Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Taarifa huripotiwa kwenye vyombo vya habari kama runinga, redio, magazeti, majarida na mitandao ya kijamii. Iliporipotiwa taarifa ya uingizwaji na uwepo wa makontena yenye jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mwanzoni iliripotiwa kuwa Makonda 'aliyakana' makontena hayo.

Baadaye, ripoti zinadokeza kuwa RC Makonda 'aliyatambua' makontena hayo yaliyokuwa mikononi mwa TRA na kudai kuwa yalikuwa na samani za shule za mkoa wa Dar es Salaam. 'Akatishia' hata 'kuwashtaki' TRA kwa Rais. Mambo yakawa kimya hadi sasa inaporipotiwa kuwa TRA wamejaribu kuyapiga mnada bila mafanikio.

Sasa inaarifiwa kuwa RC Makonda amekwenda kanisani 'kufanya maombi maalum' ya kukwamisha mnada wa makontena yake. Ametishia kuwa yeyote ambaye atayanunua atapata laana! Kimsingi, ni Dhahiri sasa kuwa RC Makonda anayatambua na kuyapigania makontena yake. Makontena hayo yana nini hasa? Kwanini yalikuja kwa jina lake?

Namsihi RC Makonda, katika hili la makontena yanayoshikiliwa na TRA, aeleweke. Aiache TRA ifanye kazi yake na si kutaka kuionyesha TRA kama iliyo kwenye 'mission' naye kuyahusu hayo makontena. Mnada ufanyike na mambo mengine yaendelee. Namsihi RC Makonda kuacha pia kuwatisha 'kimaombi' wateja wanaotaka kuyanunua makontena hayo.

Kazi njema wakuu wote!

Mh usiogope vitisho vya DAB eti munuzi atalaaniwa, nakushauri kama unahitaji kitu nenda kanunue mkuu. Huyo Bashite ana usafi gani wa kutishia watu na laana zake??
 
Kwan makonda ni nan hasa kias kwamba awanyime uhuru taasisi kubwa ya kiserikali kufanya kazi zake kwa uhuru?

Kuna mambo mengine viongoz Wetu wanafanya kias kwamba unajiuliza uyu mpaka leo anafanya nin kwann asipangiwe kazi nyingine ya kufanya au apigwe tuu chin..!!!!

Uyo jamaa kwa jinsi magu anavyo mlea ipo siku atakuja toa kauli za dhiaka kwa rais na uwongoz wake....

Sent using Jamii Forums mobile app

Babake alimlelea hivyo kwa kumsikilizaa hata pale anapofanya ujinga, baba anampa heko! Hapo unategema nini mkuu? Sasa hivi anampanda babake kichwani, hadi anazuia taasisi za serikali zisifanye kazi!! Beside, huu cares, nchi ipo mikononi mwa...... (Refer Zitto)
 
Mie naona kama ni vifaa vya shule na Makonda alikusudia kuyasambaza mashuleni,washirikiane na TRA shule zipate vifaa.

Wakipiga mnada ina maanisha shule binafsi zitanufaika zaidi

[emoji252] [emoji479]
Hapa naona kuna zaidi ya samani za shule.
Maana hili suala lingeisha zamani kama ni vifaa vya shule kweli
Laiti tungeona hata picha tu turidhike



Sent from my SM using Tapatalk
 
Swali langu moja tu....mtu makini kabla ya kuagiza mzigo nje anacheki na TRA kama mzigo huo utatozwa kodi au una kidhi vigezo vya msamaha, na kama kuna kodi anacheki ni kiasi gani ili ajiandae. Sasa makonda kabla hajaomba hiyo misaada huko nje, kwanini hakucheki na kujiridhisha na TRA kuhusu mambo ya kodi? Au alijua kwamba kodi itatozwa lakini kaagiza mizigo ije makusudi ili aanze kutafuta huruma za public?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ni makontena ya Serikali wala hakunaga tatizo unatoa bila hata senti tano, hapo kuna tatizo tu, kwa nini hakuandika Jina la Ofisi yake? angeandika Regional Commissioner, Dar es Salaam unafikiri angetumia nguvu yaani yangeenda kutolewa kiulaini na maofisa wake.
 
Makanisa ya siku hizi yamekuwa hayana misimamo, na Kwakuwa wanasiasa wanafahamu hilo watayatumia kisiasa pia. Kanisa la sasa litakuwa kama kijiwe cha wanasiasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makonda mwisho wa Siku kuna sheria za nchi..watu wote tunalipa Kodi wote na Serikali inasema kila mtu alipe Kodi ili itumike kufanya kazi za maendeleo.

Leo akija kila mtu na sera zake kwamba asilipe kodi manake taratibu zimevunjwa...tutakosa pesa na miradi itasimama miingi...

Kwa hili la Kodi ningemshauri asome kwamba sasa hata wakubwa wake wameamua kuuchuna na kufata taratibu..manake ajue sasa maisha yanabadilika hata yeye anatakiwa kutii sheria.
 
Mungu akamwambia mfalme Daudi, 'kamwe wewe huwezi kunitolea sadaka madhabahuni kwa kuwa mikono yako imetapaa damu za watu'.
 
Makonda bwana ana akili za kipimbi sana. Sijui magufuli alimpaje kaz ya kuongoza mkoa mkubwa kama dsm.
 
Back
Top Bottom