Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Mkuu Techinically umeandika jambo zito na lenye kuhitaji akili zinaoongozwa na utaifa kwanza.

Ni kweli kabisa RC alikosea kwa kutotengeneza mazingira ya kuhakikisha huo mzigo unakombolewa bandarini, kabla hata meli haijaondoka kutoka huko ilipotoka.

Tunafanya masikhara kwenye mambo ya maana na tunapenda kujifanya tupo makini kwenye mambo ya kipuuzi. Tumeukumbatia ujinga mpaka tunashindwa kutofautisha kati ya akili zenye faida na ujinga wenyewe.

Hizo furniture zingeleta kitu fulani kipya kwenye shule za Dar lakini kama kawaida siasa za kipumbavu ndio zinapewa nafasi.
Hujui ulisemalo! Hizo fanicha ni za GSM
 
Hivi sheria inasemaje? Kama hvyo vifaa havina msamaha basi mjadala umeisha maana sheria haichagui.
Siku kwa mfano mtu ameazisha shule yake ana leta vifaa asilipe kodi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema wana wivu sana na Makonda lakini mkae mkijua amewaacha mbali sana na saco cos yenu
JAMANI Kumbe waziri na TRA iko chini ya CDM jamani chadema mpeni huyo makontena yake ili mcwe na wivu sana kweli akili ni nywele na wewe unazako////////
 
Mkuu Techinically umeandika jambo zito na lenye kuhitaji akili zinaoongozwa na utaifa kwanza.

Ni kweli kabisa RC alikosea kwa kutotengeneza mazingira ya kuhakikisha huo mzigo unakombolewa bandarini, kabla hata meli haijaondoka kutoka huko ilipotoka.

Tunafanya masikhara kwenye mambo ya maana na tunapenda kujifanya tupo makini kwenye mambo ya kipuuzi. Tumeukumbatia ujinga mpaka tunashindwa kutofautisha kati ya akili zenye faida na ujinga wenyewe.

Hizo furniture zingeleta kitu fulani kipya kwenye shule za Dar lakini kama kawaida siasa za kipumbavu ndio zinapewa nafasi.
Siasa vipi?Barua ya Mpango kwenda kwa RC inatembea mitandaoni umeisoma?
IMG_20180829_195120.jpg
IMG_20180829_195122.jpg
IMG_20180829_195136.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni kweli vifaa hivyo ni kwa ajili ya shule, serikali ifanye yafuatayo:
1. ifuatilie kujua vilikotoka na staili iliyotumika kuvisafirisha;
2. Makondo ale kiapo kwamba vifaa hivyo ni kwa ajili ya mashule ya Dar es Salaam ili kuepuka kugeuziwa kibao;
3. ivipe msamaha wa kodi;
4. ihakikishe kwamba vinagawiwa vyote mashuleni kwa kumshirikisha yeye (Makonda).
Vinginevyo, mivutano hii itagawa chama na serikali. Kumbukeni tunajenga nyumba moja na hatuna sababu za kugombania fito!
Jitafakarini!
Kiapo alishakula akiwa anaapa kuwa DC then RC.
Sheria ipo.
Ifatwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SAKATA LA MAKONTEÑA YA MAKONDA KUPIGWA MNADA LITIZAMWE UPYA

Na: Mtetezi wa Wanyonge.

Nimemsikia Waziri Mipango akisema kuwa Lazima Makontena hayo Yalipiwe Kodi ama yapigwe Mnada ili serikali ipate Kodi yake...

My Take

Tukumbuke kuwa Makontena hayo ya Vifaa ni Watanzania wenzetu wamejitolea na ndiyo maana hakuna kiwanda kilichopewa tenda hiyo na huo ni msaada kama alivyopata misaada ya Miguu Bandia, Ujenzi wa Hospital, Viwanja vya Mpira, magari ya Police , Pikipiki, Computer [emoji335] na vingine vingi alivyowai kufanya.

Makonda aliomba Samani si kwa faida yake bali kwa faida ya Watanzania na Kuipunguzia Serikali mzigo wa Manunuzi ya Vifaa hivyo.

Leo Kigezo Kimekuwa SHERIA! Sawa lakini Sheria zinatungwa, kusomwa na kutafsiriwa na wanadamu na bado huacha mwanya wa busara kutumika na kila kesi huamliwa kulingana na mazingira na ushahidi wake. (Ndio maana kuna Dissenting decision/Opinion and or Consential/Concurring Opinion)

Na Ikumbukwe Kuwa Sheria ya kodi inaruhusu busara kutumika pale inapoonesha kuwa vitu au mali zitatumika kwa manufaa ya jamii ya wanyonge na sio mtu binafsi.

Ikiwa Makanisa, NGOs nk. Kila kukicha yanapewa misamaha ya kodi kwa idhini ya MaRC na MaDC kulikoni hasa haya Makontena ya Viti vya Walimu? Computer za Shule? Meza na nk...?

Nikweli Yalitumwa kwa Jina la Paul Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Lakini kampeni yake Iko wazi tangu awali na si ya kificho, Walioyatoa walitamka wazi ni ya nini na hayana faida kwa Makonda bali kwa Taifa na Watu wake hasa Wanyonge walio wengi.

Sasa Msuguwano Huu unatoka wapi?
Hiyo Kodi Ni Bei gani?
Kodi inadaiwa hapo inathamani Kubwa kuliko Samani ya hivyo Vifaa?
Hiyo Kodi Inaweza kununua vifaa vyote hivyo?
Haya Vikipigwa Mnada Serikali itapata Bei Gani? Hiyo Bei Inaweza kununua Samani zote hizo?

Tusing'ang'ane na Sheria inayotupotezea kingi zaidi kwa Kukomalia Kodi nakupoteza Mali Kubwa zaidi ya Kodi, Hekima na Busara zinaweza Tatua hili kwa Kukaa nakujadili Faida na Hasara za Kodi, Faida na Hasara zakuendelea kuwa na Vifaa hivyo, Faida na Hasara za Vifaa hivyo Kuingia kwenye Majengo yanayongoja Vifaa na Wanyonge kuvitumia.

RC Makonda Ameomba Misaada Majengo yamejengwa yanahitaji Samani, Serikali Imesaidiwa na Wazalendo wa Taifa hili waishio ughaibuni kwanini Tuwafanye wajione hawana Thamani kwa Kujitoa kwao kusaidia Nchi yao?

Mh Waziri Mipango na Wasaidizi wako na Watu wa TRA mlitizame Upya Jambo hili.

Mlio Karibu na Mh Rais Fikisheni Kilio cha Wanyonge wakatumie Vifaa hivi.
Iko Misamaha Mingi sana ya Kodi Kupitia Vifaa hivyo kuwa Vinaenda kuhudumia Jamii basi Dhamila Kuu ikatimie kwa Vifaa hivyo Kusamehewa Kodi na Vikatumike Mashuleni.

Mnyonge Mnyongeni haki yake Mpeni!
Hapa Hatumkomoi Makonda ila Tunataka Kuwakomoa Walimu na Watoto wa Shule wenye uhitaji wa Vifaa hivyo.

Sakata la Makontena Liangaliwe upya kwa Maslahi Mapana ya Taifa Hili na Wanyonge wenye Uhitaji wa Vifaa hivyo.

Waziri Mipango Fanya Mipango Vifaa viwafikie Wanyonge bila Kodi, Manake hata Mkisema Kodi ilipwe analipa nani?
Makonda aloomba kwa Niaba ya serikali?

Au Tuwaombe Pesa Walotupa Msaada tena wao Ndo walipe Kodi tena?
DAFI ..YOU NEED TO THINK BEYOND WHAT YOU HEAR.. WALIOTUMA MAKONTAINA HAYO MBONA WAMEZUA MENGINE 16 WAKTI YALIISHAANZA SAFARI. KUNAKITU NYUMA YA PAZIA.


Kwani Tunataka Kumfurahisha nani katika hili? Au Kumkomoa Nani katika Hili?

Wanaoteseka ni Walimu na Watoto wa shule, Misuli tunayotunishiana Viongozi Haitusaidii sisi watanzania kwa ujumla.

Kodi na Mnada kwa Vifaa hivyo Vyote vinatuumiza kwani Vinapelekea Kupoteza Vifaa vyenye uhitaji kwa wanyonge.

Kodi tunazikusanya ili Tununue Vifaa vya Shule, Leo Hii Vifaa Vimekuja Buree na Vingi vyenye ubora zaidi sisi hatuvitaki kisa Kodi.

Inasikitisha sana hii Hali....


Tunaomba Viongozi walitizame upya jambo huli.

Makontena haya Faida kwa Mkonda zaidi ya Faida kwa Wanyonge na Serikaki yao ambao wanahitajika Kuhenyeka kwa Mika kadhaa huku wakilipa kodi ndo waweze kununua Vifaa vyote hivyo.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli Makonda alikosea kwenye kuandika Bill of lading -ila, kwa kuwa inaeleweka vifaa vilikuwa kwa ajili ya shule za Dar es Salaam, busara ilikuwa ni kupokea na kukaa na Makonda kumwelimisha. Halafu serikali ingesimamia kuhakikisha kuwa beneficiaries wa vifaa hivyo ni exclusively shule za Dar es salaam
Muwe mnaelewa.
Kama una "Elimu ya Kubangaiza" like Makonda utapata uzito kuelewa.
Unataka aelimishweje yaani?
IMG_20180829_195120.jpg
IMG_20180829_195122.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
NYIE WATETEZI TUNAOMBA MTUAMBIE, YALE 16 ALIYOKWISHA YATOA BANDARINI YAKO WAPI? JE, MMESHAWAHI KUONYESHWA HATA WAKATI ANAGAWA HIVYO MNAVYOVIITA VIFAA VYA ELIMU
 
Hakuna anayetaka kumnyang'anya Makonda makontena yake, Yeye alipie kodi tu basi, kwa kufanya hivyo atakuwa ni mzalendo zaidi kwa sababu mbili

(1) Kalipa kodi, kaisaidia nchi hela za kununua dawa, kujenga shule, barabara etc

(2) atakuwa amesaidia vifaa vya elimu

Hapo si itakuwa poa zaidi?
 
Chadema wana wivu sana na Makonda lakini mkae mkijua amewaacha mbali sana na saco cos yenu

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu ni wewe halisi. Hatimaye umeshindwa kuficha ujinga wako ukaamua kuuanika wazi

TRA ni ya Chadema?
Kuna madarasa na ofisi nyingi za walimu Dar zinajengwa kwa juhudi binafsi za Makonda
JKT wamejitolea kujenga bure hizo ofisi .

Ngoja ziishe kujengwa alafu walimu wataenda kukaa chini humo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa ulichangia kama gentleman, I doubt sio wewe....kuna mtu alikushikia simu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makonda karipotiwa kusema watakaonunua makontena hayo watalaaniwa, Waziri kampaka Makonda, halafuMakondakaoneshwa kwenye TV akisemahana habari za makontena hayo.

Bongo Movie kwa hisani ya Serikali.
 
Kwanza kwa mlio walimu mtanielewa ninaposema waziri kakurupuka wala hazijui changamoto za elimu
ukisikiliza kwa umakini kwenye hotuba yake ya juzi utagundua kabisa aelewi anachokiongea...

Anaongelea maswala ya elimu bure kitu ambacho ni nje kabisa ya mada ya makontena

swala hapa ni vifaa kwa ajiri ya kusaidia elimu ya dsm ambayo ina changamoto nyingi ikiwa na mrundikano wa wanafunzi na mambo kibao

Makonda inawezekana kuna sehemu alikosea katika mchakato huo lakini serikali walitakiwa kuwa wajanja wangeruhusu kwanza vitu viingie ndio waanze kuvimonitor wapate ushahidi wa kutosha ndio waje kumtuhumu.

matokeo yake wananchi nao wameyabeba na kusahau watoto wao ndio wanakaa chini milele
mimi niko na ushahidi kabisa nilienda shule moja na taasisi fulani kutoa msaada wa computer lakini unakuta walimu stafu viti tu vya kukalia haviwatoshi hii ni aibu kama mwalimu hana kiti stafu mwanafunzi je darasani itakuwaje?

tukiweka siasa pembeni Makonda yupo sahihi kabisa na ana nia njema ingawa anaweza kuwa kafanya makosa kutumia jina lake kwa ushauri mbovu wa watendaji waliopo chini yake lakini naamini tatizo letu la elimu ni kubwa mno kuliko jina la makonda kuwa kwenye makontenana hili swala tunalibabe kishabiki sana kama kawaida yetu...

kwamba mimi ni chadema Gambo akifiwa na mzazi wake nashangilia, mimi ni ccm Sugu akipata msiba nashangilia upuuzi mtupu.

Hivi waziri anavipiga mnada vitu vya shule za dsm watu tunashangilia leo halafu kesho jangwani secondary inakuwa ya mwisho tunaanza kumponda makonda ...

Hivi vitu vikinunuliwa na wafanya biashara sisi wananchi wa kawaida tutafaidika vipi direct kama ambavyo tungeviona kwenye shule zetu? namimi naongeza na alaaniwe kabisa atakae vinunua.

"Form four wanakaribia pia kuanza mtihani msisahau kuleta mrejesho hapa wa shule za umma"
Kwa nature ya shule za Tanzania zile furniture zisingekuwa na msaada wowote, those were office furniture and not designed for schools.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom