Makonda na Musiba, Magufuli hayupo. Je, mmejiandaa kisaikolojia?

Makonda na Musiba, Magufuli hayupo. Je, mmejiandaa kisaikolojia?

Duh Mambo haya Kuna Mzee Mmoja Nae amekua akinyanyasa sana Watumishi anasema Mambo kibao kwamba yuko karibu na Mkuu.Nae sijui atafanyaje ametesa sana wananzengo pale Ofisi ya Mtumba .
Bado waovu wamebaki hawaishagi hawa. Moja linakufa lingine linazaliwa.
 
Kifo cha rais John Pombe Maguli ni pigo kubwa kwa taifa na Afrika kwa ujumla. Ni rais ambaye amejijengea sifa, maadui hata marafiki. Tanzania, bila unafiki wala kificho itamkumbuka baada ya mwanzilishi wake Mwl Julius Nyerere...
Kangi Lugola anafaa?
 
Weka akiba ya maneno mkuu, mama samia anamkubali makonda sana na atamrudisha kwenye mfumo
Makonda wa enzi ya Magufuli hatarudi tena. Narudia, hatarudi tena. Hata akipata uteuzi atakuwa Makonda asiye na nguvu kubwa kama ile aliyokuwa analindwa na walinzi na kutembea na msafara huku kila mtu akimnyenyekea
 
Hapa namzungumzia Makonda wa enzi za Magufuli,

Makonda yule aliyekuwa akifoka mawaziri wanakaa kimya, Makonda aliyekuwa akilindwa zaidi ya VP Samia,
Makonda aliyekuwa anatukana kila aliyekuwa kinyume na mawazo yake.

Makonda yule aliyevamia Clouds na walinzi kutoka Mweweni pamoja na CCTV camera kumnasa na Nape kutaka kuliingilia akiwa waziri wa habari matokeo yake akatolewa kitini.

Makonda aliyekuwa akitembea na msafara mrefu wenye Ving'ora, alikuwa zaidi ya RC.
Makonda yule mwenye kiburi na dharau.

Kwa sasa hata kama akipewa uteuzi atakuwa mpole kama kondoo, jeuri hiyo sidhani kama atakuwa nayo tena, Makonda wa JPM hatatokea tena.

Musiba byebye
 
Back
Top Bottom