr.Shika tulikua nae.
Simiyu/katavi loading
Paulo Albert Daudi Makonda Bashite.Hilo dua lilikwenda kwa Mungu kwa jina gani?
Sijui kwanini nashindwa kukubali hili sakata. Naona kama ni sinema ili tuamini kwamba sheria zinambana kila mtu. Usikute hata macontainer halisi yalishatolewa hayo yaliyo hapo ni bosheni tu. Kisa ichezwe movie kutuaminisha kwamba hata viongozi wanadhibitiwa kwenye kulipa kodi.