Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Yeye mwenyewe ameshalaaniwa...
Mzulumati mkubwa nayeye anaanza kupimiwa kile kipimo alichowapimia wananchi.
Yaani kipimo chake kitajaa nakusukasuka.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poor and stupid Makonda. Kwanini asimlaani baba yake aliyeruhusu hayo makontena yaliyoletwa eti kwa ajiri ya kuwasaidia walimu yapigwe mnada?
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda jana alifanya ibada maalum kanisani kwa ajili ya makontena yake yenye samani za shule yanayoshikiliwa na TRA

Katika ibada hiyo Makonda alionya watakao nunua makontena yake watapata laana kali

Pia aliwarushia dongo TRA akisema ni watu wabaya wasio na huruma na kudai kuwa wanamchukia Makonda

"Kama wanachukia Makonda waondoe nembo ya majina yangu kwenye makontena hayo" alisema Makonda

Ni mara nyingine viongozi wa serikali wanasuguana na taasisi za serikali katika kutekeleza majukumu yake huku kiongozi huyo wa mkoa akihisi anaonewa na ni wivu unaofanywa na TRA kisa anafanya vizuri katika mkoa wake

Juzi Paul Makonda alikaririwa na vyombo vya habari kuhusu kupigwa mnada makontena yake,akisema yeye hatishiki na ni mlima hawezi kuyumbishwa na wale wasiomtakia mema katika harakati zake za maendeleo ya Dar es salaam

Kwa hali ilivyo sasa ni dhahiri kuwa Makonda analaumu serikali kumhujumu na hakubaliani na TRA na mambo inayomfanyia
Si alisema anaenda kuwashitaki kwa Baba?
Je huu ndo mwanzo wa mwisho wake?
 
Nilisikiaga kama yalikanwa, kwamba si ya kwake, lakini leo nakutana na kitu tofauti hapa, huenda kuna jambo kubwa zaidi ya hili ambalo tunalijua hapa
 
Back
Top Bottom