Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Jiji la Dar kwa sasa ni sehemu salama sana tokea enzi za Mwalimu,panya Road wameishia jela, mateja yote yamesekwa Rehab,Dar inapendeza..Vigelegele waTanzania.
Kwa kweli!
 
Ondoa upuuzi wako wewe kijana mdogo!
 
Siku ya Jumapili wakazi wa jiji la Dar es Salaam na viunga vyake mnashauriwa kukaa mkao wa kiroho maana Mtumishi wa Baba askofu Josephat Gwajima
Asiyependa kuficha maovu ataweka kila kitu hadharani
Huenda nafasi ya wote kuingia kanisani ikakosekana lakini mpango unafanywa ili ibada iwe youtube live

Kwa hisani ya Dada wa Taifa
Screenshot_20180830-104042.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anajua Hakuna wa Kumgusa kwa Sababu anazojua yeye na alijua TRA watamuogopa kwa kuwa Mtoto pendwa kuliko wote na Mkulu kumbe kuna watu hawataki ubabaishaji kwenye kutekeleza majukumu yao waliyopewa na watanzania hasa kwenye kusimamia sheria! Pongezi nyingi kwa Philip Mpango na TRA, hakuna double stardand ili Tz isonge mbele. Tunasubiri maamuzi ya ngazi ya juu kuhusu nafasi yake, Hatufai kabisa huyu Bashite!
 
Makonda haogopwi, anaogopwa aliye nyuma yake. Na kwa sasa inaonekana back-up imepungua kidogo.
 
Msamaria ni mtu anayejitoa kumsaidia mhitaji, si kwamba anaweza akawa anacho kikubwa la hasha bali ni mtu aliyejaaliwa kutoa kwa ajili ya wengine na kama hana basi hata kufanya mipango ya kupata kwa mwingine ama wengine.... Wasamaria ni watu wa kaliba ya aina yao...kwakuwa hawa ni tofauti kabisa na wahisani na wafadhili... Wanaotoa kwa malengo maalum

Kama taifa tu vijana wetu, ndugu zetu jamaa na watanzania wenzetu walioko nje ya nchi... Ughaibuni! Hawa kati yao kuna wanaosoma na wengine ni wafanyabiashara, wafanyakazi nk... Hawa ni watu wanaofahamu kwa undani matatizo ya nyumbani na kuguswa vilivyo nayo...
Ni hawa ndugu zetu kupitia vyama vyao (diasaporas) nk wamekuwa wakijitoa kusaidia nyumbani kwa hali na mali kwa kile kidogo wanachopata..hasa kwenye majanga na dharura za nchi.. Kiukweli tumeona juhudi na jitihada zao na kutowashukuru ni kukosa shukrani
Kwenye msafara wa mamba kenge pia wamo.... Pamoja na sifa zote hizo lakini kuna wakati huwa ndugu zetu hawa wanatumika vibaya na pengine bila wenyewe kufahamu

Sakata la makontena 36 yaliyojaaa samani za shule lina sura nyingi za kuchanganya, kuvutia na kuchukiza pia... Mijadala imekuwa mingi lakini naamini kuna maswali ya msingi mpaka sasa hayajaulizwa.. Ngoja tuyapitie baadhi
. Chama cha wasamaria wetu waliotoa huo msaada kinasemaje? Mbona wako kimya? Au hawaguswi na msaada wao kuwa na danadana na sintofahamu nyingi?
. Kwa mzigo mkubwa kama ule kwa hakika pesa iliyotumika si haba na wahisani waliochanga wako vizuri... Hivi hawana uchungu wa kuhoji chochote?
. Wakati wa bakuli la mchango kupita, je walijulishwa kwamba wanachangia shule za Dar tu!? Nina hakika si wote wanatoka Dar
. Je wakati wa kupitisha bakuli la mchango waliambiwa kwamba wanamchangia mtu halafu akawakilishe au wanachangia taasisi?
. Je waliridhia shehena ya mzigo waliojichangisha kwa ajili ya shule za serikali uandikwe jina na anuani binafsi?
. Kama baada ya kuhangaika kote huko na kufanikiwa kupata samani zilizojaza makontena 36, je Kwanini sasa wako kimya kabisa!? Kama waliweza kula ng'ombe mzima Kwanini washindwe na mkia?
. Swali la mwisho.. Yako wapi makontena 16 ya mwanzo yaliyofanikiwa kutolewa? Je kuna shule zilifanikiwa kupata chochote?

Mwisho mamlaka husika zingejitokeza kutoa ufafanuzi kwenye hili kuliko kuliachia lielee tu na kusambaa kiholela kila mtu akiongea lake
Hili litasaidia mno kuondoa sintofahamu iliyojitokeza na pia kutowavunja moyo wahisani wengine hapo mbeleni lakini kubwa kuliko yote kuipa serikali heshima inayostahili na kuiepusha kutumiwa vibaya na wapuuzi wachache



Jr[emoji769]
 
Anajua Hakuna wa Kumgusa kwa Sababu anazojua yeye na alijua TRA watamuogopa kwa kuwa Mtoto pendwa kuliko wote na Mkulu kumbe kuna watu hawataki ubabaishaji kwenye kutekeleza majukumu yao waliyopewa na watanzania hasa kwenye kusimamia sheria! Pongezi nyingi kwa Philip Mpango na TRA, hakuna double stardand ili Tz isonge mbele. Tunasubiri maamuzi ya ngazi ya juu kuhusu nafasi yake, Hatufai kabisa huyu Bashite!
Jumapili wote kwa Gwajima - JamiiForums huyu hapa wa kugusa...
 
Write your reply...kwani kuna ubaya gani mtu kula kazini kwake.?hawajui kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba na kwamba ukiipata nafasi usi ichezee.??
mkuu hii ni point muhimu inayoelezea tulivyo wabinafsi, kuwa tukipataga nafasi twajaza matumbo yetu, alichofanya huyu ndg ni kawaida ya kibinadamu lkn ni kuiibia serikali kodi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom