Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Hii nchi kuna baadhi ya watu vichwa vyao wanafugia nywele tu basi na awachelewi kusema wanaompinga Makonda ni wauza Unga tunachokisema walio wengi kufuata utaratibu katika kuagiza bidhaa nje ikaja kama mali yake binafsi baada kua ya umma ?
 
Kwenye hili Waziri ka kosea !. Hii mizigo imetumwa na Watanzania ni rahisi tu kuongea na watumaji na kubadilisha kutoka Makonda na kuweka jina la jiji au wizara ya elimu lakini kibaya ni kuuza vitu vya msaada wa elimu na watanzania walipiga box pale state ya Washington kupakia vitu vikatumike kwenye bar au mahoteli hii hatakuwa nzuri kwa nchi na kwa diaspora. Tatizo Watanzania tunapenda ushabiki kuliko hata watoto wetu
 
Paschal huwa nakuheshimu sana ila kwa hili tumia akili kwanza.Nilitarajia ufanye utafiti nakujiridhisha kujua nyuma ya pazia lakini hata Eagles wameshindwa kukwambia ukweli. Nakwambia mizigo hiyo wameweka vitu vya shule vichache lakini vitu vingi ni kwa matumizi ya hotel yake inayojengwa mwanza. Suala la walimu wa Dar Es Salaam linatumiwa lakini linakitu nyuma ya Pazia. Hivi hukumbuki simba wakati wanaenda kucheza chambion league africa walikwa wakienda na mipira mingi ila ikifika kule wanakokwenda basi mipila inachukuliwa wanapewa mingine. Huo wakati ilikuwa ndo ujanja wakuuza Gnada kwa wafadhili simba wa wakati huo.Sasa suala la vifaa vya Makonda kunakitu kikubwa nyuma ya Pazia. Kama shida ipo basi waliovitoa watoe na lisiti walipovinunua. Fuatalia kama utaona ukweli kama kuna watanzania wamechangia mzigo huo. Mbona container 16 zimesimanishwa kuja TZ na hao waliok markeani baada ya ngoma kugoma. Mbona Makonda aliikataamizigo mwanzoni alipohojiwa. Kunauchafu mwingi nyuma ya hii sakata. Waziri kahukua uamzi sahihi.

Kwa mujibu wa sheria ya karma, hakuna laana yoyote inayoweza kumpata mtu aliyenunua mali kihalali hata kama mali hiyo ni ya wizi au dhuluma, ila laana humpata yule aliyedhulumu, hivyo kwa case ya containers za Makando, laana itamhusu anayetoza kodi vitu vya bure vya masikini waalimu wetu!.

P.
 
WATANZANIA ACHENI UNAFIKI... Kwanza vifaa gani mpaka aagize nchi za nje, viwanda vya tz vfanye kazi gani.? KAMA TUNATOZWA KODI WANYONGE NA TUNALIPA NAYE AONJE NAMNA VINAVYOUMA
 
Yaani uvunje sheria halafu baadae uihalalishe. Upuuzi wa hali ya juu huo. Kwani serikali haijui vifaa vya elimu ni muhimu na ikaviwekea kodi?yaani utangulize huruma kwenye uvunjifu wa utaratibu uliowekwa na serikali unayoitumikia?! Tax exemptions hakuiona kabla ya kuagiza samani? Si tulijitolea samani mbali ×2 yakiwemo madawati dsm! Katika utaratibu wa kodi pia. Kujitolea kuchonga dawati moja nililopeleka msaada kwa shule yeyote bado kodi yangu imetumika na nimelipa kwa njia moja au nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo mengine yanatia kinyaa!

Makonda ali-mobilize watu(diaspora) kuchangia samani za shule. Wito ukaitikiwa kwa kuchangia na kuzisafirisha hadi Dar. Aliye-mobilise ni Makonda, ametumiwa Makonda akazikabidhi katika shule za serikali.

Suala hapa kama serikali ina wasiwasi na nia hii ya Makonda basi ifuatilie konteina moja moja kuhakikisha mizigo yote inagawiwa mashuleni na si vinginevyo!

Mara nyingi mizigo mingi inayotumwa kutoka nje kwenda kwenye taasisi za serikali jina la mtu wa kufuatilia (Attn. so and so) huandikwa! Hii inakuwa rahisi kwa mtumaji kupata uthibitisho wa mizigo kufika!

Sasa ni nini watu wenye PhD kinawachanganya hapa?
Hii imefafanuliwa vizuri Sana ktk Mada zinazohusiana na hili jambo mkuu, taratibu na sheria ambazo bunge letu tukufu liltunga ndo zinazofanya kodi idaiwe. Ushauri bunge linaanza tarehe ngoja wapeleke hoja ya dharula kuhusu hivyo vifaa tuirekebishe haraka tumpe akagawe shuleni. Fuata taratibu la sivyo utapata ngiri Sana.
 
Kwanza kwa mlio walimu mtanielewa ninaposema waziri kakurupuka wala hazijui changamoto za elimu
ukisikiliza kwa umakini kwenye hotuba yake ya juzi utagundua kabisa aelewi anachokiongea...

Anaongelea maswala ya elimu bure kitu ambacho ni nje kabisa ya mada ya makontena

swala hapa ni vifaa kwa ajiri ya kusaidia elimu ya dsm ambayo ina changamoto nyingi ikiwa na mrundikano wa wanafunzi na mambo kibao

Makonda inawezekana kuna sehemu alikosea katika mchakato huo lakini serikali walitakiwa kuwa wajanja wangeruhusu kwanza vitu viingie ndio waanze kuvimonitor wapate ushahidi wa kutosha ndio waje kumtuhumu.

matokeo yake wananchi nao wameyabeba na kusahau watoto wao ndio wanakaa chini milele
mimi niko na ushahidi kabisa nilienda shule moja na taasisi fulani kutoa msaada wa computer lakini unakuta walimu stafu viti tu vya kukalia haviwatoshi hii ni aibu kama mwalimu hana kiti stafu mwanafunzi je darasani itakuwaje?

tukiweka siasa pembeni Makonda yupo sahihi kabisa na ana nia njema ingawa anaweza kuwa kafanya makosa kutumia jina lake kwa ushauri mbovu wa watendaji waliopo chini yake lakini naamini tatizo letu la elimu ni kubwa mno kuliko jina la makonda kuwa kwenye makontenana hili swala tunalibabe kishabiki sana kama kawaida yetu...

kwamba mimi ni chadema Gambo akifiwa na mzazi wake nashangilia, mimi ni ccm Sugu akipata msiba nashangilia upuuzi mtupu.

Hivi waziri anavipiga mnada vitu vya shule za dsm watu tunashangilia leo halafu kesho jangwani secondary inakuwa ya mwisho tunaanza kumponda makonda ...

Hivi vitu vikinunuliwa na wafanya biashara sisi wananchi wa kawaida tutafaidika vipi direct kama ambavyo tungeviona kwenye shule zetu? namimi naongeza na alaaniwe kabisa atakae vinunua.

"Form four wanakaribia pia kuanza mtihani msisahau kuleta mrejesho hapa wa shule za umma"
How sure u are Makonda ana nia njema? Yan ww umejuaje kua ana nia njema? Niko interested kutaka kujua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwangu mtoa mada na makonda wote wamekurupuka. kila mtu akisema aagize nje mzigo kwa mgongo wa elimu hatutafika. utaratibu muhimu ufuatwe.
 
Mkiendekezi hii tabia, ipo siku mtu ataingiza mizigo yake kwa style hii ambayo kwanza hakuna mwenye uhakika kama vifaa hivyo vyote kweli vinawafia walengwa au ni janja tu.

Na kwa jinsi jambo hili linavyokwenda mpaka sasa, ni dhahiri unahitajika uchunguzi wajulikane ni kina nani walituma vifaa hivyo na shule gani hasa zilizolengwa kupewa hiyo misaada.

Hili jambo lina ukakasi unaohitaji uchunguzi maana huenda si kila kifaa kitaenda kutolewa kama msaada.

Na nikwambie tu, vifaa hivyo vingekuwa vimeingizwa na mtu kutoka upinzani, vingeshapigwa mnada siku nyingi tena huyo Makonda angeweza hata kuingilia viuzwe haraka japo kisheria hahusiki.

Tena namshauri waziri Mpango awe makini na kama kuna mtu atamshinikiza atoe msamaha,basi ahakikishe mtu huyo anatoa agizo kwa njia ya maandishi vinginevyo ajiuzulu kwani ipo siku anaweza kuja kujikuta anawajibika kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuikosesha serikali mapato.

Wanasiasa sio watu, hawachelewi kukugeuka.

Tukumbuke sheria tunatunga wenyewe na kuzipitisha kwa mbwembwe.

Swali: Iweje leo tuzione chungu?

Tunavuna tulichopanda.
Makosa ya Makonda:-

1. Kuingiza samani zenye thamani kubwa bila kufuata utaratibu.

[emoji117] Ili upate msamaha wa kodi, sharti uanze mchakato wa ndani, upate vibali ndiyo uagize mzigo wake, lkn yeye kwa kujiamini hakuomba popote.

2. Kwenda kinyume na sera ya serikali ya awamu ya tano kuwa, serikali hii haitoagiza samani kutoka nje ya nchi.
[emoji117] Hii ililenga kulinda bidhaa za ndani na kuongeza ajira(serikali ya viwanda). Makonda hataki viwanda, anataka sifa tu.

3. Mzigo kwa ajili ya shule za dsm, kuandikwa jina lake.
[emoji117] Kuna ofisa elimu wa jiji, au mkurugenzi wa jiji, au hata mkuu wa mkoa wa dar es salaam. Hii ingeleta maana, kwani hata angehama, mzigo ungebaki kwa wana dsm. Yeye alitaka hata akihamia mwanza au Koromije au akiacha kazi, au akigukuzwa, mzigo umfuate maana ni wake.
wa wa
4. Mzigo anao udai, aliwahi kuukana na kudai siyo wa kwake. Ameshindwa kueleza umeanza lini kuwa wa kwake.

5. Kosa kubwa ni kujitaftia umaarufu kuliko mungu wake. Yeye hapendi hbr hizo

6. Kuanza kutishia watu wengine kuhusu kontena hizo. Alisema atawashitak kwa rais wanaozuia mzigo wake, kaona haijatosha kawashitaki kwa mungu, na amekuwa akitoa vitisho. That's bad.

7. Aliagiziwa kontena 36, 16 hazipo bandarini lkn mgao wake hauonekani mashuleni.

Kama asingekuwa bashite(zero brain), ange:-

1. Fuata hizo taratibu kwanza. Akikataliwa, anachukua plan B
2. Plan B, ni kuwaomba wafadhili watume pesa, samani zitengenezwe nchini. Ajira zingemwagwa sana.

Samani za bilion 2, kwa tanzania, zingejenga/kutengeneza samani za kutosha nchi nzima.

Hivi, idadi ya madawati yaliyochongwa enzi za JK, thamani yake bei gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Busara inayotumika kusamehe wakwepa kodi ,itumike pia kwenye makontena haya ili walimu wasiendelee kukaa chini na kukalia viti vichafu.

Kama tatizo ni sheria hata mikutano ya vyama vya siasa ipo kikatiba lakini imepigwa marufuku na watu wameelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana mtazoea, haki lazima tuisimamia changie mlipe kodi, siasa mwaka kesho kutwa, hapa kodi tu
 
Ukifuatilia kwa makini habari hii utatoka na conclusion nyingi tofauti kama hizi:
1: kwanini mzigo woote yaani makontena 36 toka yatokako yawe addressed kwa jina la mtu? Maana yake ni kuwa mzigo ni kwake na sio wa ofisi yake!
2: aliwahi kuukana. Kuna kitu gani leo audai kwa maombi madhabahuni na laana kibao? Jibu ni kuwa mzigo ni wake mwenyewe na hauna mmiliki mwingine tofauti!
3: kuna tetesi kuwa kulikuwa na baadhi ya walimu japo hatujui kama kweli ni walimu waliwahi kuchukuliwa kwenda kuonyeshwa baadhi ya makontena 20 kwa nje lakini hawakuonyeshwa kilichokuwemo ndani. Hili linatia shaka kuwa kuna kinachofichwa na mwenye mzigo na huenda siyo samani za ofisi bali za hoteli zake au za kuuza kwenye maduka yake! Hili linawezekana kwa jinsi mazingira ya ushirika wake na wale pugu moll mart!
Kuna vijihoja ambavyo mtu makini anaviona waziwazi na kumsukuma kufanya maamuzi ya kutokuona sababu za kutoa msamaha kwani mzigo wenyewe umekaa kibinafsi sana. Namshauri afanye yafuatayo:
i: ajiuzulu.
ii: alipe kodi
iii: aache kuitumia ofisi ya umma kujifanyia kampeni za kisiasa!
 
Hakuna aliye kinyume na uboreshaji elimu, Dar kuna shule ngapi? Viti vimekuja kwa ajii ya shule gani? Taasisi gani ya elimu imewekwa kama client? kama ni vya taasisi yoyote basi Mpango aache, lakini kama ni vya kwake mwenyewe, Makonda atuwie radhi walimu
 
mkuu umeviona thamani zenyewe vyenyewe...

kwa mwenekano tu vinafaa vitumike shule zenye miuondombinu ya kisasa kama Kaizilege, St Marian, Tusiime, Barbo n.k..

mm navaki kujiuliza kwa namna majengo na namna miundombinu ilivyo, ofis kukosa umeme na sillingboard, madilisha n.k..

how comes hizo furnitures zitaweza kustay for a long?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Techinically umeandika jambo zito na lenye kuhitaji akili zinaoongozwa na utaifa kwanza.

Ni kweli kabisa RC alikosea kwa kutotengeneza mazingira ya kuhakikisha huo mzigo unakombolewa bandarini, kabla hata meli haijaondoka kutoka huko ilipotoka.

Tunafanya masikhara kwenye mambo ya maana na tunapenda kujifanya tupo makini kwenye mambo ya kipuuzi. Tumeukumbatia ujinga mpaka tunashindwa kutofautisha kati ya akili zenye faida na ujinga wenyewe.

Hizo furniture zingeleta kitu fulani kipya kwenye shule za Dar lakini kama kawaida siasa za kipumbavu ndio zinapewa nafasi.
Una akili sana
 
hivi vitu ni vya Hotel yake ya Mwanza mambo ya kusema eti ni vifaa vya shule ni uongo ingekuwa kweli ni siku nyingi sana angekuwa amevitoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Y
Jamani eh. Kodi nayo ikilipwa si itaingia uko uko katika kusaidia elimu, kununua madawa hospitalini, kujenga miundombinu n.k sasa kwanini isilipwe ili ata watu wasio wakazi wa Dar es Salaam wafaidike

Sent from my SM-G610F using Tapatalk
Yaani muagize nje wanufaike wa nje halafu huku msilipe kodi, raisi alichasema Tanzania ya viwanda hakusema maana yake muagize viti nje alimaanisha muwape mafundi wa ndani ajira humuhumu, walipe kodi humhumu, mgawanjo wa hayo mapato yafanyike humhumu nchi isonge. Msaidieni harambee mlipe kodi, tuwape mameza yenu. Hamtaki tunauza na laana hatupati hata mmu hawatugusi. Manake wengine wameenda hija saudia, wengine juzijuzi Jerusalem kwa hiyo hizo laana zitakuwa Zabibu kwa watakanunua tu. Akilaani kule meza yako inajaa Zabibu zingine unawapa wenzio. Msihofu kabisa nunua meza za makonda tujenge nchi yetu.
 
Back
Top Bottom