Mkiendekezi hii tabia, ipo siku mtu ataingiza mizigo yake kwa style hii ambayo kwanza hakuna mwenye uhakika kama vifaa hivyo vyote kweli vinawafia walengwa au ni janja tu.
Na kwa jinsi jambo hili linavyokwenda mpaka sasa, ni dhahiri unahitajika uchunguzi wajulikane ni kina nani walituma vifaa hivyo na shule gani hasa zilizolengwa kupewa hiyo misaada.
Hili jambo lina ukakasi unaohitaji uchunguzi maana huenda si kila kifaa kitaenda kutolewa kama msaada.
Na nikwambie tu, vifaa hivyo vingekuwa vimeingizwa na mtu kutoka upinzani, vingeshapigwa mnada siku nyingi tena huyo Makonda angeweza hata kuingilia viuzwe haraka japo kisheria hahusiki.
Tena namshauri waziri Mpango awe makini na kama kuna mtu atamshinikiza atoe msamaha,basi ahakikishe mtu huyo anatoa agizo kwa njia ya maandishi vinginevyo ajiuzulu kwani ipo siku anaweza kuja kujikuta anawajibika kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuikosesha serikali mapato.
Wanasiasa sio watu, hawachelewi kukugeuka.
Tukumbuke sheria tunatunga wenyewe na kuzipitisha kwa mbwembwe.
Swali: Iweje leo tuzione chungu?
Tunavuna tulichopanda.
Makosa ya Makonda:-
1. Kuingiza samani zenye thamani kubwa bila kufuata utaratibu.
[emoji117] Ili upate msamaha wa kodi, sharti uanze mchakato wa ndani, upate vibali ndiyo uagize mzigo wake, lkn yeye kwa kujiamini hakuomba popote.
2. Kwenda kinyume na sera ya serikali ya awamu ya tano kuwa, serikali hii haitoagiza samani kutoka nje ya nchi.
[emoji117] Hii ililenga kulinda bidhaa za ndani na kuongeza ajira(serikali ya viwanda). Makonda hataki viwanda, anataka sifa tu.
3. Mzigo kwa ajili ya shule za dsm, kuandikwa jina lake.
[emoji117] Kuna ofisa elimu wa jiji, au mkurugenzi wa jiji, au hata mkuu wa mkoa wa dar es salaam. Hii ingeleta maana, kwani hata angehama, mzigo ungebaki kwa wana dsm. Yeye alitaka hata akihamia mwanza au Koromije au akiacha kazi, au akigukuzwa, mzigo umfuate maana ni wake.
wa wa
4. Mzigo anao udai, aliwahi kuukana na kudai siyo wa kwake. Ameshindwa kueleza umeanza lini kuwa wa kwake.
5. Kosa kubwa ni kujitaftia umaarufu kuliko mungu wake. Yeye hapendi hbr hizo
6. Kuanza kutishia watu wengine kuhusu kontena hizo. Alisema atawashitak kwa rais wanaozuia mzigo wake, kaona haijatosha kawashitaki kwa mungu, na amekuwa akitoa vitisho. That's bad.
7. Aliagiziwa kontena 36, 16 hazipo bandarini lkn mgao wake hauonekani mashuleni.
Kama asingekuwa bashite(zero brain), ange:-
1. Fuata hizo taratibu kwanza. Akikataliwa, anachukua plan B
2. Plan B, ni kuwaomba wafadhili watume pesa, samani zitengenezwe nchini. Ajira zingemwagwa sana.
Samani za bilion 2, kwa tanzania, zingejenga/kutengeneza samani za kutosha nchi nzima.
Hivi, idadi ya madawati yaliyochongwa enzi za JK, thamani yake bei gani?
Sent using
Jamii Forums mobile app