Makonda awataka wananchi kutulia na kutotangaza Mgonjwa wa Corona kwani hawana mamlaka

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,566
Reaction score
4,013
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda amesema Mwananchi wa kawaida hana ruhusa ya kutangaza kuwa mtu ana #Coronavirus kisa umemuona Hospitali kwani Mamlaka hayo anayo Waziri wa Afya, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais

Amesema “Mkoa wangu ndio unaongoza kwa wajuaji, sasa niwaombe msilete ujuaji, kwenye hili janga la #COVID19, tujifanye wajinga kidogo ili tupone. Hata kama una mpenzi wako hamjakutana mwezi mzima vumilia.”

Aidha, amesema vifaa vya kupimia vinakuja Jijini Dar muda si mrefu kwani amewasiliana na Watu wa China kupitia kwa Balozi na wamekubali kuleta vifaa hivyo

Pia, amemuomba Wazira wa Fedha, Philip Mpango apunguze au kuondoa kodi kwa malighafi kutoka nje zinazotumika kutengeneza Sanitizer ili kuhakikisha viwanda vyetu vinaendelea kutengeneza na zikauzwa kwa bei nafuu
 
Hahaha hii carina itatuchemsha mpaka basi. Jamani eeh namimi nna carina ukisoma upuuzi wangu tu unalo.
 
Kama wewe ni RC si waziri wa afya unaagiza vifaa vya kupimia virusi vya CORONA huo ni ujuaji au Ulugola?
 
Huyo mkuu wa mkoa wa arusha anatangaza yeye ana mamlaka gani wakati waziri husika yupo
 
Hivi na yeye ana mamlaka ya kutangaza hizi taarifa ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…