Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Hapo ndo tunaposhindwa kuwaelewa wanaume wa DAR yaani mzigo umefika mnatetea mpewe bure si mchangieni kodi makonda mkomboe mzigo ukiona hivyo
Ujuwe scana imeona kuna vitu havihusiani na elimu au waliyoyatoa si watanzania bali mtanzania wa marekani kwa utashi wake binafsi serekali unamkono mrefu kuna kitu nyuma ya pazia hapo amini muda ni mwalimu utakuja kujua
 
Sheria Za nchi lazima ziheshimiwe hatuwezi kusema kwasababu tuna shida kubwa kwenye shule zetu basi tuvunje sheria za nchi Kwa lengo la huruma hapana! Shida zimekuwepo siku zote na hazitamalizwa Na haya makontena 20 Hata siku moja!

Tukiruhusu hili Leo la Makonda basi kesho tutasikia friends of Mtaka kutoka Belgium wameleta contena 50 ya vifaa vya mahospitali, kesho kutwa friends of Gambo kutoka Canada wameleta contena 100 ya vifaa vya michezo mashuleni, week ijayo friends of Mongela wameleta contena 200 ya vifaa vya usafi mashuleni, then Friends of Mndeme RC Ruvuma ataleta contena 300 Za pads Kwa ajili ya watoto wa kike mashuleni!

Hata mbuyu ulianza kama mchicha!

Wasalam,
Nkonkilangi, Iramba Singida
 
Wasalimie wakina gullo shumbi mkuu
 
Hivi ni kweli tumeshindwa kutengeneza madawati na viti vya walimu hapa nchini mpaka tuombe nje!? Misitu ipo mafundi selemala wapo.. Na vitabu tumeshindwa kuchapisha mpaka tuombe msaada? Au hayo makontena yana vitu gani ambavyo bongo haguwezi kutengeneza? Na pia serikali haina pesa yakununua mpaka iombe msaada?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Suali una uhakika upi ukitoa msamaha vitu vilivyoandikwa Pascal Mayalla baada tu ya zile geti za bandari zitaenda shuleni au bar?

Suali la pili kwa kuruhusu utaratibu huo mie kesho pia nataka nilete msaada kwa jina langu, nikinyimwa msamaha wa kodi haitakuwa double standard?

Jibu la hili sakata lilikuwa rahisi tokea awali document zingesoma taasisi za serikali bado coordinator angetambuliwa.
 
Hii tabia ya kutaka mtu aruhusiwe kwenda kinyume na Sheria au kutofuata utaratibu eti tu kwa sababu "ana nia njema" itakuja kuangusha hili taifa.

Nia kamwe haiwezi kupimwa kwa maneno tu. Kama una nia njema fuata utaratibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
serikali inashindwa nn kuvitaifisha na kuvisambaza yenyewe mashuleni kwa kuangalia uhitaji chini ya wizara ya elimu..

maana ni kweli mazingira ya waalimu hayako poa kabisa kiuhalisia..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo point yako ni kuwa waachwe wote waendelee kuvunja sheria za kodi?
Na wewe leta 'samani' afu ufanye ubabe qa Makonda uone kitakachokukutq.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
acheni kutumia mgongo wa huruma ya elimu na walimu kutimiza matakwa ya kisiasa ..... kwanza timizeni ahadi mliyotoa kwenye kampeni 2015 ya kuwagaia walimu wote laptop
Halafu kama vilikuwa vifaa vya elimu iweje vije kwa jina lake?? Halafu mme angalia vyema vilivyomo kwenye zile container au wana amua tuu kumtetea Makonda?? Maana vifaa vilivyomo sio vya shule kama inavyo semwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Sheria zipo na hazikutungwa kwa ajili ya Makonda
 
kwa muda mrefu watu wamelalamikia utendaji wa mkuu wa mkoa wa Dar, Ndugu Makonda lakn serikali hiyo hiyo ilimkingia kifua na kusema chapa kazi.

kwa nchi zingine ilitakiwa awe nje ya ofisi za umma kwa kitendo chake cha kuwataja watu mbali mbali kwamba wanahusika na uuzaji wa madawa ya kulevya lakn wale watu wameonekana ni watu safi . lakn wakati anawataja watu mbali mbali walilalamika kwamba nia yake ni kuwachafua maana anawaomba hela wanamnyima. ilionekana ni kelele za mtandaoni tu.kwa sababu ushahidi alikua hana ilitakiwa yeye ndio awajibike!!!

sasa kumetokea yeye kujaribu kukwepa kulipa kodi. baada ya serikali kutangaza kuyauza kaenda makanisani kutangaza walaaniwe watakaonunua!!! serikali haijamchukulia hatua yeyote. sasa swali nani atakaye kuwa tayari kununua vifaa hivyo?? nani anataka kulaaniwa?? mnajua laana anayoiongelea?? labda atawalaani yeye mwenyewe!!

mimi natabiri hakuna mtu atakaye jitokeza kununua makontena hayo ya simba wa Dar es salaam. maana ukinunua na akajua ww ndio umenunua sio tu atakutaja kama muuza unga bali pia anaweza kukutaja kama muuza vichwa. mnajua kesi mbaya ukitoka ya madawa ni ipi?? mimi ninavyojua ile ilikua mbaya sana na inayofata kwa ninavyojua ni ya kichwa. sasa nani anataka kuchafuliwa?? maana hakuna atakaye watetea wenye pesa, ila atasifiwa yeye kwa kuambiwa chapa kaziiiiii!!! huku watu wako jera!!

serikali mmemlea wenyewe madhara yake hamkuyajua ila mtayaona kwenye huu mnada. huyu mtu anaogopeka hatari. kama hamjui hakuna atakeye nunua makontena yake. mnataka afanywe nini na huyu simba wa Dar es salaam???

mmemlea wenyewe sasa ngoja awaonyeshe nguvu mlizompa.huyu mtu anaogopeka mnoooo!!! nani wa kununua kitu chake?? labda kama hajipendi???
 
Jiji la Dar kwa sasa ni sehemu salama sana tokea enzi za Mwalimu,panya Road wameishia jela, mateja yote yamesekwa Rehab,Dar inapendeza..Vigelegele waTanzania.
 
Kalelew na serikali au kalelewa na sizonje ?

Sent using Jamii Forums mobile app

huwez kuitaja serikali bila kumtaja Sizonje!! kama yeye ndio alimkingia kifua nani wa kumkosoa?? nasema chapa kaziiiiiiii!!! ww ndio mkuu wa mkoa bora kuliko wengine!! nukuu toka kwa sizonje!! naye akasema anaenda kusema kwa baba kama hammuupi msamaha!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…