Gabeji
JF-Expert Member
- Sep 10, 2024
- 1,530
- 1,903
Tanzania ina viongozi vijana wachache sana wenye moyo wa kujituma, na kubuni fursa mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Binafsi mh Makonda nikiaangalia kwa jicho la tatu, ni kiongozi bora kwa Tanzania.
Huyu kila nafasi anafaaaa, kwa sababu huwa anafanya ubunifu wa hali ya juuu sana angepewa uwaziri wa Kazi bila shaka angepunguza gap la ajira nchini.
Mungu akupe maisha marefu Paul Makonda, wewe pia ni tunu ya Taifa.
==
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda, amekutana na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Bishwadip Wey, kujadili fursa mbalimbali kwa vijana wa Arusha. Miongoni mwa mambo waliyoafikiana ni kongamano kubwa la Artificial Intelligence (AI) litakalofanyika Mei 2025, ambapo mtaalamu kutoka Marekani atatoa elimu kwa vijana wa mkoa huo.
Mazungumzo yao pia yamejumuisha ushirikiano wa Arusha na chuo cha Zanzibar kinachofadhiliwa na Serikali ya India ili kuimarisha matumizi ya AI katika kazi mbalimbali. Aidha, wamekubaliana kuanzisha kilimo cha mitishamba kwa ajili ya dawa za asili, ufadhili wa masomo kwa vijana 1,000 nchini India, na mafunzo ya upishi kwa wapishi 50 wa Kitanzania kujifunza mapishi ya Kihindi ili kuvutia watalii.
Fursa nyingine muhimu ni kuimarisha kilimo cha maembe kwa ajili ya soko la India, nchi ambayo ina mahitaji makubwa ya unga wa maembe. Hatua hizi zitawanufaisha vijana wa Arusha kwa kuwapatia maarifa, ajira, na fursa za biashara zinazotokana na ushirikiano huu wa kimataifa.