Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumbe yameshafunguliwa!?Wapinzani uchwara walikuwa wanasema ati makontena yamejaa samani za majumbani pamoja na Toyota SUV moja,lakini kwa sasa yameshafunguliwa wamekuwa wakimya sana...Wapinzani Uchwara acheni fitna.
hapo kuna mtego na unaweza kwenda ndivyo sivyo ukatumbuliwa cha msingi kufuata taratibu walizpjiwekea tra kuhusu bidhaa za aina hiyo zinazo ingia.Kama ni vifaa vya Shule wangemwachia tu, akavisambaze mashuleni au hao TRA wakasambaze mashuleni kuliko kukaa nayo
Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa kwenye mnada utamuuzi mtu mbuzi kwenye gunia.Kumbe yameshafunguliwa!?
[emoji252] [emoji479]
ina maana kipenzi chake mkulu naye amekaa kimya akisikilizia inshu hapo patamu,maana hata tra nao matumbo moto hawajui wafanye nn,usishangae WAKAYAPIGA mnada akayanunua tena mwenyewe hii ndio TZ,Taarifa huripotiwa kwenye vyombo vya habari kama runinga, redio, magazeti, majarida na mitandao ya kijamii. Iliporipotiwa taarifa ya uingizwaji na uwepo wa makontena yenye jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mwanzoni iliripotiwa kuwa Makonda 'aliyakana' makontena hayo.
Baadaye, ripoti zinadokeza kuwa RC Makonda 'aliyatambua' makontena hayo yaliyokuwa mikononi mwa TRA na kudai kuwa yalikuwa na samani za shule za mkoa wa Dar es Salaam. 'Akatishia' hata 'kuwashtaki' TRA kwa Rais. Mambo yakawa kimya hadi sasa inaporipotiwa kuwa TRA wamejaribu kuyapiga mnada bila mafanikio.
Sasa inaarifiwa kuwa RC Makonda amekwenda kanisani 'kufanya maombi maalum' ya kukwamisha mnada wa makontena yake. Ametishia kuwa yeyote ambaye atayanunua atapata laana! Kimsingi, ni Dhahiri sasa kuwa RC Makonda anayatambua na kuyapigania makontena yake. Makontena hayo yana nini hasa? Kwanini yalikuja kwa jina lake?
Namsihi RC Makonda, katika hili la makontena yanayoshikiliwa na TRA, aeleweke. Aiache TRA ifanye kazi yake na si kutaka kuionyesha TRA kama iliyo kwenye 'mission' naye kuyahusu hayo makontena. Mnada ufanyike na mambo mengine yaendelee. Namsihi RC Makonda kuacha pia kuwatisha 'kimaombi' wateja wanaotaka kuyanunua makontena hayo.
Kazi njema wakuu wote!
hahaha kabisa yaninachomkubali bashite hana aibu
Kwa hiyo wewe unajua kuna nini kwenye hayo makontena?Sasa kwenye mnada utamuuzi mtu mbuzi kwenye gunia.
Madeksi na ubao wa kufundishia.Kwa hiyo wewe unajua kuna nini kwenye hayo makontena?
Hebu tusimulie tukamate fursa
[emoji252] [emoji479]
Madeksi hapo sijaelewa ni kitu ganiMadeksi na ubao wa kufundishia.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda jana alifanya ibada maalum kanisani kwa ajili ya makontena yake yenye samani za shule yanayoshikiliwa na TRA
Katika ibada hiyo Makonda alionya watakao nunua makontena yake watapata laana kali
Pia aliwarushia dongo TRA akisema ni watu wabaya wasio na huruma na kudai kuwa wanamchukia Makonda
"Kama wanachukia Makonda waondoe nembo ya majina yangu kwenye makontena hayo" alisema Makonda
Ni mara nyingine viongozi wa serikali wanasuguana na taasisi za serikali katika kutekeleza majukumu yake huku kiongozi huyo wa mkoa akihisi anaonewa na ni wivu unaofanywa na TRA kisa anafanya vizuri katika mkoa wake
Juzi Paul Makonda alikaririwa na vyombo vya habari kuhusu kupigwa mnada makontena yake,akisema yeye hatishiki na ni mlima hawezi kuyumbishwa na wale wasiomtakia mema katika harakati zake za maendeleo ya Dar es salaam
Kwa hali ilivyo sasa ni dhahiri kuwa Makonda analaumu serikali kumhujumu na hakubaliani na TRA na mambo inayomfanyia
Madeksi hapo sijaelewa ni kitu gani
Hizo mbao Za kufundishia wakagawe mashuleni.
[emoji252] [emoji479]