Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Mkiendekezi hii tabia, ipo siku mtu ataingiza mizigo yake kwa style hii ambayo kwanza hakuna mwenye uhakika kama vifaa hivyo vyote kweli vinawafia walengwa au ni janja tu.

Na kwa jinsi jambo hili linavyokwenda mpaka sasa, ni dhahiri unahitajika uchunguzi wajulikane ni kina nani walituma vifaa hivyo na shule gani hasa zilizolengwa kupewa hiyo misaada.

Hili jambo lina ukakasi unaohitaji uchunguzi maana huenda si kila kifaa kitaenda kutolewa kama msaada.

Na nikwambie tu, vifaa hivyo vingekuwa vimeingizwa na mtu kutoka upinzani, vingeshapigwa mnada siku nyingi tena huyo Makonda angeweza hata kuingilia viuzwe haraka japo kisheria hahusiki.

Tena namshauri waziri Mpango awe makini na kama kuna mtu atamshinikiza atoe msamaha,basi ahakikishe mtu huyo anatoa agizo kwa njia ya maandishi vinginevyo ajiuzulu kwani ipo siku anaweza kuja kujikuta anawajibika kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuikosesha serikali mapato(sheria tunatunga wenyewe na kuzipitisha kwa mbwembwe).

Wanasiasa sio watu!!
Umeandika vizuri kabisa ! Big up ! Hapa palikuwa panachezwa mchezo nchafu hakuna lugha nyingine !!
 
Walimu gani wanaagiziwa vitanda. Kwenye makontena kuna fenicha za hoteli ndo maana kaagiza kwa jina lake.
 
Kwanini Makonda asivilipie kodi hivyo vitu? Maana kwa kufanya hivyo atakuwa ni mzalendo mara mbili
1. Kodi yake itasaidia nchi
2. Vifaa vyake vitasaidia juhudi za elimu
 
Naungana na mtoa post kupinga vikali upigwaji mnada vifaa hivo tena vya msaada, japo nakiri kwel Makonda kukosea hasa pale alipo amua kutumia jina lake badala ya taasis ya Elimu.

Bado nawasihi viongozi watumie busara na hekima hasa katika utatuzi wa matatizo mbali mbali ili kutoleta sintofaham kwa umma zisizo na tija kwa jamii.

Da Pride

Sent using Jamii Forums mobile app
 
watu wenye akili za namna hii sijui wametoka wapi
hivi hakuna asiyemjua makonda kuwa ni mpiga dili
mtu ana kila aina ya tuhuma
eti ameagiza kwa jina lake kwa ushauri mbovu wa wasaidizi!!!!really!!!
ningekuwa karibu na wewe ningekutia ngumi
 
Kwa nini mwanzo alikataa makontena si yake halafu baadae ndio aje kukubali. Makonda anafanya kazi lakini hapa kachemka, sasa kila mtu akileta mizigo kwa jina lake akijidai ni msaada na asemehewe kama Makonda sheria itakuwa imetupwa mbali sana. Sheria ichukue tu mkondo wake kama kawaida. Hatufurahii viuzwe lakini Makonda mwenyewe alishaonyesha mashaka kipindi alipoyakana.
nasikia leo tena kayakana wakati anazindua sijui ndiyo tume ya waliotelekezewa watoto
 
Ni kitu cha kushangaza kuona uwepo wa taarifa ya familia moja yaani watoto wa baba mmoja kugombana hadharani kwa vitu vidogo ambavyo vinaweza kumalizwa aidha na wakubwa zao kiumri au wazazi wao, hapa namaanisha baba au mama ndani ya familia.

Ugomvi unao dharirisha familia, ugomvi unao ruhusu majirani kuwasema vibaya,
unaonesha hakuna mawasiliano mazuri ndani ya familia moja.

Kwanini haya yanatokea, ni uoga, kumuogopa baba yao au ni misimamo tu.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Makonda aliomba msaada kutoka Kwa watanzania wanaoishi marekani thamani pamoja na vifaa vya mashuleni, vifaa hivyo vimekuja lakini vimekwama bandarini Kwa sababu ya kodi, waziri wa fedha pamoja na mamlaka ya mapato wanao shughurika na kodi wametoa Kauli yao kwamba vifaa hivyo vimekuja lazima vilipiwe kodi na Kama sivyo vitapigwa Mnada Kama sheria inavyotaka.

TATIZO NINI?
vifaa hivyo ingawa ni vifaa kwa ajili ya mashuleni, lakini havikuja kwa Jina la wizara husika, ila vifaa hivyo vimekuja kwa jina la Paul Makonda, hii inamaana kwamba ni vifaa vyake yeye mwenyewe anataka atoe msaada yeye mwenyewe au labda kwa niaba ya hao rafiki zake wa ughaibuni, sasa kwa utaratibu wa sheria za kodi kuna vitu ambavyo vinamsamaha lakini Mkuu wa Mkoa hana msamaha wa kodi kwa vitu vyake anavyoagiza au kupewa toka nje ya nchi labda kwa maelekezo toka kwa mwenye madaraka makubwa kuliko yoyote ndani ya nchi.

KIPI KIFANYIKE!
Mkuu wa Mkoa aidha alipe kodi, au vile vifaa vikiwa palepale bandarini aandike barua kwa waziri wa fedha kupitia mamlaka ya mapato, akivitoa vitu hivyo kwa wizara husika, wizara ya elimu, akielezea ujio wa hivyo vitu hapa nchini kwa lengo la kutokomeza mazingira magumu mashuleni, sasa wizara husika ndiyo itashughurika na kodi kama kuomba isamehewe au kulipa, kwasababu bajeti ya kununua thamani mbalimbali mashuleni naamini ilikuwepo kama kuna huu unafuu wanaweza kulipa kodi.

HAIWEZEKANI.......!!!!!!!
haiwezekani husamehewe kodi kwa vitu ulivonunua au kupewa iwe unataka kutoa msaada au kugawa bure kama sheria haijatoa maelekezo tofauti haiwezekani ata umwambie prezo hiyo sahau, sio kwa jina lako, waziri na mamlaka ya mapato wako sahihi.

SWALI LA KUJIULIZA....?
hivi kweli mmeshindwa kuwasiliana kiofisi na kuyamaliza kiofisi hadi mnaongea kwenye madhabaho ya kanisa, kwenye mitandao ya kijamii?

Mmeshindwa kulifanya hili jambo kuwa ni la ndani kwa kupeana maelekezo kupitia vi- memo?




Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna wanaodhani wapo juu ya kila kilichopo nchini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila mmoja yuko sahihi Kwa tafsiri yake, Mr planner anasimamia Sheria, baba k anasimamia siasa( kiki).Inatakiwa awe mfano wa kulipa kodi Kwa vitendo ili wengine wafate,baba mwenye nyumba anahimiza watu kulipa kodi iweje mtoto awe mfano mbaya wa kutokulipa kodi.Ingekuwa ni upinzani ndo wangeagiza visingekaa hata miezi 3 storage siku nyingi vingeshapigwa mnada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza kwa mlio walimu mtanielewa ninaposema waziri kakurupuka wala hazijui changamoto za elimu
ukisikiliza kwa umakini kwenye hotuba yake ya juzi utagundua kabisa aelewi anachokiongea...

Anaongelea maswala ya elimu bure kitu ambacho ni nje kabisa ya mada ya makontena

swala hapa ni vifaa kwa ajiri ya kusaidia elimu ya dsm ambayo ina changamoto nyingi ikiwa na mrundikano wa wanafunzi na mambo kibao

Makonda inawezekana kuna sehemu alikosea katika mchakato huo lakini serikali walitakiwa kuwa wajanja wangeruhusu kwanza vitu viingie ndio waanze kuvimonitor wapate ushahidi wa kutosha ndio waje kumtuhumu.

matokeo yake wananchi nao wameyabeba na kusahau watoto wao ndio wanakaa chini milele
mimi niko na ushahidi kabisa nilienda shule moja na taasisi fulani kutoa msaada wa computer lakini unakuta walimu stafu viti tu vya kukalia haviwatoshi hii ni aibu kama mwalimu hana kiti stafu mwanafunzi je darasani itakuwaje?

tukiweka siasa pembeni Makonda yupo sahihi kabisa na ana nia njema ingawa anaweza kuwa kafanya makosa kutumia jina lake kwa ushauri mbovu wa watendaji waliopo chini yake lakini naamini tatizo letu la elimu ni kubwa mno kuliko jina la makonda kuwa kwenye makontenana hili swala tunalibabe kishabiki sana kama kawaida yetu...

kwamba mimi ni chadema Gambo akifiwa na mzazi wake nashangilia, mimi ni ccm Sugu akipata msiba nashangilia upuuzi mtupu.

Hivi waziri anavipiga mnada vitu vya shule za dsm watu tunashangilia leo halafu kesho jangwani secondary inakuwa ya mwisho tunaanza kumponda makonda ...

Hivi vitu vikinunuliwa na wafanya biashara sisi wananchi wa kawaida tutafaidika vipi direct kama ambavyo tungeviona kwenye shule zetu? namimi naongeza na alaaniwe kabisa atakae vinunua.

"Form four wanakaribia pia kuanza mtihani msisahau kuleta mrejesho hapa wa shule za umma"

Popote nikona maneno hayo kwenye red najua msemaji ni tikiti maji kichwani, ukiwa na kitu kichwani utakuwa mpuuzi kuamini mtu au kiongozi kushauriwa vibaya na watu wa chini yake. Ukiona unashauriwa vibaya na huyo wa chini yako tafsiri yake you are not competent enough na bora umuachie huyo mshauri kiti chako. Tukubali kusema kiongozi fulani kakosea, awe nani au kiongozi mwenye ndevu hadi kwenye magoti akikosea tuseme kakosea ama kwa kutokujua au kwa kupuuzia siyo kusingizia washauri.
 
Ignorance ya Makonda kisiwe kisingizio cha kutokufuata sheria. Makonda anajulikana kuwa sio muadilifu kwani alipiga sana enzi za Home Shopping Centre hivyo ni vigumu kumuamini kuwa kweli alikuwa na nia njema na hayo makontena. Toka akiwa DC anajua wazi kuwa kama hayo makontena yangeletwa kupitia registered NGO na sio jina lake , yangeweza kuingizwa bila Ushuru!! Lakini Makonda for reasons best known to the powers that be thinks that he is above the law!! Rais kuingilia sakata hili na kuruhusu sheria kuvunjwa atakuwa ana create a disastrous precedent kwa watendaji wa serikali.


Hivi ule msikiti au Ofisi za BAKWATA vile alioahidi Mr Makonda je alishamaliza kuwajengea? kuna watu wanasema Makonda anajenga Mall fulani kule Mwanza je kuna ukweli wowote? naamini kauli ya waziri Mpango haikuwa sauti yake pekeee bali kuna kitu kinachomhusu jamaa kiko jikoni na kikiiva tutakiona mezani soon...ugonjwa sugu huanza taratibu na kutoka huwa ni taratibu pia
 
Mkuu Techinically umeandika jambo zito na lenye kuhitaji akili zinaoongozwa na utaifa kwanza.

Ni kweli kabisa RC alikosea kwa kutotengeneza mazingira ya kuhakikisha huo mzigo unakombolewa bandarini, kabla hata meli haijaondoka kutoka huko ilipotoka.

Tunafanya masikhara kwenye mambo ya maana na tunapenda kujifanya tupo makini kwenye mambo ya kipuuzi. Tumeukumbatia ujinga mpaka tunashindwa kutofautisha kati ya akili zenye faida na ujinga wenyewe.

Hizo furniture zingeleta kitu fulani kipya kwenye shule za Dar lakini kama kawaida siasa za kipumbavu ndio zinapewa nafasi.

Kinachonishangaza ni kwa nini mpaka leo hili swala lipo pending wakati RC ana 'baraka' zote baada ya kushataki kwa Rais?. Kama tumeamua kufanya mambo kinyume na sheria, ni bora tuyasikie tu kama taarifa kwamba yamefanyika , badala ya kupiga danadana kana kwamba kutakuwa na mabadiliko!
 
Tusipindishe sheria kwa mgongo wa huruma kila mtu akija kwa njia hiyo nani atalipa kodi?

Kwanini hujawahi kutetea kodi ambazo zinawaumiza wananchi wa kipato cha chini na hata kupandisha gharama za maisha yao leo unamtetea mtu mmoja ambaye kwa mujibu wa taratibu amekiuka na sheria inachukua upande wake kwanini kwa huyu sheria unataka iwe na huruma kwa wengine isiwe nayo?

Acha sheria ifuate mkondo wake ili na wao wafeel namna inavyoumiza huenda watapata uelewa wa kutunga sheria vizuri
Kwani hao hayo wanayajua kipindi kile mbunge lema zile ambulance zilipozuiliwa bandarini hadi alipe kodi wakati hazikutakiwa hao hao ndio walikuwa wakishangilia kuwa sheria lazima ifuatwe,akazilipia leo ni mwenzao ndio wanatumia kuwa SHERIA YA BUSARA itumike??hiz double standard za nini??mambo haya huwezi kuyakuta kwa wazungu hata siku moja!!
 
Mkiendekezi hii tabia, ipo siku mtu ataingiza mizigo yake kwa style hii ambayo kwanza hakuna mwenye uhakika kama vifaa hivyo vyote kweli vinawafia walengwa au ni janja tu.

Na kwa jinsi jambo hili linavyokwenda mpaka sasa, ni dhahiri unahitajika uchunguzi wajulikane ni kina nani walituma vifaa hivyo na shule gani hasa zilizolengwa kupewa hiyo misaada.

Hili jambo lina ukakasi unaohitaji uchunguzi maana huenda si kila kifaa kitaenda kutolewa kama msaada.

Na nikwambie tu, vifaa hivyo vingekuwa vimeingizwa na mtu kutoka upinzani, vingeshapigwa mnada siku nyingi tena huyo Makonda angeweza hata kuingilia viuzwe haraka japo kisheria hahusiki.

Tena namshauri waziri Mpango awe makini na kama kuna mtu atamshinikiza atoe msamaha,basi ahakikishe mtu huyo anatoa agizo kwa njia ya maandishi vinginevyo ajiuzulu kwani ipo siku anaweza kuja kujikuta anawajibika kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuikosesha serikali mapato.

Wanasiasa sio watu hawachelewi kukugeuka.

Tukumbuke sheria tunatunga wenyewe na kuzipitisha kwa mbwembwe.

Swali: Iweje leo tuzione chungu?

Tunavuna tulichopanda.
sio ipo siku ataingiza.. TIARAEI wameustukia ule mzigo ulikuwa na vitu visivyohusika na shule. vitanda makabati ya hotelini na shule wapinawapi... tujiulize tu hivi huyu bashite ile elimu yake ya FA FA FA FA ulitegemea angekuwa na ujanja wa kufanya aliyofanya? katumia usanii wa kizamani ndo mana kafeli wewe ni mtumishi wa sirikale sheria za kazi kwani hazijui? na kwanini hakuzifuata ? wajanja wa gsm wamemingiza chaka imekula kwake.. ntamshanga SIZONJE akiendelea kulea yaiVIZA
 
Kwani hao hayo wanayajua kipindi kile mbunge lema zile ambulance zilipozuiliwa bandarini hadi alipe kodi wakati hazikutakiwa hao hao ndio walikuwa wakishangilia kuwa sheria lazima ifuatwe,akazilipia leo ni mwenzao ndio wanatumia kuwa SHERIA YA BUSARA itumike??hiz double standard za nini??mambo haya huwezi kuyakuta kwa wazungu hata siku moja!!
HUYU BWANA ALIZUIWA KUTOA HII GARI YA WAGONJWA ALIYOILETA KUSAIDIA JAMII ETI MPAKA ALIPE KODI YA SIRIKALE.
HAKA KABASHITE KAMELETA KONTENA 20 KANATAKA KATOE BURE NYAMBAAAFFFFFFFFFFFFFFFFFF!!
Ambulance%2BLema3.jpg
 
Yani hapa ndo Wana ccm wameshindwa wawe wapi either kwa RC or Waziri.
Mana unaweza ukawa kwa Wazira yakamkuta ya Nape wakashindwa kula matapishi yao, wakawa kwa RC ukasikia amepangiwa majukumu mengine? Niwashauri tu Wana ccm mlivyokua ni wafuata upepo kuweni tu katikati uku mkisubri Baba yenu ataamua nini, ili atakako favor ndo muende uko.

Sent using Jamii Forums mobile app
kujificha nyuma ya walimu ni utoto changamoto za walimu zilikuwepo na zitaendelea kuwepo. Ila Kuna kitu watu hawakijui, kuna siri katika makontena hayo just wait time will tell! ujanja ujanja una mwisho, lipa kodi uchukue biashara zako!
 
Back
Top Bottom