Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

jamani vitu vingine tuwe na akili hivi unadhani magufuli au serikali itakuwa haijui kuwa makonda aliagiza hizo furniture kwa ajili ya kusaidia?
 
Kwanza salaam zako Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,

Tumefuatilia suala ilo na kuguswa na namna ambavyo juhudi zako zimegonga mwamba za kuhakikisha walimu wanapata teaching aids na wanafunzi wanapata learning materials,

Mkuu wa Mkoa sisi ma diaspora tumeguswa sana na jinsi ambavyo makontena hayo uamezuiwa mbaya zaid kuna vi kashfa fulani fulani tunaomba uweke Sawa taarifa hizi ili utupe imani ya kuchanga bila wasiwasi,

1. Tunaomba tujue idadi ya makontena yaliyotumwa na mangapi yameshatoka bandarini mangapi hayajatoka na yaliyotoka yako wapi yametoka lini na yamegawiwa shule zipi?

2. Kwanini usifanye utaratibu kubadili majina yakawa ya wizara ya elimu Tanzania kuliko kuwa na jina lako pale, ili tujiridhishe kwamba nia ni kusaidia elimu na si vingine,

3. Kwanini usiruhusu au usikubali kukaa meza Moja na waziri mkapanga kwamba yauzwe nusu Hela inayopatikana ilipie mengine yatoke na yagawiwe bule,

4. Tuna omba orordha ya watu waliofanya donation na address zao kupitia magazeti ya serikali,

5. Alafu Tunaomba maelezo mbona asilimia kubwa ya furniture zile ndo kama zinazouzwa kwa ajili ya maofisi na receptions au nia yako haikuwa madawati ilikuwa kwa ajili ya Meza tu?


Mwisho utupatie uhamasishaji tuchangie kiasi kitakacho kosa makontena yatoke yakabidhiwe wizara ya elimu ndo wagawe hayo madawat na meza


Nathan JR
00069 PGH Finland. Sörnäisten rantatie 18 F Helsinki. H
+380686706696
Njaaa itakuuwa wewe yaani naona umechoka kubeba mabox huko ulipo?kwa taarifa yako huku Bashite hana tena issue

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaandika majina ili yajulikane ni juhudi zake sasa wewe unaleta hadithi ya kuyageuza yawe ya wizara ya elima sasa huoni unaenda against na mpango wake wa kujitengenezea publicity kwenye jamii ili ateuliwe kuwa waziri wa mambo ya ndani then agombee urais

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona hakupata maelekezo vizuri kutoka kwa muhusika yaani Bashite

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiukweli na bila hiyana alichokifanya mh Paul Makonda ni sahihi kwa maendeleo ya elimu mkoani kwake.Kama kuna ukiukwaji wa namna ya kuagiza ni vema serikali ikamsaidia na kusimamia ugawaji wa vifaa hivyo vya kuboreshea miundombinu ya elimu yetu.Nampongeza kwa juhudi zake za kusaidia elimu mkoa wa Dare salaam na amefanya hivyo kwa sababu yeye ni mkuu wa mkoa mmoja hivyo anajijenga kwa ajili ya mkoa wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo containers ni mali ya Makonda,ndio maana yamekuja kwa jina lake.Alipe kodi,akishindwa yauzwe serikali ipate mgao.
Hao ma diaspora kwanini wasingetuma hela madawati yachongwe huku Tz kuepuka hiyo adha wanayoipata sasa!
Inaweza kuwa wamepata bure,lakini gharama ya kuzisafirisha na hiyo kodi bora wangenunulia fenicha huku Tz.
Mkuuu fanicha nje n cheap compared na hapa bongo ndo maana wali imports

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani hapa shida ni hofu na kutokujua au kotokutazama mbali. Ukitizama karibu - short sight kama viongozi hawa wanadai sheria - in long range utakosea. Mangalizo ni mawili au matatu:
1. Consignment ikiwa katika jina la binafsi - RC kisha kuomba msamaha wa kodi kwa msingi ni sahihi sana hasa ikiwa kwamba nia ya matumizi iko wazi na tayari ana zoezi la kuboresha ofisi za walimu na tayari ameshajenga majengo kadhaa, zahanati, maabara etc kwa kuchangisha watu wa ndani wafanya biashara nk. Je kodi kiasi gani ilikusanywa kama capital gain kwa michango hiyo? Ni swali tu anyhow hakuna sheria duniani bila exception. Kila mtanzania alipe kodi na hapo hapo unakuta kuna watu wamekuwa exempted. Mathalani - Watu wote endesha gari kushoto lakini tunaona watu kadhaa na ving'ora wakiendesha kulia bila kujali mwendokasi mtoroko. Hizi ni exception. Sasa hapa ni hekima tu ingetumika zaidi ya kutunishiana misuli na kuleteana stress.

Swali jengine - naljiuliza sasa akiisha RC kulipia kodi je? mtatamani aendelee kugawa bure kwa shule za Dar au mtamshitaki akiuza samani hizi? Najiuliza tu. Aibu kweli kwa hawa wapinzani wetu wa maendeleo.

2. Consignment ikiwa katika jina la taasisi say Ofisi ya RC - hapa sasa ndiyo penye mkanganyo kwa kuwa sasa je serikali ingetumia kodi iliyokusanywa kulipa kodi? Huu ni upuuzi na upotevu wa hesabu za serikali. Anyhow I stand to be corrected BUT kuhusu hili suala la madawati na social service needs nadhani hekima imekosekana au ulevi wa madaraka. Viongozi wakikosa hekima katika madogo huleta fedheha.

3. Double taxation - Nchi yetu ina tatizo kubwa la double taxation yaani usipoangalia unaweza lipa hadi 60% 70% 80% 100% 110% hata 200% kodi na ukaishia kubaki hauna chochote. Hii inadidimiza pia maendeleo kwa kuwa inakuwa illogical to do business

Anyway kupenda vya bure hizi ndiyo gharama zake. Tutamlaumu nani sasa kwa umaskini wetu? Serikali iweke mahitaji ya elimu yakidhi haja, hii itakuwa suluhu ya kudumu kwani ni aibu sana kusema elimu bure ikiwa huwezi kuhudumia kwa kiwango cha ubora na inakuwa bora elimu bure badala ya elimu bora na bure.

FINDINGS:
Huyu RC hata kama hana PhD asiitafute kwa kuwa imeonyesha hawa wenye hizi degree wameshindwa hata kusababisha maendeleo si tu kwa maandiko ya PhD zao bali hata kwao wenyewe. Sasa mfano mkubwa ni PhD holder anapokimbilia siasa katika nchi changa kama Tanzania na kuacha job creation, inaonesha hamna creativity and so big failure. Kuwa kiongozi wa kisiasa sio professionalism, it is about moral judgement and ethics. Hawa wasomi wetu hawana moral judgement and ethics. Example: Samani zipite, zitanufaisha wengi na tutapata leverage ya kodi. Kimsingi nchi ilipasa kupamtia RC comission kwa kufanya jambo kama hili na siyo kuhitaji tena kitu kidogo kuotka kwake. Yeye alishafanya homework yake. Sasa kila mtanzania akifanya jambo creative la kimaendeleo baada ya mwaka mmoja sisi ni first world ikiwa viongozi wote wangekuwa kama huyu RC na siyo kama hawa wengine..

Naomba kuwasilisha
Hopefully una CPA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom