Your Majesty
JF-Expert Member
- Aug 29, 2018
- 3,242
- 5,345
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda jana alifanya ibada maalum kanisani kwa ajili ya makontena yake yenye samani za shule yanayoshikiliwa na TRA
Katika ibada hiyo Makonda alionya watakao nunua makontena yake watapata laana kali
Pia aliwarushia dongo TRA akisema ni watu wabaya wasio na huruma na kudai kuwa wanamchukia Makonda
"Kama wanachukia Makonda waondoe nembo ya majina yangu kwenye makontena hayo" alisema Makonda
Ni mara nyingine viongozi wa serikali wanasuguana na taasisi za serikali katika kutekeleza majukumu yake huku kiongozi huyo wa mkoa akihisi anaonewa na ni wivu unaofanywa na TRA kisa anafanya vizuri katika mkoa wake
Juzi Paul Makonda alikaririwa na vyombo vya habari kuhusu kupigwa mnada makontena yake,akisema yeye hatishiki na ni mlima hawezi kuyumbishwa na wale wasiomtakia mema katika harakati zake za maendeleo ya Dar es salaam
Kwa hali ilivyo sasa ni dhahiri kuwa Makonda analaumu serikali kumhujumu na hakubaliani na TRA na mambo inayomfanyia
Halafu kama vilikuwa vifaa vya elimu iweje vije kwa jina lake?? Halafu mme angalia vyema vilivyomo kwenye zile container au wana amua tuu kumtetea Makonda?? Maana vifaa vilivyomo sio vya shule kama inavyo semwa
Sent using Jamii Forums mobile app
Ok, nadhani wewe ni sehemu ya wafanyakazi wa GSM.
sababu kubwa ni kwamba Makonda ndiye mnyonge wa GwajimaHaya mambo ya kumshambulia Makonda, ndio yanafanya hata mamlaka zinazomsimamia zishindwe kumwajibisha maana HAZIPANGIWI!
Sasa kama ni kweli haya, Mch. Gwajima yanamhusu nini kuingilia ugomvi ambao hata kwa mbali hayamhusu?
Kwa nini tusiseme haya mashinikizo kwa Makonda yana ajenda ya siri ya kisiasa?
Anaweza akawa kweli Makonda amefanya siyofaa kufanywa juu ya zogo hili, lakini je ni sahihi kwa Mtumishi wa Mungu Gwajima kuyaingilia namna hii?
Kwa nini kina Askofu Shoo au Kina Ruwaichi hawajiingizi katika sakata hili la Makontena?
Wakati mwingine Gwajima nae anavuta bangi!
mzee baba amejitoa na ameweka wazi kodo ilipweMimi sipangiwi hapo unaponishauri ndio unaharibu kabisaaa-Mzee Baba.
Nimejinukuu mwenyeweHongera sana Mh JPM kwa kuachana na huyu kilaza anayeshindwa na Mkoa wa Dodoma kimapato halafu anataka kuendelea kukwepa kodi. Naamini kwa umakini wako utakuwa umejifungia ukitafuta jina la RC bright wa kuongoza DSM
Hahaaa kamaliza kama ulivyoombaINASIKITISHA sana serikali yaani TRA kumhujumu Makonda ili hali ni jasho la wana DIASPORA waliojitolea kwa ajili ya maendeleo ya wa Dar es salaam , watu wamejinyima ili kuletea watanzania maendeleo na sasa yanakwamishwa kwa sababu ya wivu sie wana diaspora mnatuvunja moyo kabisa .Tuanaomba kwa dhati Rais aingilie kati jambo hili kwa mstakabali wa maendeleo ya Mkoa wa Dar es salaam. Chonde Mheshimiwa Raisi tuko chini ya miguu yako tusaidiwe tumalize jambo hili mkoa wa Dar ufaidi matunda ya wana Diaspora.
Kwa matamshi hayo sina budi kusema kwamba ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA. Kukosa elimu ni sawa na ndege isiyokuwa na rubani.